Video: Rais Samia Kuifutia Tanzania & Afrika Aibu ya Njaa.Anatekeleza Maono Ya Baba wa Taifa ya Kilimo Kwa Vitendo.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,046
49,730
Toka baada ya uhuru wa Tanganyika na baadae Tanzania na Afrika imekuwa zinapata aibu kutokana na Njaa.

Njaa inadhalilisha utu wa mtu na kushusha heshima ya mtu na Taifa.Tanzania na Afrika zimekuwa kwenye aibu hiyo Kwa takribani miaka 60 Baada ya uhuru licha ya Waasisi Wetu kuwa na dhamira njema ambazo hazikuzaa matunda kutokana na sababu kadha wa kadha.

Kwa kuwa Tanzania ni Nchi yenye baraka,Mungu hajawahi acha kuikirimia viongozi makini.Mwl.Nyerere Baba wa Taifa aliasisi Maono ya kuleta mapinduzi kwenye Kilimo Kwa kuanzia kuhamasisha Kilimo kwa Kauli na matendo.

Lakini baada ya Mwl.kuachia madaraka Kilimo na wakulima walitelekezwa na tawala zilizofuatia na kufanya maelfu ya watu kuendelea kuogelea kwenye umaskini.Kilimo kiliporomoka licha ya kupambwa na Kauli tamu tamu kutoka Kwa Wanasiasa matapeli waliohitaji kura za wakulima na baada ya kupata waliwatelekeza.Kauli kama
Kilimo ni Uti wa mgongo wa Taifa,Kilimo Cha Kufa na Kupona, Kilimo kwanza na Wanyonge zilipamba majukwaa ila site waliko wakulima hakuna kitu.
Mungu amesikia Sauti ya Wakulima na kumleta Rais Samia ambae bila kujali Kauli mbinu ameamua kutekeleza Kwa matendo Maono ya Baba wa Taifa na kuweka utashi mkubwa kwenye Kilimo Kwa kutambua kwamba

-80% ya Ajira zinatoka kwenye Kilimo
-85% ya mali ghafi za viwanda zinatoka kwenye Kilimo
-66% ya Watanzania wanafanya Kilimo kama kazi Yao ya kwanza lakini njaa Bado imekuwa sehemu ya maisha.
Ni baada ya kuingia madarakani 2021 akiwa na timu Bora inayoongozwa na Waziri Bashe aliamua kubadili mtizamo wa Vijana na jamii Kwa ujumla Kupitia Ajenda 10/30 Kwa kuwaambia kwamba Ukulima ni Utajiri na akaweka utashi wa Kisiasa na kumwaga pesa Kupitia Bajeti ya Kilimo iliyovunja rekodi ya Bilioni 900 ambazo zimekuwa zikitumika kufanya mambo yafuatayo;
1.Alianzisha mara Moja utoaji wa ruzuku kwenye pembejeo za Kilimo kuanzia mbolea Hadi madawa.
2.Alianzisha program ya BBT Kwa Vijana.Inawapa Ardhi Bure ya Kilimo ambayo imefungwa mfumo wa Umwagiliaji na kupewa mikopo ya uendeshaji.
3.Amefufua Vituo vyote vya Utafiti wa Kilimo vilivyokufa Kwa kutopewa Bajeti na Vitendea kazi.
4.Ameajiri Maelfu ya Wataalamu wa Kilimo kuanzia Wahandisi Hadi Extension Officers na kuwapa vitendea kazi Ili wawasaidie wakulima.
5.Amejenga skimu Mpya za Umwagiliaji na amefufua skimu nyingi zilizokufa.Samia anataka kufikia 2030 Jumla ya hekta mil.8 ziwe chini ya Umwagiliaji kutoka hekta 700k za Sasa.
6.Amefufua mashamba yote ya Utafiti wa Mbegu.Lengo ni kuwa na utoshelevu wa mbegu na kuacha utegemezi wa Nje ya Nchi.
7.Amewatafutia wakulima masoko ya ndani na Nje ya Nchi ambapo Serikali hununua mazao na ziada huuza Nje ya Nchi.Mfani mwaka huu Serikali imenunua tank 500,000 za mazao,hii haijawahi tokea.Lengo la Serikali ni kununua na kuhifadhi mazao tani mil.3 ifikapo 2030.
8.Anaweka pesa kwenye sekta ya Barabara Vijijini zaidi ya mara 4 ya Bajeti ya awali Ili kufungua Uchumi wa Vijijini waliko Wakulima.
8.Anajenga mabwawa ya Maji Kila Wilaya Kwa Ajili ya Kilimo Cha Umwagiliaji Ili kuepukana na kutegemea mvua
9.Anajenga maghala ya kuhifadhi mazao Kwa Kushirikiana na sekta binafsi Ili kuokoa kupotea Kwa mazao baada ya kuvunwa(Post harvest losses).
10.Amekusudia kujenga visima 65,000 Kwa Ajili ya wakulima wadogo ambapo Kila mkulima aliyesajiliwa atachimbiwa kisika na kufunguwa mfumo wa Umwagiliaji wa kutosha ekari 3 Ili kuongeza Tija.
11.Amebadili sheria,kanuni,mifumo ya Kodi ikiwemo kushusha riba za banks Kwa wakulima Ili kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha wakulima Ili kushawishi uwekezaji zaidi kwenye Kilimo.Kwa Sasa Kilimo kinaongoza kuvutia uwekezaji na mikopo ya banks.

Mwisho hayo ni Baadhi tuu ya mambo ambayo Rais Samia anafanya kwenye sekta ya Kilimo Ili kufuta aibu ya Njaa Afrika na kuifanya Tanzania kuwa Benki ya Chakula Ya Dunia.
Sikiliza video hii hapa kupata mwanga zaidi wa nini kinafanyika Kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

View: https://youtu.be/cko82ib-Ndk?si=OcFlkOvdtOEP_27s

My Take
Samia ndio ataachia legacy itakayoishi bizazi na bizazi Tanzania.

View: https://youtu.be/TLtvXgyxZgI?si=tNASNVTgejjW3Cw7
 
Wakati wa kilimo kufa na kupona na kilimo kwanza wewe ulikuwa hujazaliwa! tatizo nyinyi mbogamboga mnadhan watanzania wa sasa ndio wale wa 1995
 
Wakati wa kilimo kufa na kupona na kilimo kwanza wewe ulikuwa hujazaliwa! tatizo nyinyi mbogamboga mnadhan watanzania wa sasa ndio wale wa 1995
Wewe utakuwa ni Mzee mpumbavu.Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inakiri wazi baada ya Nyerere Samia ndio game changer wa kilimo wewe unaleta upumbavu wako kisa wivu.

Haya niambie basi basi wakati mna Kilimo Cha Kufa na kupona mlikuwa na hekta ngapi za Umwagiliaji Kwa miaka 25.
 
SWALI

1.Alipoingia amekuja Mbolea na Pembejeo zikiwa zinauzwaje na yeye baada yakutoa Ruzuku imekuwa bei gani?

2.Hiyo Program ya BBT imewasaidia vijana wangapi na Hekta kiasi gani kimetolewa kwa ajili ya kilimo na hizo Hekta ziko mikoa gani?

3.Vituo gani vya utafiti alipoingia madarakani alikuta vimekufa kwa kutopewa fedha,waweza kuvitaja na kiasi vilichopewa?

4.Hao wataalamu maelfu wa Kilimo walioajiliwa waweza taja idadi yao na Vitendea kazi walivyopewa,na hizo ajira za wataalamu wa kilimo zilitangazwa lini?

5.Hizo skimu mpya za Umwagiliaji zimejengwa mkoa gani na zimejengwa ngapi?

6.Mashamba yapi ya utafiti wa mbegu yalikuwa yamekufa,waweza kuyataja na kuyaorodhesha hapa

7.Wakulima waliotafutiwa masoko ya ndani na nje ni wanaolima mazao gani,na Je kabla yeye hajaingia madarakani serikali ilikuwa inanunua Tani ngapi za mazao?

8.Pesa zinazowekwa kwenye sekta ya Barabara vijijini ni kiasi gani na ni vijijini gani na vingapi vimetengewa hiyo pesa?

9.Amekusudia kujenga visima 65000 kwa pesa zipi?,Kuna umuhimu gani kuwachimbia Visima wakulima wadogo wakati huohuo hawana visima vya maji ya kunywa?

10.Hizo sheria na kanuni zilizobadirishwa ni zipi na zile za mwanzo zilikuwa zipi?,Je hao wakulima ni wakulima wapi wanaokopesheka benki bila mali isiyohamishika?

11.Ni lini kama Taifa lilikumbwa na aibu njaa?
 
Siwezi kujibu kitu Kimoja Kimoja wakati unaweza ingia mwenyewe tovuti ya Wizara ya Kilimo ukapata majibu.

Ukiona wewe ni mbovu wa kutafuta habari tafuta video za Bashe juzi tuu hapo akiwa kwenye Mkutano wa wawekezaji wa sekta ya Kilimo utapata majibu ya maswali Yako.

Pia nimekuwekea video hapo unataka nani akusikilizie?
 
Wewe utakuwa ni Mzee mpumbavu.Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inakiri wazi baada ya Nyerere Samia ndio game changer wa kilimo wewe unaleta upumbavu wako kisa wivu.

Haya niambie basi basi wakati mna Kilimo Cha Kufa na kupona mlikuwa na hekta ngapi za Umwagiliaji Kwa miaka 25.

Sasa hivi mnazo ngapi?
 
Siwezi kujibu kitu Kimoja Kimoja wakati unaweza ingia mwenyewe tovuti ya Wizara ya Kilimo ukapata majibu.

Ukiona wewe ni mbovu wa kutafuta habari tafuta video za Bashe juzi tuu hapo akiwa kwenye Mkutano wa wawekezaji wa sekta ya Kilimo utapata majibu ya maswali Yako.

Pia nimekuwekea video hapo unataka nani akusikilizie?

Haya mambo yanafanyika nchi gani?

Huu upumbavu Tanzania haufanyiki hizo ni siasa tu za kumpamba huyo BI CHAUDELE
 
Back
Top Bottom