Hoja ya Zitto sio ya CHADEMA

ushasema jeshi so ni wazi hakunaga jeshi la mtu mmoja lakini haimaanshi hii ni hoja ya chadema no,ni hoja ya wabunge kufuatia ripoti ya cag ndio maana mnaona kuna sahihi mpaka ya mrema na cuf ambao hamuishi kuwatukana humu kwamba wameolewa na ccm kama mnavyompondaga zitto kwa kumuita kibaraka wa ccm,leo ndio huyo kashirikiana na wabunge wenzake kutoka vyama vyote

sikujua kama na wewe ni masaburi?
 
Hoja ilikotoka kila mtu amafahamu suala la kupata sahihi 70 (20%) ni kuwa haliwezi kufanywa na chama kimoja lazima waungane maana CCM wao hawawezi kulianzisha. Msingi hapa ni kuweka tofauti hizi (ndogo) pembeni na "kumshika huyu bull by the horn" ili adabu na heshima ya watanzania irudi hawa Mawziri including Pinda wanafikirikuwa hakuna wa kuwafanya kitu!
 
Kuendelea kujadili hii hoja ni kung'oa mbegu za uzalendo na Utaifa. Yawezekana ndiyo lengo la mtoa mada.
 
Ushasema jeshi so ni wazi hakunaga jeshi la mtu mmoja lakini haimaanshi hii ni hoja ya chadema no,ni hoja ya wabunge kufuatia ripoti ya CAG ndio maana mnaona kuna sahihi mpaka ya mrema na cuf ambao hamuishi kuwatukana humu kwamba wameolewa na ccm kama mnavyompondaga zitto kwa kumuita kibaraka wa ccm,leo ndio huyo kashirikiana na wabunge wenzake kutoka vyama vyote

Nakubaliana nawe japo kwa kiasi fulani,japo hii hoja imesimamiwa kwa dhati na wabunge wa cuf,nccr na cdm,wabunge wa c.c.m pamoja na wingi wao wameonyesha ni wasaliti kwa wananchi na ni wachumia tumbo,wanaotetea maovu ya chama chao na serikali yao,wale wabunge wachache wa c.c.m walioonyesha kutokua na uoga dhidi ya uozo huo,wameonekana ni wasaliti kwa chama chao na no wonder wakija kutoswa huko mbeleni,na uzuri hata wenyewe wamekiri kulijua ilo na wako tayari kwa lolote!
 
Mijitu mingine imeletwa duniani kuvuruga mshikamano wewe ni mwoja wapo
 
Sema Hoja ya Zito ni ya CCM au CUF au NCCR... Wewe ni mnafiki mkubwa, na wewe miongoni mwa wanaowagawa wananchi wa Nchi na ndiyo mnaomdanganya Zito ajione anapigana hivi vita mwenyewe.

Hoja kupambana na Ufisadi nchi hii hata ukienda kumwuliza mtoto wa Chekechea anajua kuwa ni ya Chadema na si Chama kingine wala si ya CCM wala CUF.

Practicali tushaona CDM imeongoza Halimashauri kibao na hakuna ufisadi kwenye hizo halimashauri.

Sasa Leo mtu wa CUF unakuja eti hoja ya ZITO si ya CDM ni ya nani labda useme ni ya kwako au Chama chako
 
Cjajua bado una nia gani maana ndo kwanza nasikia kwako kuna chama kinachotaka kujinufaisha kisiasa na mpango huo wakumng'oa waziri mkuu na kwanini sisi tusiamini kuwa wewe ndo unataka kulifanya hilo suala lionekane ni la kichama na pia hata kama nila kichama pia lina manufaa kwa taifa kwa ujumla hata kama litanufaisha chama. Ni tofauti na ccm kutaka kunufaishwa kwa kutuibia na kutukandamiza
 
...Hoja hii so ya chama chochote cha siasa, ni hoja kwa manufaa ya uwajibikaji ndani ya Serikali, na imepata nguvu kwa sababu ya mwelekeo wa Wabunge wa vyama vyote kuunga mkono hatua za kuwawajibisha Mawaziri...

...Mwenye akili yoyote na anayeiunga mkono hoja hii kwa manufaa ya mama Tanzania, hataihusisha kamwe hoja hii na chama chochote cha siasa, kwani kufanya hivyo ni kuwatenganisha wabunge na kupelekea kuiua hoja hii kabla haijakamilisha kusudio lake, na hii ni hekima...

...Zitto yupo juu ya siasa za vyama bungeni, na tunahitaji Wabunge wengi zaidi bungeni wanaoweza kusimamia maslahi ya nchi bila kujali manufaa ya vyama vyao, Ebu tumwache Zitto mwenyewe aseme....

LUKAZA: Hoja ya Zitto ya kutaka Waziri Mkuu Pinda apigiwe Kura ya Kutokuwa na Imani naye yakwama kutokana na kanuni za Bunge

...Amesema wabunge wa vyama vyote wamesaini ispokuwa UDP na kwamba, uongozi wa CUF umetoa maelekezo maalumu kwa wabunge wake kusaini.

...Zitto amesema hoja hiyo ni ya wabunge wote bila kujali itikadi za vyama na lengo ni kutengeneza Bunge la utendaji badala ya kulalamika.


Iwapo hoja hiyo itapitishwa na Bunge, Pinda atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.


Zitto amesema kuwa wanatarajia kuwasilisha hoja hiyo kwa Spika wa Bunge, Jumatatu kwa ajili ya hatua zaidi....

 
Mtoa mada, Naona anajaribu kuwa Alchemist, anataka kutengeneza dhahabu kutoka kwenye mchanga.

Hakuna Zitto (Mbunge) bila CHADEMA (Chama), ila kunaweza kuwa na Chama CHADEMA bila Mbunge Zitto. Huwezi kumtenganisha yeye na chama chake, haijalishi anafanya mambo ya aina gani, mazuri au mabaya.

Wewe mwenyewe umethibisha hili kwenye post yako, kwa nini unahusisha uchukuaji wa posho na chama cha CHADEMA? Au kwa sababu sio jambo zuri kisiasa?

Mabaya na mazuri ya wabunge wa CHADEMA ni ya CHADEMA.
 
hapo wa ccm ni mmoja tu,wengi ni cdm wakifuatiwa na cuf, ni ya kwako?
 
Pro-Chadema JF siku zote humu Jamvini wanasema Zitto ni pandikizi la CCM ndani ya Chadema leo kapambana mwenyewe kupeleka hoja ya binafsi mnatuambia katumwa na Chadema.

Zitto nimpambanaji anapambana kulipigania taifa letu ndio maana unaona kaungwa mkono na wabunge wengi kutoka vya vya siasa.

Ukweli hoja ni ya Zitto sio ya Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Acha uhuni wewe Zitto ni Naibu kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani na unajua chadema hiwa hatukurupuki hiyo hoja ilikuwa organized! Siku zote cdm tuko ahead ya magamba! Jitihada zenu za kumu isolate Zitto na cdm hazitafanikiwa!
 
Zitto ndiye mwanapinduzi wa kweli though ni snitch. Hoja ni ya Zitto kama ilivyoelezwa na si ya CDM. CDM ni wanafiki, wanajidai wanaipenda nchi yao kumbe wanawapaka tu wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa.

Siku wabunge wa CDM watakapoacha kuchukua posho za vikao, nitajua kweli wapo serious na machungu na nchi yao!
 
Katika watu ambao hawatumii akili kufikiri KIMKARDASH ameongoza.

Hoja siku zote zinaanzishwa na mtu moja, sasa kinachotakiwa ni akina nani wanaiunga mkono.
Ndicho kilichotokea kwenye pendekezo la zitto, aliyetaka mbunge yeyote aliyekerwa na wizi ule kuweka sahihi ya kuwasilisha hoja kwa spika.
Sina hakika kama majina yaliyowekwa humu ndivyo yalivyo kwenye karatasi ya zitto, lakini la msingi ni kwamba hoja imeungwa mkono na wabunge wa pande zote.
 
Kuna shabiki mmoja wa Chadema anakaa maeneo ya Kimara anawambia jamaa zake kuwa Zitto katumwa na Slaa kupeleka hiyo hoja.
 
WEE KARDASH muda mrefu nakuona unaishabikia ccm bila fact bt kuishabikia ccm shurti uwe na akili ya maiti,hoja yako haina mashiko.mbona ulisemaga kauli ya MTEI ni ya chadema? Sasa zitto nae c chadema.what u expert there
 
Back
Top Bottom