Binti; Sio lazima mama mkwe akupende

Binti; Sio lazima mama mkwe akupende

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
38,410
Reaction score
88,944
BINTI; SIO LAZIMA MAMA MKWE AKUPENDE.

anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wakati nampeleka Mchumba wangu nyumbani kwa mara ya kwanza. Tukiwa Dodoma nilimwona akiwa katika hali ya hofu na wasiwasi.

Alikuwa ni binti mdogo, ndio kwanza chuo mwaka wa pili, hukuwahi kupelekwa ukweni.
Nimdodosa anajihisi vipi, nini kinaendelea kwenye akili yake. Vipi uzoefu wake huo mpya anaoenda kukutana nao.

Mchumba wangu, na hapa ni Binti Kimoso(mtoto wa kimaro), akaniambia kiukweli anahofu. Hajui wazazi na ndugu zangu watamchukuliaje. Hasa Mama Mkwe ambaye ni Mama yangu.

Nikamwambia asiwe na wasiwasi. Lakini nilifurahia kumwona akiwa katika hali ile. Nami niliitumia kumtania. Basi tukawa tunacheka. Dodoma tulikaa siku mbili hivi. Kisha tukaondoka mchana na kwenda kulala Arusha. Ili Asubuhi twende Moshi, huko ndiko wazazi wangu walikuwepo kwa wakati huo.

Basi usiku mchumba alikuwa akihangaika kuchagua ni nguo gani avae. Anatoa hii anarudisha na kuchukua ile. Aiseeh huwezi amini binti alipoteza zaidi ya masaa kuchagua nguo. Mimi nikijifanya naendelea na mambo mengine.

Hatimaye Binti Kimoso akaniambia, sijui niende na nguo ipi. Nikakwambia nguo zote hizo huoni ya kwenda nayo. Akaniambia haoni.

Nikamchagulia suruali nyeusi na blauzi. Nikamwambia utavaa hii hapa. Weee kamzozo kakaanza.
Oooh! Hapana Baby siwezi kwenda ukweni hivi. Hata kwa wazazi wangu sivaagi hivi. Oooh! Wewe unataka Wakwe wanione Mhuni.

Nikamwambia wewe kama mhuni mhuni tuu. Wewe vaa hizi kesho Twende.
Akasema hapana.
Basi akawa anahangaika wee. Akaniuliza tena akiwa ameboeka. Nivae nguo gani, nikamtolea suruali nyingine. Akaniambia alishakataa kuvaa suruali mbele ya Wakwe. Nikamuambia basi asiniulize ulize na kunisumbua.
Akaninunia. Basi kazi kuchambua na kupangua nguo kwa hasira sura imenuna. Huku mara mojamoja akinikata jicho la hasira.😅😅 Nilivyo mchokozi mambo yakawa burudani.

Akaghairi! Akasema ataangalia kesho asubuhi. Tukiwa tunasubiri usingizi. Akaniuliza, vipi wazazi na ndugu zako wasiponipenda au kunikubali?

Nikamwambia kwetu hatunaga kawaida ya kuchagulia vijana au mabinti wenza wao. Uchaguzi utafundishwa kwa miaka nenda rudi tangu ukiwa mdogo, mafundisho ya nyumbani na kanisani. Ukifika wakati wa kuoa au kuolewa hata ukisema uolewe na mvuta bangi, au muuaji ni wewe tuu..

Akaniuliza, vipi ikawa mara ya kwanza ikatokea kwako. Nikamwambia, Mimi sio mtu wa kuruhusu mtu yeyote kuvuka mipaka yake.

Nikamwambia kama itatokea Wazazi au ndugu au jamaa au rafiki zangu hawakupendi au hawakutaki wewe usiwajali. Wala hilo lisiwe kwako ni tatizo.

Nikamwambia, tukifika, fanya vile unavyotakiwa kufanya. Baki kwenye laini yako, mipaka yako. Usifanye chochote ili kutaka kupendwa, au rehema, sijui kujipendekeza au ili uonekane mwema.
Hilo kwangu nitalihesabu kama kosa na sitalivumilia.

Ukichoka kazi, acha. Sema umechoka.
Sijui nani anakuongelesha vibaya vibaya bila kujali na anavuka mipaka, usimkalie kimya.
Mwambie bila kusita huku ukilinda heshima yako na yake. Mwambie unamheshimu lakini heshima hiyo isimfanye avuke mipaka.

Nilimwambia iwe ni Mama au Baba au Bibi yangu, au ndugu zangu wakike na wakiume wanajua Mimi mtoto na ndugu yao ni mtu wa aina gani. So chochote atakacho wajibu kifanane na mimi.

Nikamwambia Mtibeli ni muungwana, mpole na anabusara lakini sio zoba. Pia havumilii kukosewa heshima tena kimakusudi.

Kesho yake tuliamka. Akavaa gauni lake safi. Safari kwenda ukweni ikaanza. Tukiwa Boma ng'ombe nikamwambia unajua sijawapa taarifa wazazi wangu kwamba tunaenda? Akawa anashangaa. Huku akiniuliza kwa nini. Nikamwambia jibu Lake nitampa wakati tumefika.

Tulipofika, tuliwakuta wazazi wanakula chakula cha mchana. Ilikuwa ugali na mnavu na samaki fulani wadogo wakulumangia. Kwa wakazi wa moshi wanaelewa.
Alikuwepo Bibi yangu(Marehemu sasa), Mama na ndugu zangu. Walishtuka kuniona. Tena nikiwa na mgeni. Binti waliyekuwa wanamjua kupitia mitandao.

Walikuwa na hofu na fedheha fulani hivi. Huku wakiniangalia kwa macho ya kunilaumu. Kwa nini sikuwapa taarifa.

Sasa sehemu ya kulala mgeni hawakuiandaa.
Chakula hakikuandaliwa.
Yaani mambo yalikuwa varuvaru. Sasa walikuwa wanahaha na kuhangaika.

Nikawambia wasifanye hivyo. Mimi pale ni nyumbani. Na niliyemleta patakuwa pia nyumbani kwao.

Binti akapokelewa, akaambiwa akaoge. Wakati yupo bafuni naanza kusutwa kwa kilugha(kipare). Nimefanya nini?
Mbona nimefanyia ukatili kiasi hiko?
Kwa nini sikuwapa taarifa, ona aibu sasa.

Nikawauliza aibu gani? Uhalisia wa maisha sio aibu. Nikawaambia mlitaka mjiandae? Huku nikiwacheka. Bahati nzuri haiwapi shida coz mimi ni mtoto wao wenyewe, wamenizaa na kunilea wao wenyewe. Hivyo wananijua kwa kiasi kikubwa.

Nakumbuka Bibi yangu kipenzi akaniambia, huyu binti mzuri hivi umemleta kwenye mazingira haya, unahakika atarudi. Unahakika Robert? Aliniambia kwa kipare, huku akinitazama na macho yake ya Kizee yenye mzani wa mwanamke mwenye uzoefu na aliyeona mapito na mahusiano mengi katika maisha yake.
Nakumbuka mpaka leo jinsi alivyokuwa akinitazama Bibi yangu. Sasa alitegemea jibu langu. Huku wengine nao wakiniangalia.

Nikamwambia, Mimi ni Robert, siwezi kufanya jambo kubwa kama hili bila kulipima na bila kujiridhisha. Hata hivyo Mungu ndiye anayejua kwa nini amenileta pamoja naye binti huyu mzuri. Ikitokea binti huyu hatarudi basi nitajua hakuwa sahihi. Na Mungu atanipa binti mzuri zaidi kuliko huyu aliyesahihi.
Hata hivyo, nilimshirikisha yeye(Mungu) so huyu binti atakuwa wakwanza na wamwisho kutambulishwa na mimi. Kumaanisha sitakuja mbele yenu na binti mwingine. Na Mungu ndiye atakaye tuongoza.

Baada ya mimi kujibu hivyo. Walinielewa. Walijua kwa sababu wanajua nilikuwa na mahusiano kiasi gani na mhusika aitwaye Mungu. Hata kama sikuwa mkamilifu.

Binti Kimoso alikuwa amemaliza kuoga. Sasa itabidi chakula kingine kipikwe. Bahati ilioje Gesi ilikuwa imeisha. Hatari nakwambia. Hivyo iliwapasa wapikie Kuni huko nje.
Binti Kimoso akaenda kumsaidia Mama kupika chakula mimi nikabaki na Bibi.

Bibi na ndugu zangu, Bibi akaendelea, ulimtumia Mama yako pesa? Akaniuliza.
Nikamjibu sikumtumia.
Akainamisha kichwa chini.
Alafu kwa kitambo akainua uso. Akaniangalia; Robert hivi unaakili kweli. Aliniuliza. Lakini tulikuwa tunazungumza Kwa sauti ya chini ili huko nje wasisikie😄😆 yaani ilikuwa inafurahisha sana kwa upande wangu.

Bibi yangu ni mstaafu. Akatoa elfu hamsini huku akinitaka kunipa huku akiangalia huku na huku kama hataki atakayeingia aone. Nikamuuliza ya nini?
Akatabasamu. Niliona akinionea huruma ukizingatia mimi ni mjukuu wake pendwa.
Akaniambia wewe chukua. Nikamkatalia. Nikamwambia sijakuambia kwamba sina hela. Unataka nijitutumue? Tukacheka.

Chakula kiliiva. Ni ugali tena. Lakini haukuwa na mnavu. Bali ugali, maziwa mgando na visamaki. Tulikula mimi na mchumba wangu. Tulifurahia sana..
Kufurahia chakula hakuangalii aina ya chakula bali mahusiano ya watu.

Hekaheka za kuandaa sehemu ya kulala ziliendelea. Sisi tukiendelea kula. Alafu mara mojamoja nikirusha maneno ya uchokozi. Pande zote mbili.

Kwa wazazi na binti. Leo kazi ipo.
Maana kila mmoja anataka kujionyesha yeye ni mzuri. Binti anataka kuonekana ndiye wife materials, wazazi nao wanajitutumua kuonyesha wao ni wakarimu na familia iliyonjema.

Niliwaambia sikilizeni. Hakuna haja ya kufanya mambo yawe mengi. Tuishi kama tunavyoishi siku zote. Ikiwezekana kama tulijuana miaka elfu iliyopita.

Tulilala. Baada ya siku mbili.
Nikawaambia sasa tunaweza kupika kile chakula ambacho mngepika siku ya kwanza.
Tulinunua mboga ambaye alikuwa jogoo mkubwa, nyama, tukapika chakula kizuri na vinywaji.
Tulifurahia lakini haikuwa kama siku ya kwanza. Kwa sababu chakula ni chakula. Utamu ni mahusiano mazuri, moyo wenye furaha, na mtazamo chanya. Bila presha wala shinikizo.

Niliwaambia, Mtibeli hakarimiwi, hafurahishwi na mapokezi bandia, chakula sijui mapambo sio sehemu ya mambo yanayonifanya nione nimeheshimiwa au ukarimu.
Heshima, ukarimu, wema, uzuri hauhitaji maandalizi.

Tuliondoka. Wote tukiwa tumefurahia. Binti Kimoso ni moja ya matukio ambayo hatayasahau katika maisha yake. Alipokelewa vizuri.
Kwa heshima na aliishi kwa uhalisia wake kwa sababu niliusema, na kila alilojaribu kulifanya ili kutaka kuonekana anaheshima nililizuia. Huku nikisema mbele ya wazazi wangu.
Maisha ya familia hayahitaji ku-fake. Hayahitaji uongo.

Nataka kusema nini kuhusu kisa na Visa vyangu ambavyo kimsingi ni vyakweli kabisa.

Kijana, maisha hayahitaji kutumia nguvu ili uwe na furaha.

Usitumie nguvu ili upendwe au uheshimike. Hiyo sio heshima. Huo ni utumwa.

Kwa vijana, kupata mwanamke mzuri anayekupenda hakuhitaji uwe na pesa na utumie nguvu. Hakuna kitu kama hicho. Mtu kama hakupendi huwezi mfanya akupende.
Ishi maisha yako. Uhalisia wa maisha yako sio aibu, sio fedheha. Majaliwa yako sio aibu. Jikubali.

Binti kama mkwe hakukubali usimlazimishe. Mapenzi ni hiyari. Kumheshimu ni wajibu wako.

Wanawake wanapenda maisha mazuri. Lakini usijefikiri kuna mwanamke atakupenda kutoka moyoni kisa unamaisha mazuri. Nope! Atakutumia tuu. Then utakuja kulia kwamba wanawake hawaridhiki.
Artificial thing yaani vitu vilivyoundwa na mwanadamu haviwezi kumridhisha mtu. Kama vina expire date na kupitwa na wakati why ujiulize kwamba hard hiki?

Zaidi, unatakiwa uishi kwa kutambua ukweli na uhalisia kwa sababu hivyo ndivyo vitakuweka kwenye mipaka yako.
Mtu kuamua kuishi na wewe ni hiyari yake. Lazima uheshimu hilo. Lakini pia siku akiamua kuondoka kwenye maisha yako ni hiyari ileile aliyoitumia kuishi na wewe. Heshimu na baki kwenye mipaka yako.

Kuumia kwa kuachwa ni Dalili ya kukosa shukrani na ubinafsi uliopitiliza. Labda ulie kwa mazoea, na pia ulie jinsi mtu huyo mlivyoishi vizuri na alivyobadili maisha yako na kuyafanya yawe ya furaha.
Na sio ulie kwa kuumizwa kwamba umeachwa na unataka abaki tena kwa kumlaumu.

Mara nyingi wanaolia hivi wanaukatili na hawakufanya wajibu wao.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Umesema ukweli mtupu maisha ya kuigiza hayawezi kukupa watu real
 
Wenye mama wakwe zenu, mnaitwa huku, kuna ujumbe wenu.
😂😂😂
 
Huzi mrefu sana kama gazeti la mwananchi, aliyeelewa anieleweshe.
 
Back
Top Bottom