TANESCO Shinyanga tendeni haki kwenye mgao wa umeme

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,296
3,967
Najua hali ya umeme nchini kwa sasa ni janga kubwa na wengine tunaofuatilia siasa za nchi hii,hatuna matumaini tena iwapo hali itarudi kama kipindi cha Magufuli.

Kwani ni JK na wanasiasa machawa wa enzi hizo akina Zitto walitudanganya kuwa baada ya bomba la Mtwara tutasahau habari za mgao wa umeme

Hawa wa sasa wanaahidi vile vile eti baada ya umeme wa bwawa la mwalimu Nyerere,hakutakuwa na mgawo wa umeme.Mimi siamini wanasiasa wa hii nchi.

Hata hivyo,hapa Shinyanga kuna mgawo unaopendelea maeneo.

Yapo maeneo mgawo ni zaidi ya saa 14 na yapo maeneo kila baada ya siku moja mgawo masaa mengi zaidi ya 8-10.

Wakati huo kuna maeneo umeme haukatiki hovyo hovyo.Majirani zetu hao wanatupa pole tu kwa kuwa mtaa wetu ndio unakatiwa umeme sana.

Naombeni huu mgawo wote tuonje machungu.Hii mbinu mnayotumia wa divide and rule siyo nzuri.Maana kuna wengine hawajui kama kuna mgawo kabisa nchi hii.

Tafadhali sisi sote tunalipa kodi sawa
 
Back
Top Bottom