ComputersDAR
JF-Expert Member
- Jan 21, 2013
- 213
- 241
Au ni mimi tu siyo sielewi chanzo cha huu mgao unaondelea sasa mwezi Novemba umeanza? Sasa hivi wamekata tena umeme na utarudi baada ya giza.
-
-
Kwakuwa TANESCO walisema tatizo la umeme linasababishwa na "Kupungua" kwa kina cha maji kwenye ma Bwawa yetu, na ni baada ya kuwahadaa wananchi kwa mda mrefu wakisingizia mara kuna matengenezo mara itilafu ya mitambo na baadae kuitimisha ni kina cha maji ndio tatizo.
Watanzania tunajua tatizo la Umeme ni la kisiasa lakini hatujuwi tija yake kisiasa ni nini. Fikiria adi Marehemu Rais Maghufuli alilalamika kuna watu wana hujumu Tanesco ili wauze mafuta na vilevile bwawa limejaa matope kwa makusudi ya watu.
Kumbuka huyo ni alikuwa Rais akilalamika baada ya kutonywa na wale wa "Upande wa pili".
Naomba kuuliza ili li TANESCO ni kwamba lenyewe ni likubwa kupita taasisi ya Rais, Waziri Mkuu, Bunge hata Jeshi kwa ujumla wao.
Umeme ni uchumi wa Nchi
Umeme ni Usalama wa Nchi
Umeme ni Ulinzi wa mali za wananchi
Lakini ni Tanzania peke yake inayochukulia umeme kama Anasa ya Nchi.