Watoto; Kalamu inaweza kukutengeneza kuwa Rais Samia, Wazazi; Mtoto wa jirani ni wako

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
WATOTO; KALAMU INAWEZA KUKUTENGENEZA KUWA RAIS SAMIA, WAZAZI; MTOTO WA JIRANI NI WAKO- SUPHIAN


Wiki hii tunapoelekea mwisho wa mwaka 2023, Shule ya awali (Nursery) ya Comfort Day Care and Pre School imefanya Mahafali ya tatu ya kuwaaga watoto wa darasa la awali ambapo Mgeni Rasmi amekuwa Mdau wa Elimu na Haki za watoto, kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Suphian Juma Nkuwi.

Bwana Suphian kama Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule hiyo iliyopo Kimara, Dar es Salaam pamoja na mambo mengine alizindua Kampeni ya upandaji miti shuleni hapo ambapo alipanda miti na wanafunzi wahitimu na Wazazi kama sehemu ya kuwajengea watoto wadogo utamaduni wa kupanda miti na kuunga Juhudi za Rais Dkt Samia aliyekuwa Dubai kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na athari za mabadiliko ya tabia Nchi.

"Watoto wangu na Wazazi kabla sijaja nilimsihi Mkuu wa Shule madam Patricia Richard kuandaa Kampeni ya kupanda miti lengo ili kuwakuza watoto wetu na Utamaduni wa kupanda miti kuliko kukata miti kudhibiti ukame nchini kama sehemu ya kuungana na Rais wetu Dkt Samia ambaye yupo Dubai kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kujadili suluhu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi."

Aidha baada ya wanafunzi kumsomea Mgeni Rasmi ngojera ambapo kila mwanafunzi alitaja nyadhifa wanazotamani kuwa navyo wakikua, ndugu Suphian aliwaita wanafunzi waagwa wote mbele na kuwagawia kalamu kama zawadi na kuwafunda namna "nguvu ya kalamu" inavyoweza kuwafanya watimize ndoto zao kuu katika maisha yao ya baadae.

"Wanangu nimewasikiliza kwenye ngojera kila mmoja akitaja cheo anachotamani kuwa nacho akiwa mkubwa, sasa leo kama Mgeni Rasmi sijawaletea pipi, midoli wala maua, nimewaletea zawadi ya kalamu kwani kalamu inaweza kukufanya uwe Rais Samia, kalamu inaweza kukufanya uwe Waziri, Daktari, Mwanasheria, Mwalimu, Polisi ama yeyote yule unayeota kuwa. Itumieni vema kalamu mtafika mpatakapo."

Kwa upande wa wazazi, Suphian aliwaasa kuacha desturi mpya ya ubinafsi ya kuona kwamba mtoto wako si mtoto wa jirani yako kwani ubinafsi huu umeongeza ukatili kwa watoto majumbani na umestawisha tabia mbovu kwa watoto katika jamii kwani watoto wamekuwa na nadharia kwamba mtu pekee wa kumwadhibu akikosea ni mzazi wake pekee.

"Mtoto wangu ni Mtoto wako, Mtoto wako ni wangu na mtoto wa jirani ni mtoto wetu, akikosea msahihishe, akitenda vema mpongeze na akinyanyaswa mtetee. Wazazi tukausikilize wimbo wa "Mtoto wa Mwenzio" wa Msanii wa Injili Mwaitege, tushirikiane pamoja kuwalea vema watoto wetu kama zamani." Alisisitiza ndugu Suphian..

Akijibu changamoto za Shule zilizosomwa kwenye risala, Suphian alitimia umati huo uliohudhuria kufanya harambee "fund rising" kupatikana televisheni ya Shule ili watoto waweze kujifunza kirahisi ambapo jumla ya shilingi laki 2 na elfu 20 zilipatikana ambapo ndani ya fedha hizo yeye kama Mgeni Rasmi alianza kuchangia shilingi laki moja papo hapo.

Katika Mahafali hayo ya Shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 70 yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kutoka Sekta binafsi; Jumla ya watoto 15 waliohitimu walipatiwa vyeti vya kuhitimu tayari kwa kwenda kuanza darasa la kwanza mwakani 2024.

IMG_20231205_152123_280.jpg
_MG_6893.jpg
514D1045.jpg
IMG_20231205_152458_766.jpg
IMG_20231205_152123_257.jpg
IMG_20231205_152123_284.jpg
514D1072.jpg
IMG_20231205_152123_286.jpg
IMG_20231205_152123_292.jpg
 
Huyo mmiliki shule atakuwa ni mjinga sn, alikosa mgeni rasmi? bora hata angemchukua Mwenyekiti wa kitongozi
 
Back
Top Bottom