Ndugu Mussa Mbura: Miaka Mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan Mapato ya Viwanja vya Ndege (TAA) Yameongezeka Kutoka Bilioni 71.42 Hadi Bilioni 128.84

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura amezungumzia mafanikio ya Viwanja vya Ndege nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jinsi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ilivyoweza kuboresha miundombinu mbalimbali

"Mafanikio yaliyopatikana kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwezesha Viwanja vya Ndege kufanya kazi kwa masaa 24. Uwanja wa Ndege wa Dodoma unafanya kazi masaa 24. Tumefunga taa kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Mtwara, Songea, Songwe" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Rais Samia ametoa zaidi ameweka bajeti kubwa kuhakikisha sekta ya Kilimo inakua, kumekuwa na ongezeko kubwa la mizigo inayosafirishwa nje ya nchi, mazao yanayoharibika kwa haraka kama Mbogamboga na matunda. Airport za Tanzania zilikuwa hazipati Muunganiko wa kimataifa ya ubora wa bidhaa zinazosafirishwa kupitia Airport" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"TAA, Machi 2024 tumeweza kutunukiwa na kutambuliwa na International Air Transport Association (IATA) tukapewa cheti cha ubora kwamba sasa tumekidhi vigezo vya kimataifa vya kuweza kusafirisha mazao yanayoharibika kwa haraka (Perishables) kupiga Uwanja wa Ndege wa JNIA" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Kipindi cha Miaka Mitatu Madarakani ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, TAA tumeweza kuvutia Mashirika mengine ya Ndege ya kimataifa kuja nchini na kuanza safari kutoka kwenye nchi hizo kuja moja kwa moja mpaka Tanzania" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Miaka Mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan kumekuwa na ongezeko la Mashirika ya Ndege makubwa; Air France, Saudia Airlines, South Africa (Airlink). Jumla ya Mashirika ya Ndege ya Kimataifa yamefikia 21 yanayofanya ratiba moja kwa moja kuja nchini JNIA kwa ratiba" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Ongezeko la abiria na mizigo Airport imepelekea ongezeko la mapato kwa kiwango kikubwa sana katika viwanja vya ndege. Tumetoka Bilioni 71.42 mwaka 2020-2021 mpaka Bilioni 128.84 mwaka 2022-2023. Mapato yataongezeka zaidi ifikapo 2023-2024. Hili ni ongezeko la zaidi ya asilimia 80" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege

"Kiwanda cha kwanza cha kuunganisha na kutengeneza Ndege sasa hivi kipo Tanzania, Kiwanda kipo kwenye Airport ya Mkoa wa Morogoro. Kiwanda kinamilikiwa na kampuni ya Airplane Africa Limited. Mpaka sasa zimeshaunganishwa Ndege tatu, hizi ni Ndege ndogo za kuweza kubeba abiria wawili mpaka wanne" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
 

Attachments

  • 4a-1-1024x683sax.jpg
    4a-1-1024x683sax.jpg
    70.4 KB · Views: 3

Similar Discussions

Back
Top Bottom