Hivi ina maana wachawi hawapo kabisa JF?

Hivi ina maana wachawi hawapo kabisa JF?

Hawawezi kusema kwamba wapo, labda wale waliokua Wachawi wakaokoka.

Wachawi wengi walifundishwa Uchawi wakiwa Watoto bila kujua Madhara yake, Kwa Utoto wao wali enjoy kuruka Kichawi na kufanya Uchawi, baada ya kupata Akili, wengi wanajuta, wanatamani kuacha Uchawi lakini inakua ngumu Kadri ya mikataba Yao waliyoingia, kitendo Cha kuacha Uchawi ni Uasi, na Hukumu yake ni Kifo, utauwawa na Wachawi wenzako.

Ni wale wanaoacha Uchawi Kwa maombi ndiyo Wana Ulinzi.... Wapo Wachawi wengi wanatamani kutaka kuacha Uchawi, ila wanashindwa na njia salama zaidi ni Kuombewa na kuokoka, na bado hakuna huduma rasmi inayohudumu na kuondoa Uchawi Kwa Watu, Wachache wanaoacha Uchawi na kuokoka ni Kwa sababu ya Neema ya Mungu Kwa kile alichoweka kwao, na Shetani akawahi kuwaiba Toka Utotoni, na Wakati ukifika Mungu anawatoa huko mwenyewe, that's why Wachawi wengi na Waganga wengi wanapookoka straight wanakua Wachungaji nakuanza kuhubiri, coz wako na Chanell ambayo Mungu aliweka kwao Kwa kazi yake, na ni Chanell hiyo hiyo Shetani naye anahitaji Kwa Kazi za Giza....!

Wachawi wengi na Waganga wengi, wasingekua Wachawi wangekua Watu wakubwa.....! Na ndiyo hicho Shetani anataka, Shetani haangaiki na Mtu useless.
Mh,inahuzunisha sana....ni no kuvunja maagano mpaka kifo
 
Kwahiyo hao waganga wote tofauti kupitia ramli zao walisema kitu kimoja kwa maana wote waliona kupitia ramli kuwa huyo binti alirogwa na ndugu wa karibu?
Wote walidai hivyo ndio
 
Kosugi soma hapa usiwe unauliza vitu mara mbili mbili

Mistari ya longitude na latitude inapimika kwa kutumia GPS deivices haya tuambie uchawi unaupima kwa kutumia nini?
We kiazi mistari ya longitude na latitude ni imaginery lines hizo GPS huwa zinasoma coordinates point tu sio hizo latitude na longitude.
Nimekuuliza una uhakika kila kitu unakihisi,unakiona ama kukishika!?
Hujanipa jibu bado.
 
Tuoneshe behind the scenes ya uchawi kama tunavyoona mazingahombwe acha kurukaruka kama huna uthibitisho kaa kimya
Karne ya 15 huko ulaya watu waliuwawa kwa tuhuma za uchawi , wanasayansi wakafuatilia visa vya watu walio uwawa karne ya 17 ikaja thibitika watu hao walikua na shida ya akili, kutokana na tabia zao za ajabu wakapewa tuhuma za kichawi.🤔
 
  • Thanks
Reactions: Lax
We kiazi mistari ya longitude na latitude ni imaginery lines hizo GPS huwa zinasoma coordinates point tu sio hizo latitude na longitude.
Nimekuuliza una uhakika kila kitu unakihisi,unakiona ama kukishika!?
Hujanipa jibu bado.
Ushaanza kuleta matusi kwenye hoja ni dalili ya kuishiwa hoja
 
Karne ya 15 huko ulaya watu waliuwawa kwa tuhuma za uchawi , wanasayansi wakafuatilia visa vya watu walio uwawa karne ya 17 ikaja thibitika watu hao walikua na shida ya akili, kutokana na tabia zao za ajabu wakapewa tuhuma za kichawi.🤔
Uchawi hauwezi thibitika popote kivyovyote uongo tu
 
Uchawi hauwezi thibitika popote kivyovyote uongo tu
Kuna magonjwa kipindi cha nyuma yalisemekana ni uchawi na kulogwa ila yalivyopata fumbuzi za kitabibu hiyo dhana ikapotea.
 
Mh,inahuzunisha sana....ni no kuvunja maagano mpaka kifo
Hata Wachawi wengi hawajui Lucifer mwenyewe ndiyo anaendesha hizo Secret society za Uchawi, coz Kwa level ya Uchawi wa wengi hawawezi kumsogelea Lucifer ila wanapokea Maelekezo Toka Kwa Wakubwa wao.

Mpango wa Lucifer ni kuwafanya Watu wasimwabudu Mungu, na njia aliyotumia ni kuingiza Uchawi kwenye Kila Familia, na amefanikiwa.

Kuvunja Maagano inahitaji uelewa na Muongozo wa Mungu mwenyewe, watu Watu walikufa, kuwa Wendawazimu hata kupata Ulemavu Kwa kujaribu kuvunja Madhabahu za Ukoo Kwa Akili zao, kumbuka Uchawi umeingia kwenye familia zetu labda kizazi Cha 7 ama 10 huko Nyuma, tukiamini ni Mizimu ya familia lakini nyuma ya hizo Spirit kuna Majini (Mapepo /Family Spirit).

Kuna Maagano Mababu labda miaka 500 iliyopita walifanya wakiamini wanalinda Familia na Ubaya, kumbe waliingiza matatizo kwenye Ukoo, bila mwongozo wa Mungu SI kazi ndogo, ni HATARI kuvunja Madhabahu kwa Akili zako.
 
Kuna magonjwa kipindi cha nyuma yalisemekana ni uchawi na kulogwa ila yalivyopata fumbuzi za kitabibu hiyo dhana ikapotea.
Wakishindwa kufikiria na kutambua magonjwa na matatizo ya kimwili na kimaisha wanasingizia uchawi kitu ambacho hakijawahi kuwepo duniani kote
 
Ile ni true stori bro kama unavyoona hizi tamthilia za Ottoman empire basi na Ile ni vile vile.
Sema kwa kuendelea kwa dunia ana civilization pamoja na globalization kutamalaki haya mambo yamepungua.
Uliwahi kuona mzungu anang'ang'ania umuuzie bangili ya shaba!?
Sijawai

Ila German Wana uchawi wa kijerumaniii

Umenikumbusha nyuzii za RUPIA/ MALI ZA MJERUMANII
 
Kosugi soma hapa usiwe unauliza vitu mara mbili mbili

Mistari ya longitude na latitude inapimika kwa kutumia GPS deivices haya tuambie uchawi unaupima kwa kutumia nini?
Nimeshakukosoa HUWEZI UKAPIMA MSTARI WA LONGITUDE NA LATITUDE.
Zinazopimwa ni coordinates points zinazotokana na makisio ya hizo longitude na latitude.
Jibu swali langu unaweza ukapima kila kitu?
Can you sense,feel or touch a soul?
Can you prove scientifically that there is a soul in a body!?
 
Wote walidai hivyo ndio
Sasa kwanza hiyo inawezekanaje watu wakasema kitu kimoja kwamba ni coincedence tu au vp? Kwanini wengine wasingesema kitu tofauti labda karogwa tu na mtu mwengine au kakumbwa tu na jini na si kwamba karogwa na ndugu? Na kote huko alikopita alipatiwa matibabu akashindwa kupona au aliishia kupiga ramli tu?

Kuna maswali mengi ya kuuliza ili kuelewa hilo tukio zima, maana yawezekana ni kweli huyo binti karogwa kama walivyosema hao waganga wote kupitia ramli kwamba chanzo cha huo ugonjwa ni huko kurogwa maana wapo watu pia wana ushuhuda wa kwamba walikuwa wanaumwa ugonjwa wenye kujulikana kabisa ila wamezunguka sana mahospitali na kumaliza madawa ila wakaja kupona kwa waganga yote yapo hayo mkuu.
 
Basi ngoja nikupe mfano hai. ,kuna binti mmoja alikua anaanguka na kutoa povu , wazazi wake wakazunguka mikoa mbalimbali kwa wapiga ramli kila mmoja akasema wamelogwa na ndugu wa karibu na kutupiwa majini .

Tukamshauri aende hospital ikagundulika ni kifafaa ,akaanza dawa akarudi kwenye hali yake ya kawaida.

Ikawaje hao wapiga ramli waseme hivyo na kushindwa kugundua sababu?

Note: sijasema tiba za. Mitishamba hazipo.
Sasa hapo mkuu unajua kuna nini!?
Kuna uendekezaji wa mila za kishirikina.
Sasa ukiwa unaendekeza mila za kishirikina lazima utakutana na wajanja wa mjini wataenda sawa na imani zako vile vile watakupiga hela.
Hiyo ni kitu uendekezaji,na waganga waongo waongo sana.
Ni kama hawa mashehe ubwabwa na mapadre wajaza mitungi ya gesi kwa mdomo.
Ukiwafuata lazima wakudanganye ooh una jini mahaba ooh umerogwa.
Ukiendekeza imani za kishirikina hilo ni tatizo.
 
Back
Top Bottom