ZirlovimovicZirkov
JF-Expert Member
- Sep 3, 2025
- 260
- 450
Uko sahihi mkuu, hakuna kitu kinauma kama kufanya jambo kwa dhamira nzuri alafu Kuna mtu anakuharibia.Matapeli ni watu ambao nadhani huwa wamekata tamaa na huwa hawajali kabisa.
Kuna jamaa yangu wa karibu sana nilimpa hela baada ya kumuuliza una connection ile ofisi? Kuna Mwarabu anataka kupata documents fulani kwa ajili ya mwanae , akakubali ndio nina jamaa zangu wawili, Mimi nikampigia yule Mpambe wa Mwarabu inawezekana kupata hizo documents
Nikapewa ile hela na kama 100k ya soda 😂, jamaa akaniambia baada ya siku 10 yaani wiki mbili, basi mimi sikufuatilia tena Nikaendelea na mambo yangu nikisubiri hizi wiki mbili anipe hizo documents, kumbe jamaa alikimbia na mji kabisa kaenda kijijini kulima vitunguu kwa hela ya dhuruma.
Ilipofika muda wa wiki mbili nikampigia akawa anaanza kunizingua tu, ndio nikapata taarifa yupo kijijini huko ameanza kilimo. Aisee nilipitia kipindi kigumu hasira, hisia mchanganyiko na nikawa nalaumu jamaa kaharibu moja ya connection nzuri kabisa ilikuwa inapatikana kutoka kwa Mwarabu.
Nikaanza kutukanwa na Mwarabu kila aina ya tusi na muda wote wa wiki mbili alikuwa Hotel anasubiri documents, kumbe jamaa katapeli hela, ikabidi nianze kupambana mwenyewe kwa gharama na muda wangu mwingi, yaani within 5 days nikapata kila kitu. Nikampelekea Mwarabu documents zake akanipa na hela kidogo ya kuhangaika ila nikamwambia matusi uliyonitukana hayajafutika. Nilikueleza ukweli tumetapeliwa. Akaomba majina ya yule aliyetapeli ile hela.
Baada ya kukamilisha ule mchakato wa documents nikamwambia jamaa kwa njia ya whatsapp kistaarabu tu, Asante kwa ulichokifanya , khaaa 😅😅😅 Jamaa akaanza kunitukana tena na mbaya zaidi akampigia Mpambe wa Mwarabu ananisagia eti Dogo nilikuwa namuokoa tu lakini hela Mimi hakunipa.
Haya maneno ya huyu jamaa bado yananiuma aisee na yeye yupo kijijini huko nasikia kala shoti kwenye kilimo.
Lakini utapeli unauma sana kama niliofanyiwa bora kibaka akupore tu sio utapeli kama huu
Mimi sijasema yote mkuu, dogo aliharibu mahusiano yangu na wazazi, kaka na madogo, Yaani Mimi nikaonekana tapeli.
Changanyia nilikua na mkopo na mshua ndio alinidhamini ikabidi nizime simu tuu, deni likaja kuwa la familia nzima😂😂😂.
Kuna muda Mungu tuu ndiye anaetupa nguvu ya kusonga mbele.
Mimi nilisema huyo dogo asijekufa bali maumivu niliyopitia mimi na ndugu zake waje kupitia.