Hivi hii ya mtoto wa kwanza kuwa makamu wa wazazi ni Tanzania pekee au kote?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Nilikuwa nasoma sehemu nikakuta kuwa watoto wa kwanza wanalalamikia kuwa "Makamu Mzazi". Yaani ni mtoto anayekabidhiwa jezi kabla mchezo hajauelewa. Mtoto wa kwanza anatarajiwa kulea wadogo zake na wazazi wake at the same time. Nadhani ukiona mtu amekomaa kimawazo, unauliza tu "Hivi wewe ni mtoto wa kwanza eekh"

Kwenye jamii ni ngumu kujua mtoto wa kati, ila wa kwanza na wa mwisho ni rahisi kumbaini. hivi hili suala la mtoto wa kwanza kuwa mzazi ni dunia nzima au ni bongo tu?

Mimi kwetu ni wa kwanza, aisee, naombeni mwenye kamba aniuzie kwa bei yeyote, nina kazi nayo
 
Kuzaa watoto ni mfumo wa kitumwa, yaani mtu anazaa ili mtoto hapa duniani awe chini yake.

Wazazi ndio watu wa kwanza kuharibu maisha ya watoto wao, wao ndio chanzo wengine kuwa matajiri au maskini.

Mtu anazaa tena kundi kubwa eti ili uje kuwasaidia, kujazana dunia ni mfumo wa pata potea juhudi zote ila mwishoe mnakufa.

Zaa mtoto Africa awe mtu wa wazungu milele.
 
Ukiacha kufanya majukumu ya mtoto wa kwanza kuna atakaye ichukua nafasi yako. Utagundua hilo wakati wa vikao vya familia.

Yule anayebeba majukumu ndiye anayesikilizwa, ndiye anayeheshimiwa, ndiye mwenye sauti pengine kuliko ya baba sema heshima hufata mkondo wake, ndiye anayeamua wawe na familia ya aina gani. Ndiye anayeamua identity na heshima ya familia kwenye jamii inayomzunguka.

Unaposikia familia ya Mengi au Familia ya Ongala, au Familia ya Kikwete, au Familia ya Osea, ile heshima ni matokeo ya kazi zilizofanywa na wazazi na uzao wao.
 
Majukumu ni ngumu kuyaacha, ila nawaza namna ya kubadili utaratibu. Yaani mtoto wa kwanza unapewa majukumu mazito, wakati mwingine uko mtoto unaambiwe, "wewe ndio mkubwa", "Una wadogo zako" haya yote ni kukufanya uone tayari uko uwanjani.

Ukishaingia uwanjani ndio kimbembe kabisa, hadi mtoto wa shangazi unaletewa umuangalie wewe. Heshima unayopata ni ile tu "Huyu ndio atatuzika" yaani nazika mtu wakati mwenyewe sielewi dah
 
Mkuu, ni kweli ila binafsi naamini kuna malipo yake tofauti na kutokufanya. Ukishakuwa mtoto wa kwanza ni bora kujipa semina kabisa kuwa unatakiwa upate zaidi. Angalizo: Usibebe mzigo nje ya familia yenu, usihamie kwa mashangazi sijui wajomba. Hutotoka kwenye hiyo circle na utadondokea kwenye umasikini.

Hao wa mashangazi watakufanya uwe masikini wa kutupwa ukiwaendekeza. Bora uchukiwe tu.
 
Unapigiwa simu na mzee wako anakuambia kuna mdogo wako nimempa namba yako anakuja huko. Unapigiwa simu mtu kashafika mjini anakusubiri kwa Magufuli, mzee wako anakuambia, sasa shangazi yako anaumwa, huyo mtoto ni mwanaye haukuwahi kumuona kwa kuwa alikuwa kwa ndugu yake wa kijijini, ila kwa kuwa wewe uko mjini tumeona umpeleke shule hata VETA ili amsaidie shangazi yako.

Hapo wewe utafanyaje, na mtoto wa watu kashafika mjini.
 
Mzee wako unamwambia bila woga kuhusu ukomo wa majukumu yako na yake kwa ndugu zake. Yeye atatafuta busara ya kuzungumza nao wanapohitaji msaada.

Mfano: Ndugu anataka kuja Dar, Mwambie mzee unaweza mpokea kwa siku moja au mbili kisha aondoke, tofauti na hapo basi ada ya mdogo wangu nitahitaji hilo jukumu nilihamishie kwenu sababu ili huyu ndugu apate, inabidi kuna sehemu pakose huduma.

Ukiwa unaongea nae kwa uwazi, atajiongeza. Unampa na mifano ya pipi tano watoto watano, ili kila mmoja ale pipi moja inabidi asiongezeke mtoto wa 6.
 
Ukiacha kufanya majukumu ya mtoto wa kwanza kuna atakaye ichukua nafasi yako. Utagundua hilo wakati wa vikao vya familia.

Yule anayebeba majukumu ndiye anayesikilizwa, ndiye anayeheshimiwa, ndiye mwenye sauti pengine kuliko ya baba sema heshima hufata mkondo wake, ndiye anayeamua wawe na familia ya aina gani. Ndiye anayeamua identity na heshima ya familia kwenye jamii inayomzunguka.

Unaposikia familia ya Mengi au Familia ya Ongala, au Familia ya Kikwete, au Familia ya Osea, ile heshima ni matokeo ya kazi zilizofanywa na wazazi na uzao wao.
Acha ujinga wewe, mjomba wangu ana watoto wanne mdogo wa mwisho kafanikiwa kama ajafika kikao akifanyiki mpaka awepo na yeye ndio anaongea sana kuliko wengine. Sasa hivi aliyefanikiwa zaidi ndio anasikilizwa.
 
acha ujinga wewe, mjomba wangu ana watoto wanne mdogo wa mwisho kafanikiwa kama ajafika kikao akifanyiki mpaka awepo na yeye ndio anaongea sana kuliko wengine.
Sasa hivi aliyefanikiwa zaidi ndio anasikilizwa
Ukiona kikao hakifanyiki bila wewe, jua wewe ukoo ni wako, unaangaliwa wewe kwa kila kitu, ni nzuri na ni mbaya
 
Nilikuwa nasoma sehemu nikakuta kuwa watoto wa kwanza wanalalamikia kuwa "Makamu Mzazi". Yaani ni mtoto anayekabidhiwa jezi kabla mchezo hajauelewa. Mtoto wa kwanza anatarajiwa kulea wadogo zake na wazazi wake at the same time. Nadhani ukiona mtu amekomaa kimawazo, unauliza tu "Hivi wewe ni mtoto wa kwanza eekh"

Kwenye jamii ni ngumu kujua mtoto wa kati, ila wa kwanza na wa mwisho ni rahisi kumbaini. hivi hili suala la mtoto wa kwanza kuwa mzazi ni dunia nzima au ni bongo tu?

Mimi kwetu ni wa kwanza, aisee, naombeni mwenye kamba aniuzie kwa bei yeyote, nina kazi nayo
Dr Mwinyi si mtoto wa kwanza but ndio mlezi wa wenzie 🐒

even I,
ni mdogo miongoni mwa wanafamilia but ndio kiongozi na mlezi wa familia, miongoni mwa wanafamilia 7, na tunakwendra vizuri pamoja, kwa Neema na Baraka za Mungu 🐒
 
Nilikuwa nasoma sehemu nikakuta kuwa watoto wa kwanza wanalalamikia kuwa "Makamu Mzazi". Yaani ni mtoto anayekabidhiwa jezi kabla mchezo hajauelewa. Mtoto wa kwanza anatarajiwa kulea wadogo zake na wazazi wake at the same time. Nadhani ukiona mtu amekomaa kimawazo, unauliza tu "Hivi wewe ni mtoto wa kwanza eekh"

Kwenye jamii ni ngumu kujua mtoto wa kati, ila wa kwanza na wa mwisho ni rahisi kumbaini. hivi hili suala la mtoto wa kwanza kuwa mzazi ni dunia nzima au ni bongo tu?

Mimi kwetu ni wa kwanza, aisee, naombeni mwenye kamba aniuzie kwa bei yeyote, nina kazi nayo
Pole sana Mkuu. Mimi kamba ninayo ila naogopa nisije kuwasaidia jamaa katika hilo unalokusudia kulifanya. Kaza buti na mwisho utafanikiwa tu.
 
Unapigiwa simu na mzee wako anakuambia kuna mdogo wako nimempa namba yako anakuja huko. Unapigiwa simu mtu kashafika mjini anakusubiri kwa Magufuli, mzee wako anakuambia, sasa shangazi yako anaumwa, huyo mtoto ni mwanaye haukuwahi kumuona kwa kuwa alikuwa kwa ndugu yake wa kijijini, ila kwa kuwa wewe uko mjini tumeona umpeleke shule hata VETA ili amsaidie shangazi yako.

Hapo wewe utafanyaje, na mtoto wa watu kashafika mjini.
Huku ni kutafutana ubaya tu
 
Back
Top Bottom