Huenda ukastaajabu. Lakini huu ulikuwa upande wa pili wa maisha yangu ndani ya JamiiForums

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Habari za wakati huu wakuu,

Ni nusu mwaka sasa tokea kuwa "The Storyteller" aliyestahili tuzo humu jukwaani. Ni muda mrefu sana umepita tokea pale nilipoifahamu na kujiunga na jumuiya, japokuwa mlio wengi mtachungulia kwa profile ili kuona lile neno "joined Nov 2022", JF nimeifahamu kwa zaidi ya miaka kadhaa iliyopita

Mbali na ID ya Melki the Storyteller ,pia nina ID mama ambayo sitoiweka wazi kwa miaka hii, japokuwa ni ID kubwa na pendwa ambayo inatema madini yenye mantiki na yenye kukubalika. Katika ID hiyo nimeishi maisha yasiyo halisi kwa 100% na hakuna mtu anaweza / ataweza shitukia. Niwashukuru kwa kuniheshimisha kupitia hiyo ID

Je, The Storyteller wetu ana IDs nyingine za ziada mbali na hizo mbili tajwa hapo juu?

Jibu ni HAPANA. Lakini kwa kipindi cha nyuma nimewahi kuwa nazo kadhaa. Ndani ya JamiiForums nimeishi maisha ya uzee, ujana, usomi, ushamba, utoto, michezo, uganga, siasa n.k

Sometimes niliunda uzi na kuanza kuchangia mwenyewe huku nikibishana na kujitukana kwa ID hii na kusuluhisha kwa ID nyingine, lengo ni kusogeza uzi na kuufanya uzi kupamba moto

Niwaombe mniwie radhi kwa utoto nilioufanya kipindi cha nyuma, lakini sina budi kuuweka wazi siku ya leo

a) izo biz Hii ilikuwa ID yangu pendwa niliyoikubali kupita maelezo. Sikuwahi pitwa na tukio nisilielezee ndani ya ID hii. Nilifanikiwa kuunda nyuzi nyingi sana zenye mantiki na zisizo na mantiki ndani ya ID hii. Nikiachana na ID hii baada ya kuona wanachama wameanza kuignore post zangu na kudhani huenda zikawa ni chai, kitu ambacho sio kweli
Screenshot_20230511-221745.png

ID za karan lutha na wamatukio zilishika hatamu baada ya ID ya izo biz kususwa. Karan Lutha alitumika kuleta visa "serious" na hoja za msingi ambazo zilihitaji utatuzi makinifu ambazo kama zingewekwa kwenye ID ya izo biz zingekuwa ignored
Screenshot_20230511-222023.png

ID ya Wamatukio ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya Jokes na mikasa ya kuchekesha. Nahisi ni ID iliyokuwa pendwa kulinganishwa na izo biz ama karan lutha
Screenshot_20230511-221605.png

Tukiachilia mbali na IDs tajwa hapo juu, ID ya roselyn2 ilikuwa ni ID yangu pia. Hii niliitumia kwa ajili ya attention pamoja na changamsha kijiwe, japo kuna watu wachache walishtukia pasi na uhakika
Screenshot_20230511-222320.png

Baada ya kukomaa kifikra na kiakili, niliamua kuzichinjilia mbali ID hizi kwa namna ambayo ninaifahamu mimi i.e kwa IT ndogo niliyonayo kumkichwa

Nimeona ni vyema kuja kutubia makosa yangu hapa na kwa wakati huu. Kwa wale wote ambao niliwakwaza kupitia ID zangu, naombeni tusameheane na tuendeleze jukumu la kulijenga taifa

Narudi kwa ushuhuda zaidi...
 
Ndio maana kumekuwa na wingi wa nyuzi za ajabu na comment za ajabu hapa Jf kumbe sababu ni kama hizi!
Mtu mmoja ana I'd zaidi ya nne, je wakiwa kumi wa namna hiyo unadhani jf ya sasa hivi ingeepukika?
Sio nne tu mkuu, ni zaidi ya hizo (zinakuja). Pia sio mimi tu, ni watu zaidi ya mia humu ndani. Kuna kipindi niliweka wazi ID pacha humu JamiiForums, ila wacha tu tusifukue makaburi

Inasikitisha sana mkuu
 
japokuwa mlio wengi mtachungulia kwa profile ili kuona lile neno "joined Nov 2022", JF nimeifahamu kwa zaidi ya miaka kadhaa iliyopita
🤣🤣🤣
Hii lazima ulichekiwa Sana

Sometimes niliunda uzi na kuanza kuchangia mwenyewe huku nikibishana na kujitukana kwa ID hii na kusuluhisha kwa ID nyingine, lengo ni kusogeza uzi na kuufanya uzi kupamba moto

Subiri waunge ID zako zote hizo kwenye hii umeandika.. itakuwa vizuri.. kama kukaa kimya haujaweza.

Kwa wengine na mie bahati mbaya hizo ID sijawahi kuzinoti kukumbuka.. Ila rose.. kwa mbali naikumbuka..

Tuliza kichwa mdau.. humu ukiweka hisia unalo.. jitahidi ujirekebishe uachane na hayo ukipata nafuu kabisaaa
 
Subiri waunge ID zako zote hizo kwenye hii umeandika.. itakuwa vizuri.. kama kukaa kimya haujaweza.

Kwa wengine na mie bahati mbaya hizo ID sijawahi kuzinoti kukumbuka.. Ila rose.. kwa mbali naikumbuka..

Tuliza kichwa mdau.. humu ukiweka hisia unalo.. jitahidi ujirekebishe uachane na hayo ukipata nafuu kabisaaa

Wacha wafanye watakachojisikia. Lakini wasifikie maamuzi ya kuunga ID ya yule mwanadada roselyn2 hapa
 
Back
Top Bottom