Hivi Ugonjwa wa mama mkwe unanihusu kweli?

Hivi Ugonjwa wa mama mkwe unanihusu kweli?

Hadi dakika hii, ndugu wa mkewe wa kiume hawajielewi, wangekuwa wanajielewa kwenye hiyo mil 3 wangechangia hata robo. Na hiyo wote kushindwa kujiongeza na kurundikana kwa shemeji yao tu inaonyesha akili zao zikoje.

Hasa na mwenye nyumba kishaelemewa, inakuwaje? Mtu hachelewi 'kuhama' nyumba yake mwenyewe kwa muda....lazima hata wasiojielewa watajielewa...
 
Sasa ahangaike kugawanya kwa njia ndefu wakati njia fupi ipo. Awafukuze tu, hawana akili.

Hivi mzazi wao mgonjwa unashindwa kuchangia hata mia? Lazima kichwani ziwe haziko sawa.

Hasa na mwenye nyumba kishaelemewa, inakuwaje? Mtu hachelewi 'kuhama' nyumba yake mwenyewe kwa muda....lazima hata wasiojielewa watajielewa...
 
Huyo mkeo mwambie wazi, achague ndoa ama aende na nduguze. Sipendi watu wanaoshikiwa rimoti na ndugu zao.

Hata sisi wanawake nao tuna shida wakati mwingine...huchelewi kukuta yeye ndio mstari wa mbele kusema..hamna shida, atalipa tu... Hata kama uezo upo, si mbaya ndugu wakajipanga na wao, hasa huyo shemeji asingekuwepo ilikuwa wafanyeje?
 
Bab we maliza hzo pesa
Ukifulia huyo mkeo ndo wa kwanza kutoka nduki na hao ndugu zake watakucheka mpaka ufe
Muda mwingine wema huponza
Kama vp imetosha hzo gharama za kusafisha damu kwa pesa binafsi hutoweza na ndio maana tunashauriwa tujiunge na #MFUKO WA BIMA YA AFYA YA TAIFA# umuhimu wake ndo waonekana hapo.
 
Mama mkwe anakuhusu kabisa. Ingawa Sidhani kama ni busara ukoo mzima wa mama mkwe wako wakakutegemea wewe mtu mmoja. Hamna ndugu zake wenye uwezo ambao wanaweza kushare gharama na wew?. I can feel unavyoumia lakini pia inahitaji moyo sana Kumuacha mtu afe kwa kukosa matibabu while hela Ipo ndo maana unaona unaumia weee lakini hela bado unaitoa.

cha msingi ongea na mkeo, mwambie wewe hela zimekata kabisa. Wafanye utaratibu wa kuchangishana. Tuone kama na wao hawatotafuta hela kwa hali na Mali ili mama atibiwe. Kama watakuwa radhi ndugu yao afe basi ni sawa.

Hao ndo wanafanya vigezo vya ndoa viongezeke. Ndo maana kuna watu akishaona familia/ ukoo anaotaka kuoa kuna tegemezi wengi, anaghairi kwa kweli. Mke asigeuzwe kuwa mtaji wa wazazi wake
 
Tibu mkweo ila shirikisha mashemeji muone mtakavyosaidiana na uwaeleweshe situation yako kinagaubaga pamoja na swala la kuuguliwa na Baba yako. Ndugu wanaohang hang nyumbani, zungumza na mkeo waende kwa ndugu zao wengine walio Dar.
 
Hata sisi wanawake nao tuna shida wakati mwingine...huchelewi kukuta yeye ndio mstari wa mbele kusema..hamna shida, atalipa tu... Hata kama uezo upo, si mbaya ndugu wakajipanga na wao, hasa huyo shemeji asingekuwepo ilikuwa wafanyeje?

Ndio maana yake hapo!yaani ni aina fulani ya wanawake wapenda sifa na wasio na huruma kwa waume zao!yaani hapo yeye ndio anataka aonekane bora kwenye ukoo!stupid kabisa
 
Mama mkwe anakuhusu kabisa. Ingawa Sidhani kama ni busara ukoo mzima wa mama mkwe wako wakakutegemea wewe mtu mmoja. Hamna ndugu zake wenye uwezo ambao wanaweza kushare gharama na wew?. I can feel unavyoumia lakini pia inahitaji moyo sana Kumuacha mtu afe kwa kukosa matibabu while hela Ipo ndo maana unaona unaumia weee lakini hela bado unaitoa.

cha msingi ongea na mkeo, mwambie wewe hela zimekata kabisa. Wafanye utaratibu wa kuchangishana. Tuone kama na wao hawatotafuta hela kwa hali na Mali ili mama atibiwe. Kama watakuwa radhi ndugu yao afe basi ni sawa.

Hao ndo wanafanya vigezo vya ndoa viongezeke. Ndo maana kuna watu akishaona familia/ ukoo anaotaka kuoa kuna tegemezi wengi, anaghairi kwa kweli. Mke asigeuzwe kuwa mtaji wa wazazi wake

Hapa umeongea ukweli mpana nilimshauri dogo wangu mmoja ajifikirie mara mbili kama anataka kumuoa girlfriend aliyenaye maana mama yake mzazi anamtegemea na watoto wa mama yake mdogo analipa yeye ada demu wakati hana kazi ya maana anaungaunga tu, ukimwi kamwe hatutaweza kuudhibiti wa umaskini uliokithiri na nikionaga hivi ndio sababu za kuichukia CCM zinaongezeka wamezinajisi huduma za afya bure na elimu bure kwa wote
 
Dah! Kuna issue zingine unaweza hisi ni hadithi kumbe kweli.Mungu niepushie,pole san mkuu
 
Hao ndugu nao wangechangia Sio mzigo wote wako pekee, Mimi waniseme tu....
 
Huyo ni kama mama yako ila ongea na hao ndgu wa mkeo wajichange pia maisha magumu
 
Dah! Kuna issue zingine unaweza hisi ni hadithi kumbe kweli.Mungu niepushie,pole san mkuu

Hakuna hadithi hapo kuna wanawake ni washenzi sana bora uwe bachela hafadhari hata siku zako za kufa hazitokaribia.

Mimi mpaka leo bado nafanya utafiti ni kwa nini wachungaji wote na manabii na wanaojiiita mitume kwenye kutoa mapepo ni wanawake ndio watolewao mapepo? Kuna uhusiano au urafiki gani kati ya mapepo na wanawake?
 
kuna mambo mengine nikiyafikiria hata swala la kuoa sitaki kulisikia ....maana kwa sasa naishi kwa raha zangu hata ndugu zangu ambao kiuwezo wako chini nasaidia bila shida...ila najua ningekua nimeoa nikapata mwanamke wa type kama hiyo kwa sasa ningekua kama mti kwa kukonda ...mungu anisaidie tu nije kumpata aliye na tabia nzuri
 
Hapa umeongea ukweli mpana nilimshauri dogo wangu mmoja ajifikirie mara mbili kama anataka kumuoa girlfriend aliyenaye maana mama yake mzazi anamtegemea na watoto wa mama yake mdogo analipa yeye ada demu wakati hana kazi ya maana anaungaunga tu, ukimwi kamwe hatutaweza kuudhibiti wa umaskini uliokithiri na nikionaga hivi ndio sababu za kuichukia CCM zinaongezeka wamezinajisi huduma za afya bure na elimu bure kwa wote

Ingawa utegemezi kwa sisi waafrika ni kitu ambacho hakiepukiki, basi msiwe tegemezi hadi mumfilisi huyo mnayemtegemea. Sasa kwa hali kama hiyo, huyo kaka si atafilisika jamani kama sio kupata magonjwa ya moyo. Mmh tuwe na kiasi kwa Kila kitu
 
navin-govind

eeeee nimeishiwa na nguvu hapa akili yangu haifanyi kazi nimevaa viatu vyako hee hiyo ni hatariiiii
 
Last edited by a moderator:
Ingawa utegemezi kwa sisi waafrika ni kitu ambacho hakiepukiki, basi msiwe tegemezi hadi mumfilisi huyo mnayemtegemea. Sasa kwa hali kama hiyo, huyo kaka si atafilisika jamani kama sio kupata magonjwa ya moyo. Mmh tuwe na kiasi kwa Kila kitu

Mimi kwakweli nimeumbwa na aibu siwezi biashara ya utegemezi, shemeji yangu ameowa kwetu tukikutana namtowa out kwa gharama zangu siyo kisa shemeji basi unaganda kama sanamu ndio maana mtu mwingine kama hana pesa anaogopa hata kwenda kutembelea ukweni.

Mimi nashukuru mama yangu ameuguwa sana aliyecover bill zote ni mume wake, watoto kazi yetu ilikuwa ni bidii ya kwenda hospital na zamu ya kuandaa chakula tu basi, hakuna mtu aliyeowa kwetu aliyewahi kununuwa hata panadol.
 
Kaa ujadiliane na shemeji zako kama vipi wakauze hata mashamba/mifugo/mazao huko kijijini ili pesa ipatikane ikibidi abaki mmoja tu hapo maskani.

Hizi ni changamoto za kuoa kwenye familia ya kipato cha chini ni balaa tupu.
 
Pole sana kiongozi. Ni kweli man mkwe ni mama kama mama mzazi na ni muhimu kuonyesha kujali sana pindi kukiwa na shida upande wa ukweni, lakini wewe ni mshirikishwaji tu, sio mtoa maamuzi katika familia ya mke wako. Hivyo basi, mashemeji zako walitakiwa wakae na kuona ni vipi mama asaidiwe matibabu ili kila mtu atoe mchango wake, mama si wa mkeo tu bali wa wote wakiwemo hao ndugu wa mkeo, hivyo wote walitakiwa kishiriki katika matibabu na sio kukubebesha mzigo wote. Pole, kuna familia zipo hivyo bali kuwa mpole na tumia busara kuongea nao na kuwashirikisha wote katika matibabu ya mama.
 
Jumamosi nimewatamkia wazi ndani kwamba siwezi tena, mgonjwa anatakiwa achujwe damu kwa mashine maalum kila siku kadhaa, burhan wametaka vipimo upya kwa gharama zingine tena bado madawa na kadhalika.

Nilikua na ka akiba kangu benki sasa kamepungua kwa kiwango ambacho ni alarming na shule zinafunguliwa mwazo wa July, kwetu kijijini mzee wangu anaishi na dawa za pressure kila siku lazima ziwepo nanunua pakti nzima 32,0000 kila mwezi, yaani muda si mrefu naweza ku run mad, sio kwamba sina hela kwenye akaunti ila sasa ndo tunatumia akiba hivyo ambayo hutusaidia kwa msingi sana kama ada uendeshaji wa nyumba.

Kuchujwa damu kwny mashine maalum (Dialysis) ni gharama mno almost 2.8m per week, nakushauri kaa na wakwe mkafungulie mama mkwe Bima ya afya ya NHIF kidogo gharama zitashuka sana it only cost you 80K per month n hope utaweza kuafford

Back
Top Bottom