"Mahitaji ya umeme nchini ni kati ya megawati 300 mpaka 400, mfano leo asubuhi tulikuwa na mahitaji ya megawati 304 ukiingiza megawati 235 (Kutoka kwenye mtambo wa bwawa la Mwalimu Nyerere) utaona kwa kiasi gani itapunguza uhaba wa umeme, zaidi ya asilimia 80 ya tatizo litapunguzwa kwa kuwasha tu ule mtambo ambao taratibu zake ziko mwishoni kabisa , unaweza ukajikuta kesho au keshokutwa unaamka asubuhi unashangaa mgao wa umeme haupo," - Eng Mramba, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati