Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

Adriel Vin

Senior Member
Jun 25, 2020
148
748
Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baaba ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikua amefariki tayari

INAENDELEA

Kabla ya kuendelea naomba niweke vitu flani sawa: Hakuna mahali nimesema Baba hakua mtu mwema, au alikua mtu mbaya, nimeelezea kipande kirefu kuhusu mama sababu muda mwingi alikua na mimi kuliko mzee, Mzee pia alikua anasafiri kikazi na sisi tulikua tukifurahi maana mzee alikua mkali balaa….

Tuendelee sasa…

Usiku ule ulikua na majonzi na masikitiko makubwa, sikua mkubwa sana nakumbuka ndo nilikua form 1 ila yale machungu ya kumpoteza mama yalikua makubwa sana…Mimi, Kaka yangu na mdogo wangu kila mtu alikua na maumivu yake. Ntazungumzia yanayonihusu sana..

Asubuhi taratibu ziliendelea huku ndugu jamaa na marafiki wakiendelea kuja kutoa pole. Wanafunzi wenzetu pia walifika. Taratibu nyingine ziliendelea kama nmavyojua misiba ya kitanzania. Tulikua tunatakiwa kusafirisha siku inayofuata ambapo tuliaga mwanza pale na jioni kusafirisha kuelekea Bukoba kwa mazishi.

Ilikua mara yangu ya kwanza kutoka nje ya mkoa wa Mwanza, Tulipeleke mwili majira ya saa 10 pale custom watu wa kamda ya ziwa wanaelewa zaidi. Kipindi hiki usafiri mkuu ulikua ni meli.
Basi baada ya kupeleka mwili tulirudi kujiandaa na safari. Majira ya saa 1:30 jioni tulienda kupanda meli. Saa 3 kamili safari ilianza kwenda kumpumzisha mpemdwa mama.

Wakati huu sikua na maumivu ya msiba sana kutokana ma kampani za watu tulioenda nao lakini pia mambo ya safari, nilikua na ka ushamba ka safari so kitendo cha kupanda meli sijui nilikua naona niko kwenye nini vile.
Wakati safari inaendelea tulikua tunazunguka zunguka kwenye meli kwani tulipanda third class wote, kipindi hicho ilikua fresh tu hata third class watu walikua hawana habari.
Wazee na wengineo waliendelea kula beer mle kwenye meli kama hakuna kilichotokea.
Wakati tunaendelea kuzunguka huku na huku asee sijui tulitokea wapi ila sehemu wanayoweka majeneza yanayosafirishwa niliiona kwa mbali na niliweza kujua jeneza la marehemu mama ni lipi maana yalikua kama matatu hivi maana yake watu waliokua wanaenda msibani mle ndani ya meli walikua wengi.

Ilibidi nitoke kabisa eneo lile kwani lilinikumbusha machungu ambayo nimeshasahau, kitendo cha kuona jeneza lile hakikua kizuri kwangu.
Nilienda kulala na kaka yangu na dogo tuliungana na uncle

Saa 10 hivi asubuhi tulikua tumefika kemondo. Hapa baadhi ya watu huwa wanashuka then meli inaendelea na safari kwenda bukoba mjini.
Nilikua excited kufika bukoba na ilikua mara ya kwanza ila sasa ndo nimefika kisa msiba alafu mbaya zaidi ni msiba wa mama yangu.
Majira ya saa moja asubuhi tulifika bukoba mjini hapo tukaungana na ndugu zetu wengine tayari kuanza safari ya kwenda kumpumzisha mama huko kijijini kwetu.

Baba alikua close na sisi na hata ule ukali wake tuliusahau. Ndugu wengine waliungana na sisi hadi kijijini na taratibu nyingine ziliendelea.
Ilisomwa misa pale baadae taratibu za mila then mwili ukahifadhiwa ili kesho tumpuzishe mama katika nyumba yake ya milele.
Wakati yote yanaendelea nilikua najiuliza sana maisha yatakuaje, yani ntarudi home bila mama… lilikua swali ambalo halina majibu kwangu.

Kesho kila kitu kilikua kimekamilika na utaratibu wa kanisa ndo ulituongoza katika mazishi ya mama.
Baada ya kumaliza kuzika majira ya saa 11:30 jioni basi usiku wake tulikua na kikao cha familia na moja ya mambo yaliyotuhusu sisi watoto ni suala la shule.

Shangazi zetu pamoja na mzee na ndugu wengine walikubaliana tuhamishwe shule tukasomee Bukoba.
Kuna shule flani waliitaja jina nahifadhi na mimi na Kaka yangu kwakweli tulivyomaliza kikao tulikaa pembeni tukajazana ujinga kwamba hakuna mtu anakuja kusomea huku Bukoba “Yani tutoke mjini kuja kusoma kijijini” ilikua kauli ya bro. Upande wa dogo yeye alikua bado hajamaliza la saba so haikua issue kwake na alikua bado mdogo.

Moja ya matukio ya kushangaza ni taratibu za makabila mengi kukaa nje pale mlipozika angalau kwa siku 5…(sikua najua kwanini hadi lilipotokea tukio naomba nifafanue kidogo hapa)

Niliambiwa kijijini kuna wachawi wana tabia za kufukua maiti ya kuzila au kupeleka wanakojua. Sasa tukiwa tumemaliza mazishi usiku wake tulikua watu wengi sana nje pale pembeni ya kaburi huwa unawashwa moto ili kupunguza baridi then watu watakesha hapo wakinywa, kupiga story na mambo mengine lakini lengo kuu ni kilinda mwili uliofukiwa.
Nilikaa nje hadi saa saba na watu wengine baadae nilienda kulala maana mambo ya kukesha sikua nimezoea, pili mazingira ya kijijini sikua nimezoea bado.


Ikiwa ni siku ya 3 tangu tuzike asubuhi yake kuna maneno nilisikia watu wanaongea kuhusu kaburi kuonekana kama limetitia chini. Basi watu wakaunga story kuwa tayari wachawi walishatoa mwili ule.
Kwakweli nilijisikia vibaya sana na kukasirika sana kusikia vile, sikua naamini mambo ya uchawi kabisa ila kilichonipa moyo ni baada ya mzee mmoja kuchukua mti mrefu na kwenda kuchomeka moja kwa moja kwenye kaburi ( sikujua maana yake at first) ila baadae alituhakikishia mwili haujachukuliwa.
Nilihoji kwa uncle mmoja akasema alichoma pale katikati ya kaburi ili kusikia kama kuna kitu ndani. Anyway tuachane na hapa maana sijawahi kuamini hata siku moja hizo story.

Baada ya siku 4 kupita tulitakiwa kwenda kwa Babu (Mzaa mama, ni kijiji kingine)
Huko tulilala siku moja then tukarudi bukoba mjini tujiandae na safari.

Tulirejea Mwanza siku ya 6 na mimi na bro tulikaza kuhusu kusoma nje ya Mwanza haiwezekani.

Mdogo wetu alienda kukaa na sister mkubwa maana ni rafiki yake sana hadi leo hii, nilisema nna dada 2, So mmoja ndo dogo alienda kukaa na sisy then mimi, bro na mzee tukaendelea na maisha.

Wakati huo kaka angu alikua form 3 na mimi nilikua form 1. Baada ya kurudi mwanza ilibidi nirudi ile shule ya kata niliyochaguliwa kwani hakukua na mtu wa kulipa ada kule private coz tumekataa kusoma Bukoba. Kaka yangu yeye ilibidi amalize pale pale ….


ITAENDELEA….
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom