chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,681
Hatimaye, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, nahodha Samia Suluhu Hassan amekifikisha chombo mwisho wa mwaka 2023 kikiwa salama, hakuna hata aliyechubuka.
Ni safari ndefu yenye mawimbi makali, ambayo, kama si umahiri na weledi wa nahodha, ingetuwia ngumu.
Tanzania ndio muhimili wa amani Afrika Mashariki, hata vile vidume vilivyozoea kupigana vita, vikimuona mwamba wa visiwa vya karafuu na mlima kilimanjaro, vinaufyata na kusikiliza. Amedhibiti usalama wa nchi ndani na nje.
Uchumi umesheheni mafuta mafuta (mazezele), siasa zimejaa bashasha, watu wanapaa na ilani kwa helkopta, wanashuka, mpaka baadae wanakaa chini wanajiuliza, hivi tuseme nini tena, mbona anafanya yote?
Treni zinashuka bandarini, SGR inakwenda mwendo wa ngiri mkia juu, daraja la Magufuli, pale jangwani kitasukwa kitu cha kihistoria, daraja bora kabisa na uboreshaji wa matumizi ya ardhi, TARURA wamezagaa nchi nzima wakijenga barabara, Tanroad wamegoma kutoka saiti hata siku za sikukuu wako kazini.
Utumishi wa umma umetulia sasa, watu wamepanda madaraja mpaka wanashangaq, tukimpa mitano tena, watapanda hata ndege. Wale wanasiasa waliokuwa wanaficha udhaifu wao na kusumbua watumishi wamekomeshwa.
Sekta ya afya inawaka kama taa, inaenda kitaalamu, awamu ya sita inaheshimu sayansi, haikupigana ngumi za uso kwa uso na corona, iliruhusu sayansi itamalaki, yule aliyetaka kuzipiga kavukavu na korona, korona ilimkoroga kwa Knock out.
Viva Samia.
2024, tunatarajia mengi, tutapanda treni ya umeme kwa mara ya kwanza tangu Mungu aumbe ardhi ya nchi hii, na ile meli ya MV. Mwanza, sisi wahaya tuseme nini sasa? Tutabeba ndizi na senene humo tupeleke masokoni. Umeme ukiwaka kutoka bwawa la Mwalimu Nyerere? Ni kazi yako hiyo, chief engineer! Daraja la Busisi? Wana kanda ya ziwa umetuachia kumbukimbu kubwa sana, sengerema itakuwa, Geita, Mwanza, Kagera, Musoma, na umeme wa Rusumo, ni wewe Mama.
Tuko na wewe 2024, tukiwa na jembe kuelekea mashambani kuzalisha mali, na nyundo kwenye shughuli zetu za viwanda, biashara, na mengine mengi.
Unaukumbuka ule wimbo wa Kigoma mbali kwa wali ni karibu? Sasa hata bila wali, Kigoma, Katavi, Rukwa imefunguka kwa kupitia Mbeya au Tabora. Lami imechapwa ikachapika kwa barabara zote.
#ChamaKikoKazini
2024 twende tukajenge nchi yetu kwa nguvu zaidi na weledi mkubwa.