Hivi hakuna namna Vijana kero ya paka na kunguru mtaani tukaifanya kuwa ajira ya muda wakati tunajitafuta?

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Feb 6, 2022
276
792
Serikali inapenda kusikia sisi vijana tunawaza nini ili watusaidie!

Siyo kila wakati ni wa kulaumu laumu tu! Wakati mwingine tupeleke maoni yetu kwenye mamlaka za serikali kama vijana!

Ukipita huko mtaani kuna paka wengi sana, kuna mbwa wengi sana, kuna panya wengi sana,kuna kunguru wengi sana, kuna popo wengi sana wanaoisumbua jamii!

Halafu wakati huohuo kama taifa tuna kundi la vijana waliosoma WILDLIFE MANAGEMENT Wanalalamika hakuna ajira!

Hivi vijana wenzangu mmewahi kupeleka mapendekezo TAWA! Ya kuomba kibali cha kuvuna hao wanyama mtaani wakawanyima?

Mfano mkajisajili vijana mkapita mtaani na vibali kuomba kukamata panya, paka, kunguru n.k hamutapa pesa?

Mfano! Mkaweka Bei ya kukamata paka mmojala iwe elfu 10, panya elfu 2, kunguru elfu 10! Mtakosa pesa?

Sisi Wananchi tutawapigia muje mtukamatie paka hata usiku wa manane cha mhimu muwe mmesajiliwa!
Faida nyingine ya kuwakamata hao wanyama mtatupunguzia na uchawi mtaani automatically!

Paka ni kero mtaani hata sehemu za starehe Paka wapo chungu mzima!
Wildlife mtakuwa Hamjapiga hela hapo?

Haya ni maoni yangu Fundi umeme samico, Endapo mkifanikiwa mkapiga hela msiache kunipa kazi ya umeme na ujenzi kupitia namba yangu 0711756341
 
sawa mkuu ntakutafuta nimependa tangazo lako wewe ni mbunifu wa kiwango cha phd
Mkuu umewahi kuwaza hatima ya hao paka mtaani kwako ni nini? Wanazaliana na hawavunwi!

Si bora zaidi hawa vijana wawepo ili jamii iwe inawapigia kuja kuvuna!

Enzi za zamani kabla ya kuja waokota makopo!

Makopo yalizagaa!

Nawashauri vijana waende kwenye mamlaka wakajisajili inaweza kuwa fursa wakawavuna hao paka!

Sisi wananchi tunaokerwa na hao paka tutalipa
 
Vijana mbona tulishachukua na kuchangamkia fursa kitambo?

Tunauza sumu ya panya, tunauza manati kwa ajili ya kunguru mbwa soko lake lipo china, Kama ni mbali kuna soko la ndani mkoani Iringa, n,k
 
Serikali inapenda kusikia sisi vijana tunawaza nini ili watusaidie!

Siyo kila wakati ni wa kulaumu laumu tu! Wakati mwingine tupeleke maoni yetu kwenye mamlaka za serikali kama vijana...

Mkuu Tanzania bora huanza na wewe.

Kwani hadi wa sasa wewe umekwishalala mbele na mapaka na mbwa wangapi?
 
Back
Top Bottom