Ni wajibu wa TANESCO kutoa fidia pale Tatizo la Umeme linaposababisha hasara, umewahi kudai fidia hiyo?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu kwema?

Kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, mteja ukipata hasara kutokana tatizo la umeme, TANESCO inatakiwa kumfidia mteja huyo. Kipengele hiki kinasema;

"Kuwafidia wateja pale ambapo tatizo la umeme limesababisha uharibifu wa mali baada ya kuwa imehakikishwa kwamba tatizo hilo halikusababishwa kwa hali yoyote na mtumiaji wa umeme."

Screenshot 2024-02-12 083937.png

Mara ngapi umewahi kupata hasara kutokana na tatizo la umeme? Umewahi kudai fidia kutoka na hilo? Au ndio tunamuachia Mungu?

CC TANESCO
 
Nyumba yangu Ina mita za Luku nne tangu uanze utaratibu wa kulipia kodi Kila mwezi nimenda na kuandika barua mara kumi ikatwe moja na mpaka leo hawajaja kuhakiki.
Mi rushwa sitatoa na siku ya siku fedha za ziada zitarudi
TANESCO UBUNGO
Hili la kuomba kodi ikatwe kwenye mita moja tu linatakiwa lifanyike TANESCO au TRA?
 
Tanesco ndo wanakusanya hizo hela, na hata kama tra ndo wenye wajibu tanesco na wenyewe wanawajibu wakuandaa taarifa kuna moja mbili tatu kwwnye mita hizi, kama vile wanavokusanya hela na kuwapelekea tra
Hili la kuomba kodi ikatwe kwenye mita moja tu linatakiwa lifanyike TANESCO au TRA?
 
ni lazima na taratibu za kutoa fidia pale ambapo kunatokea matatizo ya umeme ambayo yanaweza kusababisha hasara kwa wateja. Hii inaweza kujumuisha matukio kama vile kutokuwa na umeme kwa muda mrefu au uharibifu wa vifaa kutokana na matatizo ya umeme.

Ili kudai fidia, mara nyingi unapaswa kuwasiliana na huduma kwa wateja kwenye kampuni ya umeme na kuwasilisha madai yako. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuhitaji kuwasilisha ushahidi wa hasara au uharibifu unaosababishwa na tatizo la umeme.
 
Kwa umeme upi wa kufanya uharibifu??
Shirika limejichokea km chama cha mapinduzi
 
Wakuu kwema?

Kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, mteja ukipata hasara kutokana tatizo la umeme, TANESCO inatakiwa kumfidia mteja huyo. Kipengele hiki kinasema;

"Kuwafidia wateja pale ambapo tatizo la umeme limesababisha uharibifu wa mali baada ya kuwa imehakikishwa kwamba tatizo hilo halikusababishwa kwa hali yoyote na mtumiaji wa umeme."

Mara ngapi umewahi kupata hasara kutokana na tatizo la umeme? Umewahi kudai fidia kutoka na hilo? Au ndio tunamuachia Mungu?

CC TANESCO
Yawezekana kuwa watu hawajui pamoja na wewe mleta thread kuwa wapo wateja wa TANESCO waliolipwa fidia kutokana na tatizo la umeme lililosababisha na uharibifu wa mali katika hali ambayo mtumiaji hakuhusika.

Nadhani, disputes nyingi kati ya mteja na TANESCO humalizwa na EWURA baada ya uchunguzi wa kina kufanyika; lakini kama tatizo litakuwa upande wa mteja sidhani kama kuna fidia yoyote itakayotolewa hata kama source itakuwa ni umeme, nadhani kipengele g kinahusika pamoja na sababu nyingine.
 
Vigumu sana kupata fidia. Je nyumba yako iliwekewa umeme na fundi wa umeme aliyesajiriwa kufanya kazi hiyo? Je unayo ramani ya njia zote za umeme katika nyumba yako na ambayo ilipitishwa na wataalam wa mambo ya umeme? Je ulisajiri idadi na aina ya vifaa ambavyo ungetumia katika hiyo nyumba yako?. Kama unavyo vithibitisho vyote na vingine vingi ambavyo havikuandikwa hapo juu basi anza safari ya kudai fidia ya hiyo hasara na Mungu akusaidie ufike salama.
 
Back
Top Bottom