Human Nature

Human Nature

Asante, namshukuru Mungu alinivusha salama na ndio lilikua somo la kutowaamini watu hovyo.

Haikuishia hapo, niliishia kupoteza Hela zingine. Jumla kama milioni 40 zilikwendraaaa😂😂😂😡💔
Hela nyingi ilikuchukua muda gani ku heal?
Mie siwezi kuibiwa hicho kiasi maana sina 🤣🤣
 
Na bado hela ya kula ulikua nayo 🤣🤣
Mie nilivyotapeliwa nilibaki mtupu sikua hata na piiiii 🤣🤣
Nilibakiwa na chenji chenji ila baadae ikabidi nianze kudai madeni kwa hasira pia kumkopa dogo😂😂😡

Yaani nilizoea maisha mazuri lakini mwishoni nilianza kukaanga mahindi kikawa ndio chakula😔😔😔💔
 
Usisahau ku share aisieee
Ertugrul Bey anza kufatilia

Story ya huyu mfanyakazi wangu tumwite John.

John tulikutana shambani alikuja kupruni miti baada ya kazi nikamlipa ila akaniomba kazi nyingine, bhasi nikampa kuchonga barabara ya kutenganisha miti.

John ni muongeaji sana ila hajasoma, alinivutia sana maana anajua vitu vingi lakini anaongea sana😂😂. Binafsi sipendi watu waongeaji sana kilichonivutia kwa John ni anaongea vitu ninavitamani kuvifanyia kazi shambani.

Bhasi baada ya kuishi na John ikabidi nimvute karibu zaidi na nikatokea kumuamini tuu, Inshort jamaa ni muaminifu sana tena zaidi ya sana. Maana katika kipindi hicho niliondoka kwenda Dar nikamuachia machine mpya, Chainsaw, Solar, simu na mazaga mengine ila niliporudi nilimkuta na vitu vyote. Bhasi ikabidi ndio awe msaidizi wangu wa karibu😊😊😊.

Jamaa namkubali coz alifikia kipindi akawa ananijali kuliko ninavyojijali mimi. Kule shambani Kuna Chui lakini anaishi bondeni karibu na mto ila Kuna siku alipandisha mpaka tunapoishi tukamuona, inshort Mimi niliendelea na maisha yangu ya kawaida lakini John alikua anaamka usiku anawasha moto, Mimi hata sielewi chochote😔😔💔. Kuna muda naenda kuchota maji pekeeangu John akijua inakua ni shida lazima atanikumbusha usiende pekeako chui anaweza kukuvamia huko, inshort Mimi nilikua sijali.

Baada ya dogo kutoroka na hela, Ikabidi nifunge kambi niwalipe mafundi madeni yao pia nikaenda kufunga kambi nyingine. Tukaondoka na John mpaka Songea kumsaka dogo.

Tulifika mpaka nyumbani kwake kutokana na story alizokua ananipa dogo. Tukavamia saa8 usiku kumbe dogo alishakimbia kabakia mke wake.

Mke wake anavitoto viwili vidogo tuu, huruma ikaniingia nikamwambia mke wake anipe ushirikiano ili nimpate mume wake La! sivyo atalea watoto pekeeake.

Sikuwa na muelekeo ikabidi niuze msitu uliobakia angalau niongeze fedha cash, nikauza milioni 8 benki nilikua na milion5 nikaziunganisha tukaenda kwa akina John kufanya biashara ya vigogo.

Siku nimefika kwa akina John nikazidiwa ikabidi niingie maabara kupima, Wakanikuta na vidonda vya tumbo na Typhoid. Ikabidi Mimi nilale town John atangulie kwao.

Nilianza kazi ya vigogo kwa siku nilikua naingiza 80k mpaka 130k. Lakini afya haikua poa yaani nilikua kama gari la mkaa siku Moja shambani, wiki moja gereji😂😂😂.

John akagombana na mke wake, nikabaki kufanya kazi pekee angu. Kupitia kufanya kazi alone nikapoteza milioni 6.5. Nilinunua msitu wakati nasubiri kwenda kukata vigogo nikazidiwa ikabidi nilazwe, wakati nipo hospital wahuni wakakata msitu wote vigogo siku nimerudi nakuta shamba jeupeeeee😳🥴😂💔😡😔🫵🫵🫵. Nikarudi town nikachukua gesti tuu kulala maana niliishiwa nguvu zote. Usiku wake nilidondoka na kuzimia kama mzigo.

Napata taarifa za dogo aliyechukua Hela za mbao, Nikadandia gari mpaka dar. Nikamshika dogo kanenepa na kitambi kimeota.

Dogo Hana Hela amemaliza zote kwa kunywa pombe na kuhonga mademu, amebakia na bodaboda, nikauza ile boda laki8 nikampiga search alibakia na laki Moja nikaichukua nikapanda gari kurudi mkoa. Yaani safari ya dar sikuingia hata geto kwangu nikarudi mkoa, hiki ndicho kilinisaidia hata mawazo mabaya yakaniondoka.

Niliporudi mkoa nikamsimulia John, dogo nilimshika lakini hakua na Hela. Akaanza kunilaumu kwanini hukuniambia twende wote, maneno yakawa mengi sana mpaka Mimi mwenyewe nikajikuta najutia ila nikamwambia ningemuua tuu yule dogo.

KISA CHA JOHN

John anamiliki shamba la parachichi kama ekari mbili na nusu, ugomvi wake na mke wake ni kuhusu Hela, pia Mimi na John hatukuachana kwa kauli nzuri maana ilifikia kipindi nikashindwa kufanya marejesho, afya ikadorola zaidi ikabidi nifanye maamuzi magumu ya kuacha kufanya shughuli yoyote.

Nikatangaza kuiuza Chainsaw, lakini John akaomba nimuuzie nikamwambia kwakuwa wewe ni jamaa angu bhasi nipe laki8 tuu. Tukakubaliana anipe laki3 kwanza afu nyingine baada ya wiki, kumbe hata hiyo laki4 Hana. Mimi nipo town naset nipango mingine John akawa hapokei simu zangu na hela hajaniwekea. Thamani ya chainsaw ni milioni 1.9 ikiwa mpya kwa jinsi nilivyoitumia ilifaa niiuze 1
Mil1.3

Nikamfuata John mpaka kwao nikaongea na wazazi wake, wakamdhamini nikaondoka pia bila Hela, kile kitendo kiliniudhi ila nikasamehe. Baada ya wiki nikawekewa fedha yangu namimi nikasitisha mawasiliano na John.

Baada ya parachichi za John kukomaa wahuni wakaanza kumtembelea shambani kwake. Wakaiba sana parachichi zake.

John akaamua kulinda parachichi zake, Kila siku usiku alikua analala shambani.

Siku Moja usiku akawaona wezi wake😂😂. Aaah! Ni ndugu zake kabisa Yaani wanatumia jina moja la ukoo. Wezi walikua wawili John yupo pekeeake.

Akapiga hesabu akaona jamaa wapo na mapanga ikabidi atoroke arudi nyuma kidogo, akapiga simu nyumbani kwao wakaja wadogo zake wawili. Wakawapigia ambushi wezi katika kukimbia mmoja akakimbilia njia ambayo John yupo. John akamkata mwizi na nyengo mguuni.

Mwizi kakamatwa akaomba msamaha John huruma na hasira vikachangamana, kwa maelezo yake anasema yeye hakuendelea kumpiga lakini aliwaambia wadogo zake kwamba wamvunje mwizi miguu, mwizi katika kupigwa mdogo ake John akampiga mwizi na rungu kichwani💔💔😡😔.

Mwizi kadondoka chini, damu zinatoka puani, mdomoni na masikioni. John akaingia ujasiri akampigia simu mwenyekiti na babaake kijana, mpaka wanafika na pikipiki kijana ni ameanza kupoa Yaani haeleweki ni anakoroma kama ng'ombe inataka kufa.

John akatoroka saa hiyo hiyo, anasema alikua anakimbia huku anajiongelesha mwenyewe, maneno anayoyakumbuka ni YESU nisaidie na unisamehe.

Baada ya mwezi mmoja yule mwizi alipata nafuu na ndipo John alirudi nyumbani kwao.

Sahivi Bado nipo na John tunapiga kazi, ila nikimwambia tufanye maamuzi magumu juu ya mtu yeye ndio anakua wa kwanza kunikataza😂😂😂.

John siku hizi anasali wakati wa kula, anakimbia nyimbo za dini pia. Kitu ambacho sijawahi kumuona John akifanya hapo kabla.
 
Mkuu hiki kidonda hakijapona vizuri 😂😂😂

Huyo dogo nilimsaka nikamkamatia Gomzi, amejaa mashavu na kitambi kimemtoka. Anachomiliki ni bodaboda tuu😡😡😡💔

Kama sio Mungu ningekuwa segerea pale, maana nilitamani kumuua na ndicho nilikipanga akilini mwangu.

Katika milion 28.6 niliambulia milion 1.32 niliamua kusamehe tuu na kuanza upya.
Ilikuwaje hii bingwa?
 
Story ya huyu mfanyakazi wangu tumwite John.

John tulikutana shambani alikuja kupruni miti baada ya kazi nikamlipa ila akaniomba kazi nyingine, bhasi nikampa kuchonga barabara ya kutenganisha miti.

John ni muongeaji sana ila hajasoma, alinivutia sana maana anajua vitu vingi lakini anaongea sana😂😂. Binafsi sipendi watu waongeaji sana kilichonivutia kwa John ni anaongea vitu ninavitamani kuvifanyia kazi shambani.

Bhasi baada ya kuishi na John ikabidi nimvute karibu zaidi na nikatokea kumuamini tuu, Inshort jamaa ni muaminifu sana tena zaidi ya sana. Maana katika kipindi hicho niliondoka kwenda Dar nikamuachia machine mpya, Chainsaw, Solar, simu na mazaga mengine ila niliporudi nilimkuta na vitu vyote. Bhasi ikabidi ndio awe msaidizi wangu wa karibu😊😊😊.

Jamaa namkubali coz alifikia kipindi akawa ananijali kuliko ninavyojijali mimi. Kule shambani Kuna Chui lakini anaishi bondeni karibu na mto ila Kuna siku alipandisha mpaka tunapoishi tukamuona, inshort Mimi niliendelea na maisha yangu ya kawaida lakini John alikua anaamka usiku anawasha moto, Mimi hata sielewi chochote😔😔💔. Kuna muda naenda kuchota maji pekeeangu John akijua inakua ni shida lazima atanikumbusha usiende pekeako chui anaweza kukuvamia huko, inshort Mimi nilikua sijali.

Baada ya dogo kutoroka na hela, Ikabidi nifunge kambi niwalipe mafundi madeni yao pia nikaenda kufunga kambi nyingine. Tukaondoka na John mpaka Songea kumsaka dogo.

Tulifika mpaka nyumbani kwake kutokana na story alizokua ananipa dogo. Tukavamia saa8 usiku kumbe dogo alishakimbia kabakia mke wake.

Mke wake anavitoto viwili vidogo tuu, huruma ikaniingia nikamwambia mke wake anipe ushirikiano ili nimpate mume wake La! sivyo atalea watoto pekeeake.

Sikuwa na muelekeo ikabidi niuze msitu uliobakia angalau niongeze fedha cash, nikauza milioni 8 benki nilikua na milion5 nikaziunganisha tukaenda kwa akina John kufanya biashara ya vigogo.

Siku nimefika kwa akina John nikazidiwa ikabidi niingie maabara kupima, Wakanikuta na vidonda vya tumbo na Typhoid. Ikabidi Mimi nilale town John atangulie kwao.

Nilianza kazi ya vigogo kwa siku nilikua naingiza 80k mpaka 130k. Lakini afya haikua poa yaani nilikua kama gari la mkaa siku Moja shambani, wiki moja gereji😂😂😂.

John akagombana na mke wake, nikabaki kufanya kazi pekee angu. Kupitia kufanya kazi alone nikapoteza milioni 6.5. Nilinunua msitu wakati nasubiri kwenda kukata vigogo nikazidiwa ikabidi nilazwe, wakati nipo hospital wahuni wakakata msitu wote vigogo siku nimerudi nakuta shamba jeupeeeee😳🥴😂💔😡😔🫵🫵🫵. Nikarudi town nikachukua gesti tuu kulala maana niliishiwa nguvu zote. Usiku wake nilidondoka na kuzimia kama mzigo.

Napata taarifa za dogo aliyechukua Hela za mbao, Nikadandia gari mpaka dar. Nikamshika dogo kanenepa na kitambi kimeota.

Dogo Hana Hela amemaliza zote kwa kunywa pombe na kuhonga mademu, amebakia na bodaboda, nikauza ile boda laki8 nikampiga search alibakia na laki Moja nikaichukua nikapanda gari kurudi mkoa. Yaani safari ya dar sikuingia hata geto kwangu nikarudi mkoa, hiki ndicho kilinisaidia hata mawazo mabaya yakaniondoka.

Niliporudi mkoa nikamsimulia John, dogo nilimshika lakini hakua na Hela. Akaanza kunilaumu kwanini hukuniambia twende wote, maneno yakawa mengi sana mpaka Mimi mwenyewe nikajikuta najutia ila nikamwambia ningemuua tuu yule dogo.
Alooooo nimesoma nimebaki shocked yaan wewe na mwizi wako uso kwa uso na ukaamua kusamehe hongera sana asieee pesa ilikua ndefu

Usipotumia busara unaweza kumuumiza mtu

Lakini bora ya hivyo
Japo ungeweza hata kumfunga
 
Ninakaudhaifu Fulani hivi Lakini ndio nguvu yangu pia.

Mimi ni mzito kufanya maamuzi ila nikishaamua Huwa sirudi nyuma.

Huyo dogo mama yake anapresha alafu alifanya hivyo baada ya kaka yake kuuza miti Yao ya familia na hakupewa mgao wowote. Hivyo alifanya hivyo ili kwamba ndugu zake ndio walipe hizo fedha. PUMBAVU kabisa
 
Nilikaa miezi mitatu siongei na mtu, sifanyi kazi, nakula na kulala tuu😂😂😂💔
Matapeli ni watu ambao nadhani huwa wamekata tamaa na huwa hawajali kabisa.

Kuna jamaa yangu wa karibu sana nilimpa hela baada ya kumuuliza una connection ile ofisi? Kuna Mwarabu anataka kupata documents fulani kwa ajili ya mwanae , akakubali ndio nina jamaa zangu wawili, Mimi nikampigia yule Mpambe wa Mwarabu inawezekana kupata hizo documents

Nikapewa ile hela na kama 100k ya soda 😂, jamaa akaniambia baada ya siku 10 yaani wiki mbili, basi mimi sikufuatilia tena Nikaendelea na mambo yangu nikisubiri hizi wiki mbili anipe hizo documents, kumbe jamaa alikimbia na mji kabisa kaenda kijijini kulima vitunguu kwa hela ya dhuruma.

Ilipofika muda wa wiki mbili nikampigia akawa anaanza kunizingua tu, ndio nikapata taarifa yupo kijijini huko ameanza kilimo. Aisee nilipitia kipindi kigumu hasira, hisia mchanganyiko na nikawa nalaumu jamaa kaharibu moja ya connection nzuri kabisa ilikuwa inapatikana kutoka kwa Mwarabu.

Nikaanza kutukanwa na Mwarabu kila aina ya tusi na muda wote wa wiki mbili alikuwa Hotel anasubiri documents, kumbe jamaa katapeli hela, ikabidi nianze kupambana mwenyewe kwa gharama na muda wangu mwingi, yaani within 5 days nikapata kila kitu. Nikampelekea Mwarabu documents zake akanipa na hela kidogo ya kuhangaika ila nikamwambia matusi uliyonitukana hayajafutika. Nilikueleza ukweli tumetapeliwa. Akaomba majina ya yule aliyetapeli ile hela.

Baada ya kukamilisha ule mchakato wa documents nikamwambia jamaa kwa njia ya whatsapp kistaarabu tu, Asante kwa ulichokifanya , khaaa 😅😅😅 Jamaa akaanza kunitukana tena na mbaya zaidi akampigia Mpambe wa Mwarabu ananisagia eti Dogo nilikuwa namuokoa tu lakini hela Mimi hakunipa.

Haya maneno ya huyu jamaa bado yananiuma aisee na yeye yupo kijijini huko nasikia kala shoti kwenye kilimo.

Lakini utapeli unauma sana kama niliofanyiwa bora kibaka akupore tu sio utapeli kama huu
 
Back
Top Bottom