sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Elimu sio ya kuibeza lakini ni vipi kama mzazi/mlezi una biashara ama umejiajiri kwanini umkazanie mtoto awe anasoma tu wakati wewe una formula ya uhakika ya kupiga pesa ? inasahangaza kuona mzazi anaingiza almost milioni 3 na kuendelea kila mwezi lakini anamkazania mtoto awe anasoma tu ili aje "KUJARIBU BAHATI YA KUAJIRIWA" (ni bahati kwasababu ajira zimekuwa ngumu na huenda mtoto shule ikamshinda), Kuna haja gani ya kusubiria mtoto apitie msoto ndio uanze kumshirikisha kwenye biashara wakati unaweza kuanza nae tangu ana miaka 10 ? mbaya zaidi ukiondoka mapema hata watoto hawana idea ya kusimamia mambo yako watauza mali zako kwa bei za kutupa na biashara kufilisika.
Na hapa kuna wazazi wanawafundisha watoto biashara ama kujiajiri ndivyo sivyo, Biashara kama duka unakuta mtoto tangu mdogo anachojua ni kuuza tu wala hajui faida inayopatikana, mzigo unaponunuliwa, vibali, kodi, n.k. Na mzazi anajisifu na kujipiga kifua kwamba anamfundisha mtoto biashara, LA HASHA !! Unamwandaaa aje auzie wengine maduka kwa mshahara wa laki 1.
Nao waliojiajiri mfano wakulima na wafugaji unakuta wanachofundisha watoto ni kuchunga ngombe na kulima tu, wala hawajawahi kwenda nao mnadani ama sokoni kutafuta wateja, kumfundisha mtoto kunegotiate, kumpa mtoto iridha ya wateja, n.k. mtoto akiulizia mzazi anamwambia soma kwanza !! ni kweli kusoma ni muhimu lakini kuna ubaya gani kumuongezea elimu ya kujipatia kipato cha uhakika ? kumyima mtoto haya maarifa ni kumuandaa awe shamba boy au mchungaji wa mbuzi.
Mimi binafsi kama mzazi nilipomaliza chuo nilipitia msoto nikimaliza soli kutafuta ajira, nilipewa kamtaji kufungua duka langu ila ugeni wangu katika biashara ulizifanya changamoto nazokutana nazo kwa mara ya kwanza zinilambe mitama huku nikipata faida ndogo sana, baada ya miaka kadhaa nikapata ajira stable lakini nikaona kazini pekee kutegemea mshahara ni kuridhika, sikukomaa vizuri kwa uzoefu kwenye biashara niliyofanya kabla sijaajiriwa lakini baada ya kuajiriwa bado nilikuwa na kiu kiu kuendelea na biashara, kama kawaida changamoto zilinilamba mitama ila kwa with time nimekuwa mzoefu na nina biashara kadhaa zinazonipa faida, nipo na confidence kubwa kwenye biashara na ndio imenibadilisha hata kiuchumi, account inasoma visifuri vya ziada.
Nilipostuka nimefungua kaduka ka mahitaji kwa mtaji wa kawaida kabisa kwa lengo la kusimulate watoto, nimeweka binti wa kuuza, ila watoto nilienda nao TRA kukata tax clearance, Niliwashirikisha closely kupata Tin namba ya eneo la biashara, niliwaonesha namna ya kulipia leseni ya biashara, wao ndio watakuwa wanalipia kodi ya makadirio kila baada ya miezi minne, kufanya stock kila siku litakuwa jukumu lao, n.k. Baada ya mwaka au miezi 6 nimepanga kuifunga hii biashara kisha nifungue upya kwa lengo la kuwazoesha wazoee process za kufungua na vibali.
Mwakani hivi naona watakuwa wamezoea zoea ndio ntaanza kuwashirikisha kwenye biashara zangu kuu.