Hongera sana Mkuu mpya wa shule ya sekondari Nyiendo halmashauri ya mji wa Bunda kwa uchapakazi uliotukuka

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
201
439
Ukweli ni lazima usemwe tu hata kama watu wengi hawataupenda. Shule ilikuwa imepoteza mwelekeo kabisa.Kila siku ilipokuwa inapita unatamani heri ya Jana.

Makundi baina ya walimu, morali ndogo kwa walimu wasio wanamtandao, kiwango kidogo cha nidhamu kwa wanafunzi yalikuwa baadhi ya mambo yaliyoikwamisha shule kupiga hatua mbele zaidi.

Leo ni miezi miwili tangu uanze kazi.Makundi ya walimu yamekufa na kuzikwa rasmi.Morali ya walimu kiutendaji ipo katika intensity kubwa sana,nidhamu ya wanafunzi imeimarika sana.

Ilifikia hatua mwanafunzi anaingia darasani akiwa na daftari mbili lakini tangu uweke mkazo kila mtoto kuja na daftari zote tisa tena akiwa na begi mwitikio umekuwa mkubwa na tunaamini walimu wenzako,jamii,serikali watazidi kukuunga mkono

Kila la heri madame Neema Michael kuiongoza hii taasisi.

img-20231020-wa0030.jpg
 
Back
Top Bottom