TANESCO: Dar es Salaam kuanzia leo Februari 23 hakutakuwa na mgawo

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema kuwa kwa jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Ijumaa ya Februari 23 hakutakuwa tena na mgao wa umeme.

Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha GOOD MORNING kinachorushwa na kituo cha redio cha WASAFI FM asubuhi hii.

===
Tumekuwa tunafanya kazi hii ya kuratibu upatikanaji wa umeme katika maeneo mengi ya nchi yetu bila kutoa upendeleo, lakini kwa kuzingatia kiwango cha umeme ambacho kinazalishwa"

Kuanzia jana usiku (Februari 22, 2024) kuna jitihada kubwa ambazo zinaendelea kufanywa na Serikali pamoja na Shirika kwa ujumla, kuanzia jana usiku maeneo yota ya Kinondoni yamekuwa yanapata nishati ya umeme. Maneno yote ya Temeke yamekuwa yanapata nishati ya umeme, maeneo yote ya Ilala yamekuwa yakipata nishati ya umeme na maeneo yote ya Kigamboni yamekuwa yakipata nishati ya umeme. Maana yangu ni kwamba kuanzia jana usiku, mkoa wa Dar es Salaam wote umekuwa ukipata nishati ya umeme.

Lakini kama hiyo haitoshi, kuanzia leo Mkoa wa Dar es Salaam wote utakuwa ukipata nishati ya umeme na hali hiyo tunategemea itaendelea kuwa hiyo siku zinavyozidi kwenda.

Jitihada kubwa zinaendelea kufanyika kuhakikisha kwamba hali hii inakuwa ya uimarikaji na ya uendelevu kutokuwa na upungufu wa umeme Katika mkoa wa Dar es Salaam lakini pia hali hiyo tutaanza kuiona Siku za hivi karibuni kwenye mikoa mingi, kama siyo yote ya nchi yetu ya Tanzania.
 
Watawaambia matengenezo ya Nguzo na mitambo..
Sasa wapigieni simu waambie Mnatengeneza sehemu gani?
Wakiwajibu wanakotengeneza niambieni..
Na kama wakishawajibu hakikisheni kweli wana matengenezo Sehemu hizo..
#Siasa imeingilia Proffesionalism
 
Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema kuwa kwa jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Ijumaa ya FEBRUARI 23 hakutakuwa tena na mgao wa umeme. Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha GOOD MORNING kinachorushwa na kituo cha redio cha WASAFI FM asubuhi hii.
Ni mapema sana kuwaamini sisiem
 
Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema kuwa kwa jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Ijumaa ya FEBRUARI 23 hakutakuwa tena na mgao wa umeme. Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha GOOD MORNING kinachorushwa na kituo cha redio cha WASAFI FM asubuhi hii.
"Siwezi kusema mgao wa umeme utaisha lini ila tunachofanya sasa hivi ni kupunguza makali ya mgao wa umeme kwa kubuni vyanzo vingine vya uzalishaji umeme"- Dr Dotto Biteko naibu waziri mkuu na wazir wa nishati.
 
Back
Top Bottom