Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,586
50,683
Habari ya wakati huu JF members, nina imani mnaendelea salama. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kushare japo kidogo hili swala ninalolipitia.

Mimi na familia yangu(baba, mama, kaka na wadogo zangu) hatukutoka kwenye familia ya yenye uwezo. Maisha tuliyokuwa tunayaishi tangu nikiwa mdogo binafsi nilikuwa siyapendi kabisa na niliapa mimi wala watoto wangu hatutakuja kuishi maisha maisha niliyoyaishi nikiwa mdogo na niliapa kuja kubadilisha historia ya wazazi wangu.

Kwa ufupi tu haikuwa kazi rahisi lakini Mungu ni mwema, nililoliomba kwa miaka mingi limefanikiwa kwa asilimia 92. Ndugu zetu kwa upande wa baba kwanzia baba wadogo, babu, mashangazi walikuwa hawatukubali wala kutuombea mema.

Walituhesabu sisi ni fungu la kukosa, maisha hayakuwa rahisi lakini Mungu mwingi wa rehema amenitumia mimi kubadilisha familia ili nizidi kuongeza Utukufu.

Nitaruka ruka kidogo ili kufikisha ujumbe maana ni ndefu sana, najua hii ni personal life lakini nimeamua kuileta huku sidhani Kama kuna ubaya.

Wazazi wangu walitengana kama miaka 20 na zaidi iliyopita kila mtu akaishi kivyake, hali ya utengano iliunyong’onyeza sana moyo wangu kuna wakati nilikuwa nikienda kumsalimia mama najikuta namkumbuka baba yangu (hapo sijui alipo), nikajiuliza ni kwanini ninaumia hivi juu ya utengano huu wa wazazi wangu, nikajisemea moyoni hapana mimi ndie ninaetakiwa kuirudisha hii familia pamoja tena.

Mungu alivyomwingi wa rehema akanibariki nikafanikiwa kujenga kijumba kidogo kwa ajili ya wazazi wangu (nikamrudisha kwanza baba nyumbani) baada ya baba kurudi vita vya ndugu vikaibuka nilikuwa na maswali mengi sana nikajisemea moyoni badala hawa ndugu wamshukuru Mungu ndugu yao amerudi nyumbani wao wanaanza kumpiga vita.

Maisha yakaendelea wakati Niko endelea kufanya utaratibu na kuzungumza na wazee ili kama kuna mila zifanyike başı mama yetu arudi nyumbani.

Wakati baba yuko nyumbani ugomvi ukawa ni mwingi sana na mashangazi, mara leo limetokea hili kesho lile nikasema ngoja nikate mzizi wa fitna maana ilikuwa inaonekana kama mama angerudi başi Vita ingekuwa kubwa ikabidi nizungushe ukuta kote kupunguza maneno.

Nikajisemea mpaka mtu aje kugonga geti kuanzisha ugomvi basi atakuwa amedhamiria kweli.

Baada ya kumalizana na ujenzi wa ukuta nikamrudisha mama nyumbani so kwa sasa wa naishi kwa upendo na Amani ingawa majaribu ya upande wa ndugu wa baba hayana budi kuja lakini Mungu anamuepusha nayo.

Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!

Moyo wangu unavuja damu, koşa langu liko wapi? Ninastahili maombi mabaya namna hii? Moyo wangu unamajeraha.

Nimeifupisha naomba kuiwasilisha.
 
Kwa Familia za Kiafrika ukiona hivyo tambua wewe Una nyota, Kata mnyororo wa Umaskini, Jiimarishe Kiroho, usikate tamaa pambana hapo hapo zidi kuwekeza. Epuka kuwajibu hao ndugu kaaa kimia kama huskii kama huoni. Pi uwe mwangalifu pindi unapokutana nao na ukiweza weka kauzibe ka kuwakarbia ingawa kutoa misaada pale inapobidi fanya.

Pole Mkuu wengi wamepitia tanuru hilo na wametoboa.
 
Habari ya wakati huu JF members, nina imani mnaendelea salama. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kushare japo kidogo hili swala ninalolipitia.

Mimi na familia yangu(baba, mama, kaka na wadogo zangu) hatukutoka kwenye familia ya yenye uwezo. Maisha tuliyokuwa tunayaishi tangu nikiwa mdogo binafsi nilikuwa siyapendi kabisa na niliapa mimi wala watoto wangu hatutakuja kuishi maisha maisha niliyoyaishi nikiwa mdogo na niliapa kuja kubadilisha historia ya wazazi wangu.

Kwa ufupi tu haikuwa kazi rahisi lakini Mungu ni mwema, nililoliomba kwa miaka mingi limefanikiwa kwa asilimia 92. Ndugu zetu kwa upande wa baba kwanzia baba wadogo, babu, mashangazi walikuwa hawatukubali wala kutuombea mema.

Walituhesabu sisi ni fungu la kukosa, maisha hayakuwa rahisi lakini Mungu mwingi wa rehema amenitumia mimi kubadilisha familia ili nizidi kuongeza Utukufu.

Nitaruka ruka kidogo ili kufikisha ujumbe maana ni ndefu sana, najua hii ni personal life lakini nimeamua kuileta huku sidhani Kama kuna ubaya.

Wazazi wangu walitengana kama miaka 20 na zaidi iliyopita kila mtu akaishi kivyake, hali ya utengano iliunyong’onyeza sana moyo wangu kuna wakati nilikuwa nikienda kumsalimia mama najikuta namkumbuka baba yangu (hapo sijui alipo), nikajiuliza ni kwanini ninaumia hivi juu ya utengano huu wa wazazi wangu, nikajisemea moyoni hapana mimi ndie ninaetakiwa kuirudisha hii familia pamoja tena.

Mungu alivyomwingi wa rehema akanibariki nikafanikiwa kujenga kijumba kidogo kwa ajili ya wazazi wangu (nikamrudisha kwanza baba nyumbani) baada ya baba kurudi vita vya ndugu vikaibuka nilikuwa na maswali mengi sana nikajisemea moyoni badala hawa ndugu wamshukuru Mungu ndugu yao amerudi nyumbani wao wanaanza kumpiga vita.

Maisha yakaendelea wakati Niko endelea kufanya utaratibu na kuzungumza na wazee ili kama kuna mila zifanyike başı mama yetu arudi nyumbani.

Wakati baba yuko nyumbani ugomvi ukawa ni mwingi sana na mashangazi, mara leo limetokea hili kesho lile nikasema ngoja nikate mzizi wa fitna maana ilikuwa inaonekana kama mama angerudi başi Vita ingekuwa kubwa ikabidi nizungushe ukuta kote kupunguza maneno.

Nikajisemea mpaka mtu aje kugonga geti kuanzisha ugomvi basi atakuwa amedhamiria kweli.

Baada ya kumalizana na ujenzi wa ukuta nikamrudisha mama nyumbani so kwa sasa wa naishi kwa upendo na Amani ingawa majaribu ya upande wa ndugu wa baba hayana budi kuja lakini Mungu anamuepusha nayo.

Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!

Moyo wangu unavuja damu, koşa langu liko wapi? Ninastahili maombi mabaya namna hii? Moyo wangu unamajeraha.

Nimeifupisha naomba kuiwasilisha.
USIWASIKILIZE

USIRUHUSU MTU YEYOTE AKUAMBIE 'SHANGHAZI YAKO ANAKUSEMA HIVI'

MARA OOH SIJUI NANI ANAKUSEMA HIVI

Hata mama yako asikuletee taarifa zozote kutoka kwa ndugu zako

Jiepushe Kuumizwa bila sababu
 
Na koo zetu nyingi za kimasikini zikiona kuna mtu anajichomoza kwenye ukoo kidogo anapata zinapigana kumsusha wew ao shangazi zako sjui Baba mdogo ao sio watu kabisa usipo kua makini wanakupukuta wew na huyo Bi mkubwa wako Na ivyo ni Mwanamke watakuonea Sana inabidi usimame ngangari kweli kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom