Uongozi shule ya sekondari Nyiendo wilayani Bunda mtukumbuke walimu wa kujitolea-Part time teachers

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
200
431
Chondechonde mkuu wa shule, kamati ya uongozi na bodi ya shule ya Sekondari Nyiendo tunawapigia magoti kwa huruma yenu mtusaidie kuhusu mambo yafuatayo.

1. Malipo ya mishahara yetu sasa tunaelekea ndani ya miezi minne hatujalipwa mishahara yetu.Sisi kama binadamu tuna wategemezi,tuna familia, tuna mahitaji binafsi ya kila siku hivyo tunapaswa kulipwa kwa wakati.

Kukaa muda mrefu bila kulipwa inatupunguzia ufanisi wa kazi.Matokeo yake tunaanza kutapatapa namna ya kupata mahitaji yetu ya Kila siku.Hali hii hupelekea tupoteze ufanisi wa utendaji kazi zetu.Matokeo yanapotoka vibaya tunanyooshewa vidole na jamii kwamba hatuwajibiki.Baadhi yetu wameamua kufundisha shule zaidi ya Moja ili wapate mkate wao wa kila siku,siyo kitu kizuri ila watafanya nini ili kuweza kujikimu?Wakati mwingine tunafundisha masomo ya ziada, hili nalo pia tunaishia kupigwa vita kwamba darasani hatuwajibiki ila tuition tunawajibika zaidi.

Ni kweli hali ya pesa ni ngumu ila hatuoni jitihada zozote kuanzia kwa walimu wa madarasa,zamu na mkuu wa shule kuhamasisha wanafunzi kulipa pesa za walimu wa muda.Inashangaza event zisizohusu masomo wanafunzi hulipa sana michango ila linapokuja suala la michango ya walimu wa sayansi,tunabaki wakiwa.
Nitatoa mfano hai;kipindi cha mahafali wanafunzi wa kidato cha nne wamegharamika kuanzia sh 100k +Kwa Kila mmoja ili kufanikisha mahafali kuanzia gharama za mavazi,disco,usafiri na chakula ila sh 6000/=za walimu wa muda zilikuwa ni kizungumkuti!

Nilishangaa kipindi cha kuelekea mahafali walimu walikuwa bize wakizunguka madarasa mbalimbali kutoa elimu na hamasa kuhusu umuhimu wa kuchangia mahafali ila sijui inashindikana wapi kuhamishia hizo nguvu kwenye malipo ya walimu wa muda!

Niliwahi kumuuliza mwalimu mmoja kwa nini walimu wanafanikisha sana upatikanaji wa pesa za mahafali kutoka Kwa wanafunzi mpaka ziada lakini wanashindwa kushirikiana nasi katika kufanikisha pesa za walimu wa kujitolea?Alijibu kifupi tu kwenye pesa ya mahafali Kuna "commission" au keep change hupatikana tofauti na pesa za walimu wa muda.

Kuhusu jambo hili hili la malipo kuna jambo linashangaza kidogo huwa tukifanya ukaguzi wanafunzi wengi huonekana washakamilisha michango yao,sasa huwa tunajiuliza hapa katikati Kuna tatizo gani mpaka tulimbikiziwe hivyo?Pia wanafunzi waliohitimu kidato cha nne miaka ya nyuma wanapoleta pesa zao inaonekana zinakumbana na mazingaombwe" mengi sana!

Ushauri sasa
1.Pesa zilipwe bank badala ya kupokelewa mkononi.
2.Iundwe kamati ya kufanyia auditing michango ya walimu wa kujitolea.
3.Uongozi wa walimu wa part time ubadilishwe
4.Shule itupe ushirikiano kwenye kuhamasisha michango ya walimu wa muda,wasisubiri tu michango yenye maslahi binafsi.
5.Kuiga siyo dhambi tujifunze kwa wenzetu waliofanikisha,wao waliwezaje hili zoezi nasi tunafeli wapi
6.Kwa mwaka huu event kama mahafali wanafunzi wawekewe Sheria kama hajalipa pesa ya walimu wa muda hatoshiriki mahafali
7.Shule zikifunguliwa tuitishe staff meeting na agenda iwe Moja tu kuangalia namna ya kutatua hii changamoto.Walimu wawe huru kutoa mawazo yao
8.Wanafunzi wa kidato cha kwanza mara tu watakaporipoti na kulipa pesa ya walimu wa kujitolea tulipwe pesa walau hata nusu ya deni.

Tusicheze na elimu

Heri ya mwaka mpya na fanaka tele
 
Back
Top Bottom