Huu mti unaitwaje kwa kiswahili?

Huu mti unaitwaje kwa kiswahili?

Hahahahaha umewahi kutumia mafuta yake maa?

Naam, mamii nnayajuwa mafuta yake na sikuyatumia mimi binafsi bali Marehem bibi yangu alikuwa/nilikuwa nikimpaka miguuni akiyatumia kwa miguu kufa ganzi.

Pia huu mti leo ndiyo moja ya chanzo cha "diesel" itokanayo na mimea.
 
Farkhina kwani we upo nchi gani kwa sasa? Huu mti ni mnyonyo au mbarika.
Mama alikua akinikanda enzi zile nishaumia mpirani naye akinipa huduma kwa majani yake. Na mafuta yake pia ni dawa.
 
Farkhina kwani we upo nchi gani kwa sasa? Huu mti ni mnyonyo au mbarika.
Mama alikua akinikanda enzi zile nishaumia mpirani naye akinipa huduma kwa majani yake. Na mafuta yake pia ni dawa.


Anakukandia kwa majani yake?
 
Huo ni mnyonyo majani yake ni tiba sana kwa watoto ambao hawapati choo ...yanatwangwa yanakuwa kama kisamvu unamuwekea nyuma mtoto dakika tano ni nyingi mtoto anapata haja kubwa lkn yana maumivu
 
Huo ni mnyonyo majani yake ni tiba sana kwa watoto ambao hawapati choo ...yanatwangwa yanakuwa kama kisamvu unamuwekea nyuma mtoto dakika tano ni nyingi mtoto anapata haja kubwa lkn yana maumivu

Shukraan sana kumbe una matumizi sana huu mti

Ubarikiwe
 
Ipo mingi sana maeneo ya Gairo Morogoro kama unaelekea Dodoma. Sijajua hili kwao ni zao la biashara au laa

Zamani kidogo kabla ya Uhuru,zao la nyonyo kwa maeneo ya Dodoma na kondoa lilikuwa zao la biashara. Baada ya azimio letu wanunuzi wakakimbia na biashara ikafa.
 
Huku bongo unaweza kuwa mrefu kama mhogo mpira/mihogo inayotumika kwa kisamvu
mkuu kule kagera hurefuka zaidi na kuwa miti mikubwa ambayo hutumika kuusapoti mgomba usiangushwe na ndizi kabla ya kukomaa. mikia haraka sana na kurefuka mbegu zake hiliwa na njiwa pili, pia watoto huzitumia kama rublicants kwenye baiskeli zao za miti.
 
Mono,Mnyonyo,Mbono au Mbarika. Mbegu na majani vina matumizi mengi sana. Mbegu pia hutoa mafuta yatumikayo kama diesel.
 
Back
Top Bottom