Kalamu Yangu, Rais Ali Hassan Mwinyi na Kitabu: "Mzee Rukhsa" Safari ya Maisha Yangu"

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
KALAMU YANGU, RAIS ALI HASSAN MWINYI NA KITABU: ''MZEE RUKHSA: SAFARI YA MAISHA YANGU''

Makala hii fupi niliandika May 2021 baada ya kutoka kitabu cha maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

''Leo nimeingia Maktaba nikawa naangalia makala ambazo nimeandika kuhusu mambo tofauti ya serikali wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Kilichonifanya nifanye hili ni kule kusoma sehemu za kitabu cha Mzee Mwinyi na katika kusoma huko kukanikumbusha baadhi ya matukio muhimu ambayo yalinisukuma kuandika makala wakati mwingine katika magazeti ya nje kama inavyoonekana katika picha - Africa Events na New African yote majarida yakichapwa London na wakati mwingine tukiandika katika magazeti yetu ya ndani.

Hapa nitacheka kidogo kwani ujana hakika una raha zake, wakati mwingine tukiandika kutoka ''msituni.''

Kwa hakika kipindi cha utawala wa Mwinyi hakupungukiwa na watu waliokuwa wanaona raha kumshambulia.

Ilisikitisha kuwa kulikuwa na magazeti yalimpa nafasi Reverend Mtikila kumshambulia Rais.

Kuna baadhi ya vijana wa wakati ule waliona wana wajibu na dhima kubwa ya kumtetea Rais pale ilipodhihiri kuwa hakuwa na mtetezi.

Nilikuwa mmojawapo wa vijana walioamua kumtetea Rais Mwinyi.

Namsoma Rais Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Historia ya Maisha Yangu,'' na natingisha kichwa kwa mengi ninayokutananayo.

Natingisha kichwa kwa kuwa baadhi ya matukio na mambo yaliyomo kitabuni mimi na wenzangu tuliyafahamu kwa undani na tuliyaandika kwa yale yaliyostahili kuandikwa na mengine tuliyanyamazia.

Ninapotembea katika Maktaba hakika inanikumbusha mengi na kuwaleta wenzangu wengi tuliokuwa pamoja baadhi wameshatangulia mbele ya haki.

Maktaba inanikumbusha watu muhimu sana wa nyakati zile kama Augustine Mrema Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Waziri Mkuu, Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro na Mchungaji Christopher Mtikila Muasisi na Kiongozi wa Full Salvation Church.

Hakika zile zilikuwa nyakati za aina yake.''

1709267579728.jpeg

1709267622236.jpeg

1709267650667.jpeg

1709267683330.jpeg
 
Um

Umefanana na Zembwela
 
Kama kawaida yao!

Wakishaandika kitabu ujue muda was kufa umekaribia!hawachukui muda!

Refer mkapa, Reginald mengi,n.k

Hata jk siku akizindua Cha kwake inabidi niende msoga nikamuone Kwa mara ya mwisho!WAKIZINDUA HAWAISHI TENA MUDA MREFU!

IPO siri nyuma ya hii kitu!!
 
Kama wafanyakazi wa serikali wakistaafu miaka mitano mingi sana. Wanstafu na magonjwa sijui.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom