Hongera sana Rais Samia kwa kuwainua kiuchumi wakulima, umeliinua taifa kwa kuwainua wakulima

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu watanzania,

Asilimia kubwa ya watanzania Ni wakulima waliojiajiri katika kilimo, wanao tegemea kilimo kuendesha maisha yao, wanaojenga na kununua sare za shule kwa sababu ya kilimo, wanao fungua miradi kwa sababu ya kilimo, wanao nunua magari kwa sababu ya kilimo, wanaojenga nyumba Bora na za kisasa kwa sababu ya kilimo.

Hivyo Basi ukikiinua kilimo maana yake umewainua mamilioni ya watanzania kiuchumi, umeliinua Taifa kiuchumi, umeinua Secta ya viwanda, biashara, umekuza na kuongeza ajira kwa vijana na akina mama.

Ukikiinua kilimo maana yake umepunguza umaskini na ufukara Tanzania,maana yake umepunguza umaskini wa Kaya moja moja na jamii kwa ujumla, maana yake umeongeza Tabasamu na furaha katika mioyo ya watanzania walio wengi, maana yake umeboresha Afya ya mwili na akili ya watanzania walio wengi.

Lakini ukikidharau na kukiipuuza kilimo maana yake umewadharau na kuwapuuza mamilioni ya watanzania, ukikinyima bajeti na kipaombele kilimo maana yake umewanyima bajeti watanzania na kuwaathiri kiuchumi.

Kwa kulitambua Hilo Rais Samia na serikali Yake ameamua kuwafuta machozi wakulima,ameamua kuacha Alama katika mioyo ya wakulima, ameamua kujiwekea Rekodi yake ya kuwainua Wakulima kiuchumi na kupunguza umaskini wa Kaya, kwa kuongeza bajeti kutoka billioni Mia mbili na point Hadi billioni Mia Tisa na point.

Pamoja na kutoa billion Mia moja hamsini Kama Ruzuku kwenye mbolea, Hali iliyoleta mapinduzi ya kilimo, lakini pia Rais Samia na serikali Yake ameamua mkulima ajiuzie mazao yake mahali palipo na Bei nzuri bila vikwazo.

Rais Samia Hataki Hataki kumuonea mkulima juu ya jasho lake, Hataki mkulima abaki mbavu tupu kwa kukonda huku wanaonenepa kwa jasho la mkulima wakiwa kwenye viyoyozi, Hataki mkulima awe Kama mtumwa ndani ya nchi yake, Hataki mkulima ndio awe wakuingia hasara kila mwaka,Hataki mkulima awe wa kupangiwa Bei na mahali pa kuuza kila mwaka.

Sasa wakulima Ni vicheko na furaha, Ni Tabasamu na shangwe juu ya Rais wao kipenzi mama Samia kwa namna anavyowalinda na kuwapigania juu ya ustawi wao, Sasa wakulima wanajenga nyumba Bora na za kisasa.

Wananunua magari, wanafungua miradi ya kuwapatia kipato Cha kila Siku, wanaongeza mashamba na wanatumia mbolea kupandia na kukuzia, Sasa wakulima wanapendeza hata watembeapo njiani, Afya zao Ni nzuri,sura zao Ni za furaha kwa kuwa Wana matumaini ya kuinuka kiuchumi na kufaidika na jasho lao.

Sasa wale wanyonyaji wa miaka yote, wasiojuwa ugumu wa jembe, wasiojuwa hata Bei ya mbolea, wasiojuwa hata jembe linashikwaje mpini, wasio wahi kukanyaga shambani, wasio wahi hata kumiliki au kukodi shamba wanapiga kelele, wanalia Lia huku wakiwa wamejibanza mijini, wanasema sembe Bei juu, Mchele Bei juu na hata maharage Bei juu.

Ukiwauliza mlitaka mnunue kwa shilingi ngapi? Hawana majibu,ukiwauliza mnajuwa Bei ya mbolea msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi ngapi? Hawana majibu, ukiwauliza Kama wamewahi kulima au kwenda shambani wanasema hawajawahi kulima Wala kwenda mashambani.

Sasa Napenda niwaambie kuwa kilimo ni kigumu, Ni Vita ya kimwili,Inahitaji uvumilivu, Subira na ujasiri, ujasiri wa kufukia mtaji wako wooote ardhini ili uje uvune baadaye, ujasiri na uvumilivu wa kuamka alfajiri na kushinda kutwa nzima shambani bila kuweka chochote kile mdomoni kwenda Tumboni, siyo Rahisi Wala mzaha, haihitaji maneno maneno ukiwa umeshika jembe maana utajikuta unachoka huku ukiwa hujafanya kazi.

Chini ya Rais wetu mpendwa mama Samia Tunasema kilimo Ni biashara, hakuna anayetaka biashara ya hasara, hakuna anayetaka biashara ya kumletea madeni kila Siku, hakuna anayetaka kuumia na kulia kwa hasara kila siku.

Hakuna anayetaka kupoteza na kufirisika kimtaji kila siku, hivyo kila mwenye ardhi Arudi akalime apate chakula na ziada ya kuuza, kila mmoja akatafute shamba alime, ondokeni na pungueni mijini mkalime vijijini kwenu halafu mtarejea baada ya kulima.

Au tumeni pesa kwetu tuwalimie na kuwapandia na tutawasaidia kuwavunia na kusafirisha mpaka mliko maana sisi Ni waaminifu, kila Kona ya nchi yetu ardhi Ni yenye rutuba, hivyo acheni maneno Njooni mlime na nyie.

Wakulima wapo bega kwa bega na Rais wao na wanaona Ni mkombozi aliyekuja kuwakomboa na kuwatua mizigo ya umaskini, ufukara, kuonewa na kunyonywa ambako walikuwa wakitendewa miaka yote, wakulima walichoka kuonewa, walilia lakini machozi Yao yakawa Kama ya samaki ziwani.

Sasa wamempata Rais wao anaye wajali na ambaye amekuja kuwafuta machozi na kuwatia moyo, wanaendelea kumshukuru Samia wao kwa upendo mkubwa alio uonyesha kwao wakulima ambao Ni wengi kuliko kundi lolote lile hapa Tanzania, Kama unataka Vita na ugomvi na wakulima Njooni majukwaani muwaambie wakulima juu ya kufunga mipaka muone namna mtakavyo zomewa na kuondoka kwa aibu kubwa.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Angejua tulivyomchoka na vi tried vyake sifia sifia hata paspositahili?? Angekuwa kaacha kitambo
Kama unaona Mimi nasifia Sana Basi na wewe kosoa kwa hoja zenye ushahidi unapoona Pana mapungufu ili ujibiwe kwa hoja
 
Nendeni mkasema jukwaani mbele ya wakulima kuwa mipaka ifungwe ili muone kitakachotokea,maana nyie chadema akili zenu mnaZijuwa wenyewe
Hili la kutaka mipaka ifungwe ni la mtu na mtu wala siyo la chadema.

Kuna watu wansdanga, wanabet, ni machawa, wanacheza pool kuntwanzima, n.k halafu wanataka wenzao walioamua kwenda shamba kuisaka mali waingie hasara kwa mipaka kufungwa. Ili wao wanunue chakula kwa bei nafuu.

Never again. Rais Samia shikilia hapo hapo.
 
Hili la kutaka mipaka ifungwe ni la mtu na mtu wala siyo la chadema.

Kuna watu wansdanga, wanabet, ni machawa, wanacheza pool kuntwanzima, n.k halafu wanataka wenzao walioamua kwenda shamba kuisaka mali waingie hasara kwa mipaka kufungwa. Ili wao wanunue chakula kwa bei nafuu.

Never again. Rais Samia shikilia hapo hapo.
Hakika Rais Samia amewafuta machozi wakulima na kuamsha matumaini ya wakulima kuinuka kiuchumi
 
Hakika Rais Samia amewafuta machozi wakulima na kuamsha matumaini ya wakulima kuinuka kiuchumi
Mwenye hili sisi wakulima bila kujali vyama vyetu tunasema asilegeze kamba.

Ingawa mwaka huu mbolea imechelewa kuwafikia wakulima.
Sababu tunaelezwa kwamba kampuni iliyopewa tenda ya kuagiza na kusambaza mbolea ilikuwa haina uwezo na uzoefu wa kufanya kazi hiyo.

Ikabidi utaratibu wa kuipoka na kuirudisha kazi hiyo kwa kampuni ya zamani ufanyike.
 
Back
Top Bottom