Miaka 3 ya Rais Samia Demokrasia imeimarika tukizishinda nchi zote za Afrika Mashariki. Hongera sana Kwake!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,994
Leo 19/03/2024 Rais Dr Samia Suluhu Hassan anatimiza Miaka 3 ya Uongozi wake kama Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu

Nchi za Africa Mashariki zimekuwa na tatizo kubwa la Demokrasia na Tanzania ilikuwemo lakini jambo kubwa sana alilofanya Rais Samia ni kurejesha Misingi ya Demokrasia iliyokuwa imefifia

Kwa sasa Vyama vya Siasa na Taasisi za Dini ziko huru kufanya Shughuli zao zote bila kuingiliwa na Serikali

Hii ni hatua kubwa sana kwa sababu Demokrasia ndio baba na mama wa Maendeleo

Mungu wa mbinguni endelea kumbariki Rais Samia

Ramadan Mubarak 😄
 
Wenyewe hao mademocraticas wanasema kenya ndio ina demokrasia kwa waweza mpiga kibao ruto na kunya bustan ya ikulu usifanywe kitu!
 
Bwashee,
Bado tuna safari ndefu ili tufikie demokrasia ya kweli.
Baadhi ya mambo muhimu ambayo bado hayapo:
1. Katiba mpya inayobeba matakwa ya wananchi
2. Tume huru ya uchaguzi itakayotoa fursa kwa sanduku la kura kuheshimiwa
3. Bunge huru, yaani ambalo siyo chawa wa serikali
4. Mahakama huru inayoamua kesi bila maelekezo kutoka muhimili wa serikali
 
Ni kweli

Lakini safari ni hatua tumeanza Vizuri
 
Leo 19/03/2024 Rais Dr Samia Suluhu Hassan anatimiza Miaka 3 ya Uongozi wake kama Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu

Nchi za Africa Mashariki zimekuwa na tatizo kubwa la Demokrasia na Tanzania ilikuwemo lakini jambo kubwa sana alilofanya Rais Samia ni kurejesha Misingi ya Demokrasia iliyokuwa imefifia

Kwa sasa Vyama vya Siasa na Taasisi za Dini ziko huru kufanya Shughuli zao zote bila kuingiliwa na Serikali

Hii ni hatua kubwa sana kwa sababu Demokrasia ndio baba na mama wa Maendeleo

Mungu wa mbinguni endelea kumbariki Rais Samia

Ramadan Mubarak 😄
Vipi kuhusu Hali ya maisha na sukari ,unga,Mchele au wewe unakula demokria, vipi Kuna Mladi wowote WA maana umeanzishwa Tanzania au anaendeleza ya Yule aliyewadhibiti lakini tulikuwa tunaona maendeleo na maisha yalikuwa chini .
 
Maendeleo ya watu; vitu kwa ajili ya watu, sio watu kwa ajili ya vitu.
Haikuwa hivyo Toka Mwanzo

Mtu aliumbwa atawale hivyo vitu

Ndio yule Ibilisi Shetani akaleta kitu kiitwacho Demokrasia na kuiteka dunia
 
Vipi kuhusu Hali ya maisha na sukari ,unga,Mchele au wewe unakula demokria, vipi Kuna Mladi wowote WA maana umeanzishwa Tanzania au anaendeleza ya Yule aliyewadhibiti lakini tulikuwa tunaona maendeleo na maisha yalikuwa chini .
Safari ni hatua

Nyie badala ya kuchapa kazi mnakimbilia kuandamana

Mnadanganywa tu Wenzenu akina Boni Yai na Sugu wanauza Mayai na Maharage
 
Back
Top Bottom