Waraka kwa DED wa Halmashauri ya Mji wa Bunda

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
200
431
Waraka kwa DED wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Emmanuel Mkongo

Heshima yako mkuu!

Nitajitahidi kuandika andiko fupi sana!Nakumbuka kwenye vikao vyako vingi huwa unawaencorage sana wana Bunda kupambana zaidi badala ya kukata tamaa! Awali hawakuweza kukuelewa ila Kwa sasa wamekuelewa vizuri kiongozi.

Mwaka juzi kwenye semina mojawapo ya walimu ulitoa ahadi ukasema umetokea Wilaya ya Arumeru,mahali ambapo kuna shule ya maarufu ya Kisimiri inayoongoza katika mitihani ya kidato cha sita.

Nakumbuka ulisema furaha Yako ni kuona Halmashauri ya Bunda pia inatoa shule Bora.Wengi walijua ni porojo ila kumbe kiongozi ulimaanisha. Majuzi shule ya Bunda High school imeingia katika kundi la shule 10 Bora kitaifa! Haikuwahi kabisa kutarajiwa Halmashauri ya Bunda kutoa shule itakayoingia katika 10 Bora kitaifa.Hongera mkuu kwa hili.

Pia pongezi zaidi kwa ujenzi wa haraka zaidi Kwa shule mpya ya Sekondari inakayojengwa katika kata ya Bunda. Lakini pia miaka ya nyuma wilaya yetu ilikejeliwa Sana Kwa kupata hati chafu kwenye suala zima la matumizi ya pesa. Kila CAG alipokuwa akitoa taarifa zake Bungeni ilikuwa nadra kulikosa jina la Bunda.

Kwa sasa hali ni tofauti,umefanikiwa zaidi kwenye matumizi (expenditures) ya mapato ndani ya halmashauri,uwazi (transparency)ni mkubwa pamoja na uwajibikaji (accountability)

Kuhusu suala la elimu katika halmashauri,imekuwa ni bahati nzuri sana unafanya kazi na maafisa elimu mahiri sana upande wa msingi na Sekondari ndio maana kumekuwepo na ongezeko zaidi la ufaulu katika shule ndani ya halmashauri.

Afisa elimu Sekondari ndani ya hamashauri ya mji hatujui kama tunaweza kuwa nae kwa siku nyingi maana Kwa namna anavyojituma,anavyotumia busara na alivyotengeneza mazingira rafiki Kwa walimu ambaye nae haitashangaza kuhamishwa na kupelekwa wizarani au kupandishwa cheo zaidi!

Bahati mbaya zaidi nafasi ya u-DED siyo ya kisiasa ni ya kiutendaji zaidi ndio maana wengi huwa hawaoni mazuri mnayoyafanya zaidi ya kusubiri mtajwe kwenye mabaya kupitia vyombo vya habari, ila kwa wafuatiliaji wa mambo huwa tunapenda kukosoa au kusifia ili mtu ajifunze hapo hapo!

Kwangu Mimi you are the best DED,Kisha namba pili naitupa Kwa Janeth Muyanja katika historia ya Bunda!

🙏 All the best, chalii ya Chugga!

NB: Maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari kata ya Bunda unavyoendeleakwa Kasi.

FB_IMG_1699601085125.jpg

1.Bunda High School wamefikia hatua hiyo? Hongera sana kwao. Kumbe headmaster Charles Robert Somba anafanya kazi njema.

2.Hapo Idara ya Elimu Sekondari yupo nani? Mr.Kasaba au nani? Anyway, yeyote aliyepo hapo aongeze tu bidii, mamlaka zitamuona. Nakumbuka hata REO wa Mkoa wa Mwanza, Martin Nkwabi, alitokea hapo hapo Bunda.

3.Huyo Janeth Muyanja uliyemtaja ni nani?
 
Migungani ni bunda mjini au bunda stoo

Ni kweli hiyo shule imejengwa kwa kasi ndani ya miezi 2 lakini sio ya bunda mjini ingawa inasemekana bunda mjini imekoswa eneo imejengwa kata ya bunda stoo (mingungani) kama unaenda makaburini na dampo

Suala la accountability na transparency mmh au tuseme yale mamilioni yaliyopigwa wiki 2 zilizopita
 
Migungani ni bunda mjini au bunda stoo
Mtoa mada ila Kuna mgogoro huko Mekomariro vs remng'orori umemshinda kuutatua baada ya kula maokoto. Uongozi wa mkoa nao umeshindwa kuutatua. Ndo unaongeza. Eneo la Kijiji Cha Mekomariro wametenga eneo la kuchungia ila watubwa Serengeti wamavamia

Mkuu wa wilaya alikuja wakaweka bikon za mpaka. Lakn Cha kuskitika Mkuu wa mkoa amekuja na kuwambia watu wajenge.
 
Weka namba ya simu ili TED akuteur uAEK au uHM

Rejea
 
Ngoja makonda aje
 
Yote ayo nayajua mji wa bunda una rushwa huu sijui kwakuwa umesahaulika hela zinapigwa mpaka unasisimka

Mkoa auna stand
Watu wanakunya popote
Masoko ayana taa yamechoka
Miundombinu ya mtela uko mwanjebe ndo kabisa watu wanalia
Mji uko hovyo aujulikani masoko kila sehemu
 
Ni yeye mwenyewe
Weka namba ya simu ili TED akuteur uAEK au uHM

Rejea
 
Back
Top Bottom