Kwanza hongera kwa swali hili, pili jf ya sasa imebadilika sana, mtu unatoa hoja, badala ya watu kujibu hoja kwa hoja au kwa hoja mbadala, watu wanajibu hoja kwa viroja!.
Kwenye hizi hoja za Udini, Tanzania tuna tatizo la mazoea ya kitu kinachoitwa Mfumo Kristu, unaoshikiliwa na Kanisa Katoliki Tanzania kupitia TEC, ambapo it's is systematic rais wa Tanzania akiwa Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki!. Hii haijaandikwa popote ila ndio hivyo!. Juliasi ni Mkatoliki, Benyamin ni Mkatoliki, Yohana ni Mkatoliki, anayefuata ni Emanueli!.
Hii imewafanya Wakatoliki kujisikia kuwa na an upper hand kwenye utawala wa nchi hii!.
Kwa sababu pia ni ukweli usiofichika, idadi ya wasomi Wakristo ni kubwa zaidi ya wasomi Waislamu, automatically kwenye teuzi nyingi lazima kutajaa Wakristo, hii ikapelekea Wakristo kujiona wao ni deserving kutawala idadi ya teuzi zote.
Tuhuma za Udini zikaanzia kwa Mwalimu Nyerere kuwa amejaza Wakatoliki kwenye serikali yake, Waislamu wakaanza kuita ni Mfumo Kristo, Father Sivalon ameandika kitabu kuhusu Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania.
Wakati wa Nyerere, kuwapata Waislamu wenye sifa za kuteuliwa ilikuwa ni wa kutafuta kwa tochi.
Mfano Benki Kuu ya Tanzania, ilihitaji kuwa na Naibu kutoka Zanzibar, sifa ni awe na Ph.D ya uchumi +10 years experience post Ph.D, mtu huyo hakuwapo, hivyo wa kwanza kupatikana ni enzi za JK.
Tanzania tuna ma CDF 8, kati ya hao mwenye jina la Kiislamu ni mmoja tuu, Abdullah Twalipo tena usikute ni jina tuu kama Jaji Mkuu Saidi au Jaji Ramadhani, majina ya Kiislamu, wenyewe Wakristo.
Samia akiteua CDF Muislamu sasa hivi utasikia kelele jeshini!, hii ndio mara ya kwanza Mnadhimu Mkuu ni kutoka Zanzibar!, kelele!.
Hakuna rais alukuwa na mkabila, mdini na nepotism kama JPM, kwa vile alikuwa Mkatoliki, hakuna kelele, sio tuu aliteua kabila lake tuu, ndugu zake, rafiki zake hadi something zake!, watu kimya.
Samia kateua tuu mtoto na mkwe, kelele!. Kiukweli Samia hana udini wowote, tatizo ni
1. Ni Mwanamke
2. Muislamu
3. Mzazibari mwenye nywele za singa
Enzi za Mwinyi hakukuwa na kelele hivi, hivyo huyu Mama wanamuonea tuu kwa uanamke wake!, dini yake na asili yake.
Tusiruhusu
P