CCM yampinga Balozi Karume/ACT-Wazalendo. Yasema Upinzani haujawahi kushinda Zanzibar

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema madai ya Balozi Ali Karume kuhusu uchaguzi mkuu akisema CCM haikushinda si mageni kwani aliyekuwa Makamo Mwenyekiti CUF Mussa Haji Kombo amewahi kutamka mgombea urais wa CUF hayati Maalim Seif Sharif Hamad hakuwahi kushinda urais .

Hadi leo hakuna ushahidi wowote unaoonyesha upinzani umeshinda kama ACT-Wazalendo kinavyotaka kueneza madai hayo.

Ufafanuzi huo umetolewa na katibu wa kamati maalum ya NEC-Zanzibar , Mbetto Khamis Mbetto , akijibu tuhuma za Katibu wa Habari,Uenezi na Mawasiliano kwa umma , Salum Bimani alipohutubia mkutano wa hadhara huko.....

Mbetto alisema madai ya baadhi ya wanasiasa ambao matlaba yao kisiasa hayakufikiwa na kutamka majukwaani kuhusu uchaguzi , wana hamaki na jazba ili kuvuruga upepo pale wanaposhindwa au wakipovuliwa uanachama.

Alisema Kombo na Karume hawajawahi kuwa wenyeviti au maafisa wa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) hivyo hawana haki kimamlaka na kisheria kusikilizwa au kuzungumzia matokeo ya uchaguzi wakati wowote.

"Madai ati CCM haijashinda wakati inaongoza Serikali ni upuuzi unaostahiki kupuuzwa. Hata Kombo amewahi kusema Maalim Seif hakushinda uchaguzi wowote Zanzibar . Maalim seif na kina Bimani hawajakanusha madai hayo mpaka leo "Alisema Mbetto.

Aidha katibu huyo Mwenezi CCM Zanzibar alisema kinachoonekana kwa viongozi wa ACT-Wazalendo wanataka kuibeba kauli ya Balozi Mstaafu Karume wakidhani utakuwa ndio mtaji mpya kisiasa utakaowapa manufaa .

"CCM iweje kisishinde wakati ndicho kinachoaminiwa na wananchi. Wazanzibari si wajinga hadi wauchague upinzani kwa kubahatisha . CCM kimeshinda chaguzi zote na kitaendelea kushika madaraka na kuiongoza Zanzibar" Alisisistiza

Katibu huyo Mwenezi alidai kombo aliwahi kusema CUF kulikuwa na uhodari wa kueneza propaganda hasi kwa nguvu hasi zikakubalika kitaifa na kimataifa na kulikuza jambo lolote lakini hakuna ushahidi CUF au ACT-Wazalendo vilishinda.

"CUF walitaka wawe na makamishna wao ndani ya ZEC pia hawakushinda. Wakataka Daftari la kudumu la wapiga kura hawakupata ushindi . Wakaomba kuwe na kadi za mzanzibar mkaazi hawakupata ushindi. Ni chama kisicho na sera za matumaini hivyo ni vigumu​
 
Kama Ccm haijawahi kushinda Zanzibar ilikuaje Yeye Ally Karume akakubali kuwa Waziri katika Serikali haramu iliyoingia kwa haramu ?

hivi kama Hussein Mwinyi asingekata na kung'oa Mirija ya Ally Karume kwny madili ya Karume Airport na ukodishwaji wa visiwa angeongea aliyoongea?

ifike hatua Familia ya Karume ijue haina hatimiliki ya Siasa za Kisiwandui …mbona familia ya Julius Nyerere imetambua kuwa zama zao zimekwisha kwenye Siasa za Chimwaga na Kizota japo Baba yao alifanya mengi na makubwa kwa Nchi?
 
The bitter truth to cope with , ni kwamba wa Le republica de kusadikiker won't last forever. Hata hii generation yetu isiposhuhudia , maybe the next .
 
Back
Top Bottom