unasahau kuna sahihi ya mrema na wana cuf wale mnaosemaga wameolewa na ccm hapo,msipende cheap poularity nyie,na hapo mngependa aanzishe mwingine huko cdm sio zitto maana kiukweli hamnaga mapenzi nae,hapa mnajichekesha kwake kinafiki tu
Zitto is an independent organ ndani ya CDM! Ana msimamo na anajua anachokifanya. Yupo tofauti kabisa kimaamuzi na wabunge wengine wa CDM. Ndio maana hata njaa za vihela vya posho hana!!
Hivi sisiemu walipoiba hoja ya katiba mpya pia ulitufahamisha? hebu nikumbushe kidogo, au wakati huo hukuwepo nchini!
umesahau kuwa aliyeanzisha mjadala wa kumpigia pinda no confidence ni lissu bungeni kabla zitto kuiendeleza,kwani zitto anatoka chama gani?roho inakuuma,unatamani kujiunga cdm ila unaona aibu kula mitapishi yako!
Kwa kuongezea mie nimehesabu na kukuta katika hao 71 wabunge toka CHADEMA ni 40 sasa sijui alitaka ushahidi uweje ili aamini kwamba CHADEMA ndiyo yenye uchungu na wananchi wa Tz. Lakini nipende kuwapongeza wajumbe toka NCCR-Mageuzi, TLP na CUF kwani wameungana na waanzisha kupambana na ufisadi nchini. Yawezekana kabisa hao watuhumiwa siyo mafilauni kwa kiasi hicho lakini usimamizi mbovu katika maeneo yao inatosha kabisa kuwaondoa kwa nanma yoyote ile.
Jifunze siasa wewe mkuu,
sisim kuanzisha ile hoja ilikuwa ngumu kidogo ila walitaka waropokaji waanze kisha wao waisimamie, huoni sasa sisim ndio wasimaiaji wa kuu wa mchakato?
ULITAKA AONGEE KINGEREZA KAMA ANAANDIKA KISWAHILI..Wabongo kwa kujifanya wanajua kingereza hamjambo...
Tambwe Hiza, aliyepaswa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni mtoa hoja wakati akihitimisha hoja yake. CDM wana mwenyekiti mmoja tu wa kamati ya kudumu. Sasa huyo mwingine uliyetaka wewe atoe hoja angekuwa nani? Cheyo, Mrema ama nani? Acha kukurupuka bwana Hiza.unasahau kuna sahihi ya mrema na wana cuf wale mnaosemaga wameolewa na ccm hapo,msipende cheap poularity nyie,na hapo mngependa aanzishe mwingine huko cdm sio zitto maana kiukweli hamnaga mapenzi nae,hapa mnajichekesha kwake kinafiki tu
Ningependa kuweka sawa hili,kumekuwepo na upotoshaji wa makusudi wa genge la watu wa chama kimoja cha siasa kutaka kuteka ama kudandia hili suala la waheshimiwa wabunge wa bunge letu kutaka kuwasilisha hoja ya kuibana serikali na kulifanya ni lao kwa maana la iko chama chao kitu ambacho si kweli.Sababu za genge hilo kifanya hivyo kwanza ni kuupotosha umma na kuondoa umuhimu na unyeti wa suala lenyewe lakini pili ni kujaribu kukipatia chama iko cheap popularity na kukifanya kionekane ndio kaka mkuu mwenye uchungu zaidi na nchi hii kitu ambacho si kweli kwani wabunge wa chama iko ukimuacha MH.ZITTO bado wameendelea kutubebesha mzigo mkubwa walipa kodi kwa kupanga foleni ya kuchukua posho ya kukaa tu kitako pale bungeni.
Sasa ili kuweka kumbukumbu sawa na kuzuia upotoshaji huo wa makusudi unaofanywa na hilo genge la chama iko nimeamua niwaletee orodha ya waheshimiwa waliolishikia bango suala hili na vyama wanavyotoka kwa vitendo then mpime wenyewe na kuona kama chama iko kinastahili kubeba ushujaa wa hili ama kinajaribu kuteka hii hoja ili kujinufaisha kisiasa.Majina ya wabunge waliotia saini hoja ya mh.zitto kabwe
- Mhe. Rashid Ali Abdallah – CUF
- Mhe . Chiku Aflah Abwao- CHADEMA
- Mhe . Saluim Ali Mbarouk – CUF
- Mhe . salum Khalfam Barwany – CUF
- Mhe . Deo Haule Filikuchombe - CCM
- Mhe.Pauline Philipo Gekul - CHADEMA
- Mhe. Asaa Othman Hamad - CUF
- Mhe. Prof.Kuliyokela Kahigi- CHADEMA
- Mhe.Naomi Mwakyoma Kaihula – CHADEMA
- Mhe . Sylvester Kasulumbayi - CHADEMA
- Mhe. Raya Ibrahim Khamis - CHADEMA
- Mhe. Mkiwa Hamad Kiwanga - CUF
- Mhe. Susan Limbweni Kiwanga - CHADEMA
- Mhe. Grace Sindato Kiwelu – CHADEMA
- Mhe. Kombo Khamis Kombo – CUF
- Mhe. Joshua Samwel Nassari – CHADEMA
- Mhe. Tundu Antiphas Lissu - chadema
- Mhe Aphaxar Kangi Lugola - CCM
- Mhe susan Anselim Lymo - CHADEMA
- Mhe. Moses Machali – NCCR Mageuzi
- Mhe. John Shibuda Magalle – CHADEMA
- Mhe. Faki Haji Makame - CUF
- Mhe . Esther Nicholas Matiko - CHADEMA
- Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi - CHADEMA
- Mhe. Freman Aikaeli Mbowe - CHADEMA
- Mhe. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – CHADEMA
- Mhe. Halima James Mdee - CHADEMA
- John John Mnyika - CHADEMA
- Mhe. Augustino Lyatonga Mrema - TLP
- Mhe . Maryam Salum Msabaha - CHADEMA
- Mhe. Peter Msingwa - CHADEMA
- Mhe. Christowaja Gerson Mtinda - CHADEMA
- Mhe. Philipa Geofrey Mturano - CHADEMA
- Mhe. Christina Lissu Mughwai - CHADEMA
- Mhe. Joyce John Mukya – CHADEMA
- Mhe. Mchungaji Israel Yohane Natse – CHADEMA
- Mhe. Philemon Ndesamburo- CHADEMA
- Mhe. Ahmed Juma Ngwali - CUF
- Mhe. Vincent Josephat Nyerere - CHADEMA
- Mhe. Rashid Ali Omar - CUF
- Meshack Jeremiah Opulukwa - CHADEMA
- Mhe. Lucy Philemon Owenya - CHADEMA
- Mhe. Rachel Mashishanga - CHADEMA
- Mhe. Mhonga Said Ruhwanya – CHADEMA
- Mhe. Conchesta Rwamlaza – CHADEMA
- Mhe. Moza Abedi Saidy - CUF
- Mhe. Joseph Roman Selasini – CHADEMA
- Mhe. David Ernest Silinde - CHADEMA
- Mhe Rose Kamili Sukum - CHADEMA
- Mhe. Cecilia Daniel Paresso - CHADEMA
- Mhe. Kabwe Zuberi Zitto - CHADEMA
- Mhe. Magdalena Sakaya – CUF
- Mhe Rebecca Mngodo - CUF
- Mhe. Sabreena Sungura - CHADEMA
- Mhe. Hamad Rashid Mohammed- CUF
- Mhe. Rukia Kassim Ahmed (CUF)
- Mhe. Mustapha Boay Akoonay (CHADEMA)
- Mhe. Abdalla Haji Ali (CUF)
- Mhe. Khatibu Said Ali (CUF)
- Mhe. Hamad Ali Hamad (CUF)
- Mhe. Riziki Omar Juma (CUF)
- Mhe Haji Khatibu Kai (CUF)
- Mhe. Anna Marystella John Malack - CHADEMA
- Mhe. Hamad Rashid Mohamed (CUF)
- Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed (CUF)
- Mhe. Thuwayba Idrissa Muhamed (CUF)
- Mhe. Masoud Abdallah Salum (CUF)
- Mhe. Muhamad Ibrahim Sanya (CUF)
- Mhe. Ali Khamis Seif (CUF)
- Mhe. Haroub Muhammed Shamis (CUF)
- Mhe. Amina Amour Nassoro (CUF)
Nawasilisha
Chama | Idadi yao bungeni | Idadi ya Waliosaini | % of their total | % of the total in parliament | Position by percentage of the total |
CCM | 266 | 2 | 0.75 | 0.56 | 3 |
CHADEMA | 48 | 40 | 83.00 | 11.23 | 1 |
CUF | 36 | 27 | 75.00 | 7.58 | 2 |
NCCR | 4 | 1 | 25.00 | 0.28 | 4 |
UDP | 1 | 0 | 0.00 | 0.00 | 5 |
TLP | 1 | 1 | 100 | 0.28 | 4 |