Hongera Rais Samia! Tanzania kinara biashara Jumuia ya afrika mashariki

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,805
1,872
Ripoti ya benki ya dunia Desemba, 31, 2023. Juu ya mauzo ya bidhaa katika Jumuia ya nchi za Afrika mashariki. Jikite pale tunauza kiasi gani, nasi tunanunua kwao kiasi gani.​
  • Tanzania kwenda DRC (Kongo) -Tzsh 769.6 bilioni. DRC kwenda Tanzania tzsh 6.79 bilioni
  • Tanzania kwenda Burundi-Tzsh 518.09 bilioni. Burundi kwenda Tanzania Tzsh 7.254 bilioni.
  • Tanzania kwenda Rwanda- Tzsh 530.66 bilioni. Rwanda kwenda Tanzania Tzsh4.275 bilioni.
  • Tanzania kwenda Kenya -Tzsh 724.32 bilioni (2021/2022- 993.42bilioni). Kenya kwenda Tanzania Tzsh 1.06 Trilioni (2021/2022- Tzsh 892.82 bilioni.
"Upungufu (2021/2022 -2022/2023) unatokana na sintofahamu (hali ya kisiasa) iliyoendelea nchini Kenya (2022/2023/" -alisema mtaalamu wa masuala ya biashara" - Oscar Mkude

Biashara kwa ujumla Jumuia ya Afrika masharika 2022/2023 , Tanzania iliuza katika nchi za Afrika masharika jumla ya bidhaa zenye dhamani ya Zaidi ya 3,26 Trilioni Tzsh, huku ikinunua bidhaa zenye dhamani ya 1.37 Tz sh Trilioni.
Chanzo:
  1. Kenya yapindua meza biashara na Tanzania
  2. Benki ya Dunia.
My take. Rais Samia anafungua nchi, watanzania tumuunge mkono. Pili, tumpe maua yake kwani EAC ni tegemeo la kuongeza ajira Tanzania. Tumpe Maua yake.
 
TZ kwenda DRC bado tuko chini sana, kwa ukubwa wa ile nchi inatakiwa tupambane ifikie 10x
 
Ni kweli, nakubaliana nawe asilimia 100, tena si DRC tu bali nchi zote EAC. Ndio maana nawaomba watanzania tumuunge mkono kwa kuchangamkia Fursa hizo, hasa kipindi hiki ambapo ajira ni changamoto.

Isitoshe mambo mengi yaliyokuwa changamoto huko nyuma baina ya nchi na nchi, au jamii ya nchi moja kwa jamii ya nchi nyingine yameondolewa.
Kumbuka DRC imejiunga katika jumuia mwaka juzi tu.
 
Je, Hivi vikwazo vilivyopo nani amesababisha viwepo???
Hizi nchi zetu za kiafrika bado tunatatizo (adui) kubwa moja "UJINGA". Kila nchi inafikiri mwenzake atafaidika sana akifungua milango kwake. Na biashara za bidhaa zinaanza na watu kutembeleana katika nchi jirani na kuona fursa.
Leo hii mgeni toka bara jingine anathamani kubwa kuliko muafrika mwenzako wa nchi jirani.
Katika mabara yote duniani, bara ambalo wananchi wake wana vikwazo sana kutembeleana kati ya nchi na nchi ni Afrika.
Kwa hiyo vikwazo vimeanza kuwekwa kwa mimi na wewe na wakazi wote wa Afrika (Afrika mashariki) kutokubali kukaribishana na kuheshimiana. Hili si la viongozi tu.
Hapo ndipo pa kuanzia, na Rais Samia amedhamiria kuvunja vunja hiyo aibu.
 
Mbona hujajibu swali uliloulizwa? Nani aliifunga nchi? Nani aliyesababisha vikwazo viwepo? Hayo ndio maswali ya msingi uliyoulizwa.
 
Back
Top Bottom