Hivi Ugonjwa wa mama mkwe unanihusu kweli?

Hivi Ugonjwa wa mama mkwe unanihusu kweli?

1. Pole sana. . . . . Lakini mkeo anajua uwezo wako sidhani kama anafanya asilolijua au mzee ulijivika u boss de boss siku ulipoenda kuoa??!!

2. Mkweo anakuhusu kabisa ila badala ya kususa waite shemeji zako wa kiume hao ndio mnaweza kuongea mkaelewana sababu na wao wana familia na koromeo kama wewe "perspective" ya kiume mtaelewana fasta.

3. Wageni kama wengi timua kweli kama ni kuuguza watatokea makwao kwanza si kalazwa wao wanafanya nini kwako, wabaki wawili wanaolala hospitali wengine pyeeee kwao

4. Endelea kuchangia kwa uwezo wako bila kuathiri zaid maslahi ya wanao ila kamwe usimsuse mama wa mke wako

Lastly; Kuwa mume mwema na baba wa familia sio favour kwa mkeo ni wajibu wako

Kuna tym hua nikisoma post zako zinanichukiza napita kimya kimya.. ila hili leo naomba nikupe LIKE laki nane!!!
 
Kidogo sasa!yaani huyo ni wakuachwa hivyohivyo halafu uone kama ndugu hawatamtibu!yaani huyo mke anataka aonekane yeye ndiye ameolewa na tajiri mwenye huruma na anapendwa sana!
Dawa ni hiyo tu,ukiwa mpole sana nayenyewe ni mbaya,bora kuwa bandidu tu

Huyo mwanamke anamkomoa kwanza hao ndugu zake walishauri amwache yeye sasa akuna upendo zaidi kumkomoa yani mama yao mzazi wamwachie mtu mmoja michango yote na bado adi gharama za familia ni yeye alafu ndugu wanakaa tu kuangalia hili hali jamaa ajawahi kumtibu mzazi wake yoyote Kwa ela hiyo alafu awazi ata kuna watoto wataishaye badae sometimes mtu unaweza kujuta Kwa mini nilioa na kuwa na familia unaona bora ungeishi single tu
 
Kwanza nakupongeza kwa msaada ambao umeshautoa hadi sasa, umefanya jambo la maana sana kusaidia kuokoa maisha ya mama mkwe wako, kwa kweli una moyo wa kipekee kabisa. Ngoja niwaulize wale wanaokushambulia, kwani hivi kuoa kwenye familia flani ni kwamba umeoa familia nzima? Madhalani huyu bwana naye angekua hana hata hiyo kumi ya matibabu je wangefanyaje? Kwanza kukaa hapo kwako na kupata huduma zote huo ni msaada tosha. Wao ilipaswa wachukue jukumu la kuhakikisha mzazi wao anapata matibabu na sio mzigo wote wanakuvisha wewe. hata kama una pesa nyingi lakini si kwamba hazina matumizi. Watoto wako wanakuhitaji sana kuliko yeyote yule. Tuchukulie mfano mdogo tu leo imetokea huna uwezo je hao ndugu watawasomesha watoto wako, si ndio hao ambao watabaki kuwasimanga. Cha muhimu kwa sasa ni familia yako kwanza hao wengine ni ziada tu. Washauri ndugu waitane viako, wajichange kwa ajili ya kuhudumia mgonjwa, sio zigo lote ulibebe wewe eti kisa umeoa. Umeshatoa msaada halafu bado watakuona una roho mbaya washasahau pesa kibao ushaitumia kwa ajili ya mgonjwa. hata kama tenda wema nenda zako lakini mengine ni maudhi sana. Ndoa isiwe adhabu kwako. Hao wanao kushambulia hapa utafikiri wao ni wema , lakini ni kwa vile tu hayajawakuata, ngoja yawakute utaona kulalamika kila mahali. Maisha ya kiafrika yanajulika kabisa kwamba ni kusaidia, lakini na wewe unayesaidiwa mpe nguvu anayesaidia "ukishikwa shikamana" Pole sana mkuu
 
Salaam zenu wakuu,

Mambo ya ndoa ni mengi mno kwa kweli ukiamua kuwa mtoto mtiifu kwa mke ni tabu ukisema uendelee na uzinzi bado ndoa haiwi na amani, sasa sijui mtu ufanyeje. Ni kama mwezi umepita nimeamua kuacha dhambi zote zilizokua zikimkasirisha Mungu na mke wangu, for the past one month kama sikosei nimekua nikirudi saa moja kamili home, sijagusa pombe wiki ya tatu sasa, wakianza mapambio yao usiku nami nipo ingawa nakua kimya tu.

Sasa pamoja na kuonesha tabia nzuri kiasi hiki nikiamini ndoa itatulia kumbe wapi, mama mkwe wangu kaja wiki mbili zilizopita kwa ajili ya matibabu, kwa kweli ana hali mbaya alipewa rufaa kuja muhimbili, tatizo kubwa ni gharama za matibabu ambazo zipo juu mno, alipofika tu alifanyiwa vipimo mbali mbali katika hospital ya Agakhan baada ya huduma na vipimo kusuasua sana wakati mwingine wakwambie kipimo flani kimeharibika hivyo akahamishiwa Agakhan .

Wakati wanamwamishia agakhana mm nilidhani wana uwezo wa kulipia gharama kumbe hawana, Agakhan huwa wanataka deposit ya one million kabla ya admission, wife akanigeukia mimi nilipe hiyo hela, sikua nayo wakati huo nikaenda town kutoa kwenye akaunti yangu huku nikiugulia moyoni. Baada ya wiki wakamtoa, wamemwamishia burhani hospital ambayo bei zake si kama agakhan lakini bado zipo juu. Hadi anatoka Agakhan nimeshatumia 3.2 million

Jumamosi nimewatamkia wazi ndani kwamba siwezi tena, mgonjwa anatakiwa achujwe damu kwa mashine maalum kila siku kadhaa, burhan wametaka vipimo upya kwa gharama zingine tena bado madawa na kadhalika. Nilikua na ka akiba kangu benki sasa kamepungua kwa kiwango ambacho ni alarming na shule zinafunguliwa mwazo wa July, kwetu kijijini mzee wangu anaishi na dawa za pressure kila siku lazima ziwepo nanunua pakti nzima 32,0000 kila mwezi, yaani muda si mrefu naweza ku run mad, sio kwamba sina hela kwenye akaunti ila sasa ndo tunatumia akiba hivyo ambayo hutusaidia kwa msingi sana kama ada uendeshaji wa nyumba.

Na bahati mbaya insurance kazini inatuhusu, mm, make na watoto tu, tangu Jumamosi nilipotoa tamko la kutoendelea na hizo gharama nyumba imegeuka kosovo, wanandugu wa wife wamekusanyika hapo nazungumzwa vibaya asubuhi hadi jioni mimi na mwenzangu hatuzungumzishani tunapishana tu ameninunia. Maajabu ni kwamba mwezi wa nne nadhani, tulipokua na matatizo na wife yaliyosababishwa na mimi hao hao ndugu walimshauri aachane na mimi kwamba miim ni mzinzi sasa Leo mama yao angetibiwa na nani hadi kufika hapo?

Gharama zote tangu mama huyo anaondoka ugweno kwa Gari ya kukodi hadi dar ni mimi. Sasa wanataka kunipangia maisha yangu?Niliyoyafanya yote hayana maana? Kumbe ningemkataa from day one angekua ameshajifia siku nyingi tumezika. Nina hasira sana kwa kweli Kwanza naona nikawatimue wote sitaki mtu kwanguHivi hii ni haki kweli? Familia imejaa wanaume kwa wanawake lakini wanashindwa kutibu mama yao?

Najua cha kufanya ngoja

Kununiana sio suluhisho, mimi ningekuwa kwenye nafasi yako kwanza ningekaa na huyo mke wangu nimweleze hali halisi na kumkumbusha majukumu yetu mengine kama wanafamilia (maana anajifanya amesahau ) baada ya hapo ni kuongea na ndugu wa mke juu ya gharama za hospitali kimsingi ningewaambia wanipokee kijiti kwa maana ngwe yangu imeisha (kwa lugha ya kiungwana) ingawaje bado ningeendelea kufanya pale inapobidi sio kama nitakua nimewabwagia.. na hao ndugu kila mtu atudi tu kwao maana anayeumwa sio mke wangu na mgonjwa yuko hospitali.

Kimsingi me naona uko sahihi ulipokosea ni hapo pa kununiana na mkeo tu.
 
kuna mambo mengine nikiyafikiria hata swala la kuoa sitaki kulisikia ....maana kwa sasa naishi kwa raha zangu hata ndugu zangu ambao kiuwezo wako chini nasaidia bila shida...ila najua ningekua nimeoa nikapata mwanamke wa type kama hiyo kwa sasa ningekua kama mti kwa kukonda ...mungu anisaidie tu nije kumpata aliye na tabia nzuri

mkuu nakubaliana na maneno yako asilimia 100. Ndoa nyingi ni zuga tu kuwa wanapendana lakini ukweli ni majanga tupu. Nilishajipanga kabisa kuoa, lakini nilighairi dakika za mwisho baada ya kugundua kuwa kama nataka kupunguza siku za kuishi basi nioe huyu mwanamke. Maana ni pasua kichwa, unaweza kuwa kichaa. Lakini kuishi alone bana ni raha sana aisee. Bado nipo sanaaa
 
Hapa umeongea ukweli mpana nilimshauri dogo wangu mmoja ajifikirie mara mbili kama anataka kumuoa girlfriend aliyenaye maana mama yake mzazi anamtegemea na watoto wa mama yake mdogo analipa yeye ada demu wakati hana kazi ya maana anaungaunga tu, ukimwi kamwe hatutaweza kuudhibiti wa umaskini uliokithiri na nikionaga hivi ndio sababu za kuichukia CCM zinaongezeka wamezinajisi huduma za afya bure na elimu bure kwa wote

Hicho kisiwe kigezo mkuu, kama wanapendana amuoe, mradi mwanamke aelewe nafasi yake na ajue huyo ni mume sio mwokozi wala ATM, aelewe bado anawajibika kwa familia yake kwa kiwango kile kile cha mwanzo..

Ingawa mwanaume ana wajibu wa kumsaidia mpenzi wake lakini isiwe sheria ya kujilemaza na kusubiri kupewa tuuu..

Mwisho, mwanamke mwenye majukumu na asiye na majukumu (namaanisha yaliyozidi mana hakuna alokosa majukumu ) wote wana haki ya kupendwa na kuolewa.
 
Mwambie mkeo umeishiwa hela acha kusikitika tu. Be a man. Umeoa mke sio mkwe. Toa msaada kwa kadri ya uwezo wako na katu hilo sio jukumu lako. Period.
 
Wacha masimangu ndugu pesa zipi hizo unazoongelea wewe milion 3 unaweza fananisha na uhai wa mtu achilia mbali mama aliyekuzalia mke?
Kama unauwezo fanya kadiri ya uwezo wako na bila kulalama iko siku hata wewe utakuja hitaji msaada wa namna yeyote kutoka kwa wanafamilia hiyo...
Tuko tofauti sana mimi na familia ya ukweni kwangu wamekuwa kama ndugu zangu tulozaliwa nao tatizo likiwa juu ya uwezo wangu tutakaa tudiscuss tujue tutafanyaje...si kulalama na vi milion 3..

Ndugu 3m. co ndogo ni msaada ambao uko ndani ya uwezo wake na yeye mpaka kuja hapa kuomba ushauri sio jambo dogo kaona linaanza kumshinda,kwa hivyo tumshauri vyema sio kuanza kumsimanga na kumbuka kila mtu ana maisha tofauti na mwenzake aidha ni wewe au mimi.
 
Wanawake mchague waume zenu kwa makini.... la sivyo yatawakuta kama yanayomkuta mke wa mleta uzi....


Anyway.... ulishakaa na ndugu za mkeo kuzungumzia hilo?
Kwa nini msipitishe mchango utakaojumuisha ndugu wa mkeo? Au wote hawana uwezo/ moyo wa utoaji????

Mshazungumza nao kuhusu gharama za kuuguza? Maana yake sometimes unaweza kuwa na mgonjwa halafu wanaokuja kumtembelea wakawa wengi na gharama kuwahudumia kuliko mgonjwa na hapo wanakuja mikono mitupu
 
POLE SANA!kuna familia zingine ni mtihani tupu!sasa wameshakugeuza wewe ATM machine,mimi nawaza kama wewe na ningefanya ulivyofanya tu!
Wacha watibu ndugu yao na wewe mtibu baba yako hayo mengine achana nayo!utaishi kinafiki mpaka lini bwana?!kama hawataki kumtibu ndugu yao basi wacha afe!
Mimi nilivyosikia kaoa UGWENO basi nampa pole sana maana hilo GUBU lake ataikimbia nyumba tu
  • Gharama zote tangu mama huyo anaondoka ugweno kwa Gari ya kukodi hadi dar ni mimi.
  • Kumbe ningemkataa from day one angekua ameshajifia siku nyingi tumezika.
  • Kwanza naona nikawatimue wote sitaki mtu kwangu
  • Familia imejaa wanaume kwa wanawake lakini wanashindwa kutibu mama yao?
Najua cha kufanya ngoja
navin-govind pole jamaa yangu km na ww si mpare ndio tatizo lake tafuta wa Usangi akawakomalie
 
Duh ishakuwa taabu sasa una mpango gani na hiyo familia !.Ingekuwa mgonjwa ni Mama yako mzazi ungelalamika ?.

Wakati mwingine tujiulize,kama mtu ameisha gharamia zaidi ya 3ml na anaona wazi anaelemewa atafanyaje mchango wake kama haujaonekana na wife bado hajaridhika maelewano hakuna sababu kaishiwa hela za kumhudumia mama mkwe tell them the truth kuwa sina pesa nimeishiwa and then let nature ichukue nafasi yake,hakuna namna kwa nini mtu ugeuke chizi kwa mawazo wakati you have already tried na ukaishia njiani.?waamue wao watafanya nini maana wangekuwa waungwana wangekaa na kushauriana wanasaidiaje ili mama yao apone na wasimpe mtu mzigo mkubwa huo ndio uungwana.
 
Imezoeleka KUA wanaume ss NI KAMA ATM za wakwe zetu
 
suala la kuijifanya we ndio mfadhili wa familia wakati mko wengi ndio linaanziaga hapa.
tatizo linapowakuta kama wanafamilia inatakiwa mkae na kujadili mtalitatua vipi kwa kuchangishana.
yale mambo ya mmoja kujidai mi nna uwezo wakati anategemea kwingine ndio shida yake.

Sasa hivi anachojali yeye ni sifa ya kuonekana yeye ndiye kamuhudumia mgonjwa huku mtafutaji wake anateseka.
 
Ugweno? wapare hao! Wachungu kwa hela hao, mabahiri balaaa. Fanya maamuzi magumu, kama mgonjwa anakugharimu na wao wanakuja kukaa kwako tena kukuongezea mzigo mwingine. Timua hao watu then angalia jinsi ya kumsaidia huyo mgonjwa lakini kama ni wapare ni bahili hao hakuna.
 
Duh pole ongea na wife juu ya tatzo lako kuw hupendi tabia hyo na endapo itaendelea utawaondoa ndg zake hapo nyumbani ama ikishindikana utoke kwa mda uache umelpa karo za shule kila ktu kw watot then uwaache kw mda wa miez miwil bila pesa ama mawasilian ndo urudi.
 
1. Pole sana. . . . . Lakini mkeo anajua uwezo wako sidhani kama anafanya asilolijua au mzee ulijivika u boss de boss siku ulipoenda kuoa??!!

2. Mkweo anakuhusu kabisa ila badala ya kususa waite shemeji zako wa kiume hao ndio mnaweza kuongea mkaelewana sababu na wao wana familia na koromeo kama wewe "perspective" ya kiume mtaelewana fasta.

3. Wageni kama wengi timua kweli kama ni kuuguza watatokea makwao kwanza si kalazwa wao wanafanya nini kwako, wabaki wawili wanaolala hospitali wengine pyeeee kwao

4. Endelea kuchangia kwa uwezo wako bila kuathiri zaid maslahi ya wanao ila kamwe usimsuse mama wa mke wako

Lastly; Kuwa mume mwema na baba wa familia sio favour kwa mkeo ni wajibu wako

mkuu huenda jamaa alienda na nyundo yani hammer kipindi anaenda kutoa mahari
 
Bora ww mama mkwe anakutambuwa .mie mwezio girlfriend wangu alishawai kuniambia ujinga Kama huo .mengine na mfanyia lakin akisema habari za mama ake nafsi inakuwa mzito kufanya. Histoshe nahisi mama yake mchawi kwa sababu alicho niambia akihingi akilini
 
1. Pole sana. . . . . Lakini mkeo anajua uwezo wako sidhani kama anafanya asilolijua au mzee ulijivika u boss de boss siku ulipoenda kuoa??!!

2. Mkweo anakuhusu kabisa ila badala ya kususa waite shemeji zako wa kiume hao ndio mnaweza kuongea mkaelewana sababu na wao wana familia na koromeo kama wewe "perspective" ya kiume mtaelewana fasta.

3. Wageni kama wengi timua kweli kama ni kuuguza watatokea makwao kwanza si kalazwa wao wanafanya nini kwako, wabaki wawili wanaolala hospitali wengine pyeeee kwao

4. Endelea kuchangia kwa uwezo wako bila kuathiri zaid maslahi ya wanao ila kamwe usimsuse mama wa mke wako

Lastly; Kuwa mume mwema na baba wa familia sio favour kwa mkeo ni wajibu wako

Usimbebeshe migo usiokuwa wake kwa vile wewe haukuhusu.
 
Back
Top Bottom