Kuna raia wana roho mbaya aisee.
Gharama zote tangu mama huyo anaondoka ugweno kwa Gari ya kukodi hadi dar ni mimi. Sasa wanataka kunipangia maisha yangu?Niliyoyafanya yote hayana maana? Kumbe ningemkataa from day one angekua ameshajifia siku nyingi tumezika. Nina hasira sana kwa kweli Kwanza naona nikawatimue wote sitaki mtu kwanguHivi hii ni haki kweli? Familia imejaa wanaume kwa wanawake lakini wanashindwa kutibu mama yao?
Najua cha kufanya ngoja
Jumamosi nimewatamkia wazi ndani kwamba siwezi tena, mgonjwa anatakiwa achujwe damu kwa mashine maalum kila siku kadhaa, burhan wametaka vipimo upya kwa gharama zingine tena bado madawa na kadhalika.
Nilikua na ka akiba kangu benki sasa kamepungua kwa kiwango ambacho ni alarming na shule zinafunguliwa mwazo wa July, kwetu kijijini mzee wangu anaishi na dawa za pressure kila siku lazima ziwepo nanunua pakti nzima 32,0000 kila mwezi, yaani muda si mrefu naweza ku run mad, sio kwamba sina hela kwenye akaunti ila sasa ndo tunatumia akiba hivyo ambayo hutusaidia kwa msingi sana kama ada uendeshaji wa nyumba.
Kuchujwa damu kwny mashine maalum (Dialysis) ni gharama mno almost 2.8m per week, nakushauri kaa na wakwe mkafungulie mama mkwe Bima ya afya ya NHIF kidogo gharama zitashuka sana it only cost you 80K per month n hope utaweza kuafford
@navun-govind
Nnachokiona hapa ni ubahili wako tu.
Malalamiko yako yanaishia na mahesabu ya pesa tu, hakuna zaidi.
Sijuwi huyu hizo pesa ulikuwa una "save" za nini? kama hizo pesa ulizo save haziwezi kusaidia wakati wa shida kama hii ya mama mkwe wako unataka uziweke zisaidie ukisha kufa? Fikiri.
Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
Wacha masimangu ndugu pesa zipi hizo unazoongelea wewe milion 3 unaweza fananisha na uhai wa mtu achilia mbali mama aliyekuzalia mke?
Kama unauwezo fanya kadiri ya uwezo wako na bila kulalama iko siku hata wewe utakuja hitaji msaada wa namna yeyote kutoka kwa wanafamilia hiyo...
Tuko tofauti sana mimi na familia ya ukweni kwangu wamekuwa kama ndugu zangu tulozaliwa nao tatizo likiwa juu ya uwezo wangu tutakaa tudiscuss tujue tutafanyaje...si kulalama na vi milion 3..