Mtoto wa kwanza kwetu amechukua nafasi ya mzazi

imekuaje

Member
Jan 28, 2024
34
46
Habari.

Ninaishi kwenye familia ambayo wazazi wamempa nafasi kubwa mtoto wa kwanza Tuseme first born wetu.

Kiukweli hali hii imekuwa ikinikwaza sana hadi niliapa siku nikija kuzaa sitafanya hivi kwa watoto wangu.

First Born wetu ni kama ndo msemaji mkuu wa familia, kila anachosema yeye ni sahihi hataki mawazo wala ushauri hali hii imepelekea mimi kugombana naye muda mwingi.

Kiukweli amekuwa na mchango mkubwa katika familia Yetu hata kuhakikisha sisi Wote tumesimama wenyewe.

Leo hii nimekuwa mkubwa najigemea ila nimejikuta Niko mbali na familia yangu kwa kitendo cha kuchukia dada yetu mkubwa kutaka kuchukua nafasi ya wazazi na kunyenyekewa.

Anaamua kuuza kiwanja anaamua chochote akipigwa hataki na mzazi atamsapoti kwa kila kitu.

Muda mwingi amekuwa na ukaribu na baba name Wanashirikishana Siri zao wenyewe.

Mtazamo wangu nimeamua kuwa mbali na ndugu.
 
Anaamua kuuza kiwanja anaamua chochote
Usimkimbie, mfate huko huko alipo mwambie arudishe hicho kiwanja alichouza, kama ni kuuza akauze kiwanja chake binafsi na si cha familia.

Hao ma first born ukicheka nao wanakombaga mali zote za familia na kuzitapanya pasipo faida.
 
Usimkimbie, mfate huko huko alipo mwambie arudishe hicho kiwanja alichouza, kama ni kuuza akauze kiwanja chake binafsi na si cha familia.

Hao ma first born ukicheka nao wanakombaga mali zote za familia na kuzitapanya pasipo faida.
Ndo kinachotokea amemlaghai mzazi kuuza viwanja viwili kisa huo mkoa hakuna anayekaa mimi ndo nimekomaa Kiwanja kimoja kimebaki.

Mashamba heka kumi akataka kuuza nimemgomea ugomvi mkubwa.

Hapa anataka kuuza na nyumba.

Wazazi wanamwangalia Tu.
 
Mashamba heka kumi akataka kuuza nimemgomea ugomvi mkubwa.

Hapa anataka kuuza na nyumba.

Wazazi wanamwangalia Tu.
Wala asikutushe, komaa naye asiuze mali za familia kwa matakwa yake binafsi.

Ukizubaa atauza kila kitu.
 
Unalilia viwanja vya mzee wako?

Mimi urithi wangu nitaangalia mtoto Yule mwenye akili na mwenye kumiliki vyake. Siwezi mpa mtoto ambae hana chochote maana hachelewi kuuza. Yule mwenye nacho kama angekuwa muuzaji angeuza vyake.

Huwezi ukawa unateseka na Mali za wazazi wako. Wamechuma wao ni haki yao kufanya wanachokihitaji
 
My sister ni mjuaji mbaya 😂😂😂. Pole sana. she is not involved in anything na shukuru sana.
 
Huyo dada yako mjanja. Watoto wanaoelewana na baba hula mema ya nchi. Watoto wengi huwa ni wapuuzi kuegemea kwa mzazi mmoja. Ninawashauri watu wote ambao wazazi bado wapo kuwa nao karibu sana hasa baba. Akina baba wana mambo mazito ila huwa wameuchuna tu.
 
Back
Top Bottom