Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,890
NAMNA YA KUJIHAMI NA PANYA ROAD, AU MAKUNDI YA NAMNA HIYO!
Anaandika, Robert Heriel
Mara ya Kwanza Panya Road niliwaona mwaka 2016, Maeneo ya Tandale, kipindi hicho nilikuwa nasoma chuo, DSM. Kilichokuwa kinanipelekea Tandale licha ya kuwa nilikuwa nikiishi Sinza Lion; ni kwenda kushangaa maisha ya uswahilini ambayo sikuwahi kuyaona, hivyo kila jumamosi na jumapili nilikuwa nikienda huko Tandale Kwa rafiki yangu niliyesoma naye O'Level huko Makanya, Same, Kilimanjaro. Huko niliona mambo ya kustaajabisha, kuchukiza na pia kufurahisha. Huko ndiko niliona Vigodoro na vigoma, hivi vilikuwa vinanivutia mno ukizingatia nilikuwa kijana Mdogo damu inachemka.
Nilikuwa napenda Sana kuona wanawake wakicheza huku wakibinua makalio Yao juu Kwa staili ya chura, Kama hiyo haitoshi Baadhi ya Maeneo Kama uwanja wa laana wengine walifikia hatua ya kuvua nguo na kubaki uchi au navichupi tuu. Hiyo kwangu ungeiita starehe ya kufurahisha macho.
Kama nisingeyaona hayo Kwa umri ule ningali kijana Mdogo sitegemei Kama ningeyaona wakati mwingine wowote ule katika ukuaji wangu nikayafurahia, ulikuwa wakati sahihi Kabisa.
Mbali na vigodoro niliwahi ona matukio mawili ya Panya road;
Siku hiyo ikafika baada ya usumbufu WA muda mrefu.
Ilikuwa jioni nyakati za jua kupunga, Rafiki yangu akaniambia Leo utawaona Panya road, nilijawa na shauku ya kujua wakoje.
Akaniambia, Leo kuna mechi Kati ya Tandale na Mwananyamala, hivyo Leo lazima ujionee panya Road.
Tukiwa njiani nikitaka tufike huko uwanjani, Rafiki yangu akasema ilete simu yako panga road sekunde chache zijazo watakuwa wametia Timu. Kabla hajamaliza nilishuhudia kundi kubwa la Vijana likitokea mbele yetu umbali wa urefu WA uwanja wa mpira. Walikuwa wametoka kwenye mpira lakini walikuwa wakipiga kelele za kihuni; Oyo! Oyo! oyo! Huku wakiimba nyimbo za kihuni nisizokuwa nimewahi kuzisikia.
Wakati wakifanya hivyo walikuwa wakivamia Upande wa kushoto na kulia wa barabara na kupora na kujeruhi watu hovyo hovyo!
Watu wa mtaa ule niliwaona wakikimbia hovyohovyo wakiingia ndani huku baadhi ya wanawake na watoto wakipiga kelele.
Taikon niliogopa wale nisiwadanganye, niliogopa Kwa sababu mbili; Mosi, walikuwa wakipiga kelele na kutengenez hofu. Si unajua kelele zinaleta utisho. Mbili, matukio waliyokuwa wanafanya Kama kuchoma watu visu na bisibisi, kuwapoga watu hovyo huku wakipora vitu vya wafanyabiashara waliokuwa wanauza pembezoni mwa njia Ile inayotokea Sokoni.
Jambo moja nililo-note ni kuwa Panya road hawakuvamia wala kupita karibu na Wakaanga chips, nafikiri waliogopa Kumwagiwa Mafuta ya Moto, pia hawakuwa wanapita karibu na Wauza vipande vya miwa, nafikiri walihofia wauza miwa na vipande vyake kuwa na silaha Kama visu na mapanga,
Mimi sijanyoa kiduku, na mtu yeyote akiniona hata Kama nipo Rafu atajua tuu Mimi sio mhuni. Lakini sio Kwa Rafiki yangu, yeye alikaribiana nao kufanana, alikuwa na uduku kichwani, nguo zilifanana nao, pamoja na ngozi isiyo na rutuba.
Rafiki yangu akaniambia sogea pembeni kabisa, tukasogea pembeni lakini akasema usisimame tutembee tupishane nao, basi walipotukaribia Kama hatua kumi hivi, Rafiki yangu akawapokea Kwa kusema Oyo!Oyo! oyo! Huku na Mimi nikiwa nadakia kuonyesha tupo pamoja. Nilimuona rafiki yangu akiwa kaupenyeza Mkono wake kwenye kiuno mahali ambapo anawekaga Bisibisi ndefu , ili kujihami Kama lolote lingetokea. Lakini wale pants road walitupita tukawa katikati Yao Kwa sekunde kadhaa kutokana na wingi wao. Baadaye walikuwa wametupita huku Mimi wakiniacha Hoi Kwa hofu.
Kwa vile tamasha lile lilikuwa la bure basi watu walifurika mno, wahuni wakiwa wengi zaidi.
Wahuni kutoka Tandale, Mwananyamala, Manzese, Magomeni, na wambali zaidi walitokea Mbagala na Temeke (hawa walikuwa wachache)
Nilienda kwenye tamasha hili nikiwa na Yule Yule Rafikiangu, unajua wengine tunapenda ku- socialize ukiniita sociologist hautakuwa umekosea.
Kujichanganya kwenye jamii inakupa kitu inaitwa Interpersonal skills yaani Ujuzi wa kuchangamana na kujamiiana na watu wengine. Hii itakufanya uhitimi kozi ya kitaaolojia. Elimu ya mtaani.
Hicho ndicho ambacho nilikuwa nakitafuta.
Hakika Rafikiangu licha ya kuwa nilikuwa nimemzidi kielimu Kwa mbali mno, lakini kwenye elimu kitaaolojia aliniacha mbali Sana.
Tulipokuwa kwenye lile Tamasha tukimsubiri Mgeni Rasmi Paul Makonda ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Mkoa.
Rafiki yangu alikuwa akiniambia tuhame hapa twende pale, kisha tukifika pale, akawa ananipa sababu za kuhama eneo la awali, akasema; unawaona wale washikaji(nikawatazama), wale ni wahuni, panya roads, kukaa karibu nao lolote linaweza kutokea, wanaweza kukuibia, au Polisi wakija wakibebwa na wewe unaweza kujikuta umesombwa nao.
Akaendelea; unaona pale, wanataka kumuibia Yule mshikaji aliye na demu wake. Hapo nikataka nione wataibaje, dakika tano hazikuzidi wakamuibia kutokana na msongamano, Yule kijana baada ya kugundua ameibiwa ndani ya Ileile sekunde tukio la wizi likifanyika akageuka lakini nikamuona Yule mwizi akiondoka huku wezi wenzake wakijaribu kumsonga Yule kijana wakijifanya wanamuuliza umeibiwa, umeibiwa nini, simu gani, huku wakijitahidi kumsaidia kumbe wakimzuia Yule kijana na kusababisha Yule mwizi azidi kuepa na kutokomea.
Tukio hili likanipa ujumbe kuwa, ukiibiwa kwenye matukio ya namna hii, 90% watakaokuzonga na kujifanya wanakupa msaada ni sehemu ya wezi.
Ukiwa kwenye mikusanyiko ya watu hasa watu usiowajua ni vizuri ukasoma Maumbile, saikolojia ya mwili, Mavazi, nyendo za wanaokuzunguka, iwe ni kwenye matamasha, iwe mi kwenye fukwe za starehe. Usikubali kuzungukwa na watu usiowajua, usikubali kuzungumza na watu usiowajua ikiwa sio wewe uliyeyaanzisha mazungumzo, jitahidi unapoongea na mtu umtazame machoni, asikubabaisha Kwa kukuzuga na vitendo vyake ukapoteza umakini WA kuangalia macho yake.
Macho ndio yamebeba Kwa kiasi kikubwa saikolojia ya mwili WA binadamu.
Tamasha lile walikuwepo Askari Kanzu, lakini walikuwepo wachache, vurugu zilipotokea Polisi na magari Yao walifika, basi ikawa mshike mkamate, wahuni walikuwa wakikimbia huku Raia wema nao wenye hofu nao wakikimbia Hali iliyofanya Polisi kukamata yeyote aliyekaribu. Walikamatwa baadhi ya panga road huku mmoja akinusurika kufa Kwa kujirusha kwenye Gari la polisi na kuangukia chini ya Daraja pale Uwanja wa TP.
Jambo moja ninalotaka kulisema, kwenye matukio Kama haya ukiona yametokea, Kama wewe sio Mhuni usikimbie kimbie hovyo, ikiwezekana tafuta Nafasi ujifiche, iwe ni kwenye mti au Jiwe au ukuta n.k. kukimbia kutafanya ukamatwe na polisi kwani watadhani nawe ni mmoja wao. Hivi ndivyo ilivyotokea.
Lakini hakikisha, waliokuja kukamata ni polisi, ndio ufanye hivyo, usije ukasimama kumbe tukio hilo linaratibiwa na wahuni au Magaidi kama Kule Garisa KENYA.
Baada ya kuandika maelezo mengi ambayo wengi hamyapendi, sasa hivi ndivyo jinsi mtakavyo jihami na panga road au makundi ya namna hiyo;
1. Elewa maumbile na saikolojia yao.
Panga road wengi wao ni dhoofu ilhali, hawana Afya kutokana na lishe duni, hivyo hawana nguvu, hivyo hawatakuruhusu upigane nao kwani wanajijua hawana nguvu pia wengi wao umri wao ni mdogo hivyo watatumia silaha Kama visit, bisibisi, viwembe au marungu.
Saikolojia yao imetawaliwa na vilevi na madawa, hivyo ukikutana nao usithubutu kujieleza, amua kupigana na uwe umevurugwa zaidi Yao, au kimbia( utakimbia Kama upo barabarani lakini kama ni nyumbani kwako usikimbie).
2. Usiwekwe mtu Kati unapopishana na watu au kundi la watu.
Unapotembea barabarani au kichochoroni, ikiwa mbele wanakuja watu wawili au kundi la watu, usikubali upite katikati Yao, jitahidi ukae pembeni kabisa hasa upande ambao ni rahisi kujihami aidha Kwa kukimbia au aliyeupande huo ni mdhaifu kuliko kuliko wewe.
Usiende upande wa mtu unayemuona ananguvu kukushinda, jitahidi usome nyendo zao wakati mnapishana hasa macho na mikono Yao.
Au ukae upande ambao ni rahisi kukimbia, Kama ni barabarani pasiwe na maporomoko, daraja au vichaka vyenye miba. Kaa upande ambao ukishindwa kujihami utakimbia.
3. Mwanaume yeyote usikose silaha ndogo ya kujitetea.
Silaha Kama kiwembe, Bisibisi, Kalamu, na Kama upo ndani ya Gari basi silaha Kama Kisu, jambia, Rungu, au Bastola.
Wanawake wao hutembea na Pochi na kuweka vitu vyao, Kama vipodozi, vioo, kanga n.k.
Hivyo na Kwa mwanaume lazima utembee na silaha yoyote ya kujihami lolote linapotokea.
Kama huna Ujuzi WA mapigano ya kujilinda.
Mara nyingi panya road hawapambani na watu wenye silaha Kama wao, watu waliojiandaa Panya road hawapotezagi muda wao, labda wawe wengi nawe uwe pekeako.
Matukio ya Panya road yaliwahi tokea Magomeni watu walikimbia wakaacha magari Yao. Ila Kama kila mwenye Gari angekuwa na silaha yoyote ya kujilinda basi wangeweza kupambana nao.
4. Panya road wengi wamejiandaa kufa hivyo pigana ukijua unayepigana naye Hana chakupoteza. Usiogope Jela.
Unapopigana na mtu ambaye haogopi kufa basi itakubidi wewe usiogope Jela, kwani ukiogopa jela hautapambana vizuri na utaiweka roho yako rehani na kujikuta wewe ndiye unakufa alafu mwenzako anaenda Jela.
Piga kadiri ya mtu anayetaka kuua, mengine yatajulikana mbele Kwa mbele.
5. Hakikisha hapo Mtaani kwenu wanakujua kuwa wewe unaroho mbaya Kama Shetani.
Jitahidi mtaani wamama na vijana wakujue kuwa wewe sio mtu wa mchezo ikiwa unakaa mitaa ya uswahilini.
Ni lazima ufanye tukio moja kubwa ambalo litakufanya ujulikane Mtaa mzima na serikali za mitaa.
Kama ni kijana amejaribu kukuibia ukamuona, mtafute umpige kipigo heavy, umvue nguo uanze kumburuta akiwa uchi hakikisha Mkono au mguu umeuvunja au kuukata iwe watu wakishuhudia, usiogope Kwenda polisi au mahabusu.
Saikolojia ya wahuni inawaogopa zaidi watu wasioogope Polisi au Jela.
Ndio maana Wahuni kamwe hawawezi kuwasumbua Wenye pesa, Wachawi, Wanajeshi, Kwa sababu watu hao maamuzi Yao wanakupiga kipigo heavy alafu mengine ndio yafuate.
Watu hao hawakushtaki Ila wewe ndio utaenda kushtaki mwenyewe au kujishtaki.
6. Vaa nguo na viatu Kama Mwanaume ambavyo muda wowote unaweza kukabiliana na hatari yoyote.
Sio unavaa nguo ambayo huwezi kurusha hata teke,
Au unavaa viatu ambavyo havikazi vizuri ukikimbizwa vinakusumbua.
7. Jifunze Self Defense.
Vibaka wengi ukienda kwenye viwanja vya mpira wanajifunza kupigana iwe ni masumbwi, karate n.k.
Mwanaume lazima ujue ngumi walau Basic.
Lazime ujue wakati WA kupigana Maeneo nyeti mfano;
1. Eneo ambalo nikimpiga mtu anapoteza Balansi na inakuwa rahisi kumshambulia, mathalani, Kwenye Bega iwe la kushoto au kulia, kwenye kidevu n.k.
Sio umpige au umsukume mtu kifuani bado mwili wake utakuwa na mhimili.
2. Eneo ambalo ukimpiga mtu unamlegeza, mfano chini ya paja nyuma ya Goti.
3. Eneo ambalo nikimpiga mtu anaumia na anaweza kuacha kupambana, mfano, Kwenye koo(hapa utajua), Kwenye macho(ulenge jicho kabisa), chembe ya Moyo, Korodani, kwenye mbavu changa n.k.
Sio unapigana tuu Kama mjinga usiyejua pakupiga, unashindwa hata na wanyama jamii ya Paka au nyoka.
8. Kama hujui mapambano, Epuka kuishi Maeneo hatari au kupita njia hatari zenye wakora.
9. Fanya mazoezi ya Pumzi na Yoga.
Hii itakufanya uwe na uwezo wa kupambana walau Lisaa limoja.
Hiyo ni kwa mtu binafsi. Kama ni kwenye jamii undeni umoja wa kina Baba WA kudhibiti uhalifu Kwa kushirikiana na serikali.
Taikon nimemaliza. Hongera Kama umefika mpaka hapa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Ukonga, DSM

Hili nilitaka kujionea Kwa macho yangu hao Panya road walivyo. Nilikuwa nikimsumbua Mara kadhaa Rafiki yangu anipeleke mahali ambapo nitawaona panya road. Basi Rafiki yangu akaniambia ipo siku atanionyesha.1. Tukio la Kwanza;

Nafikiri lilikuwa Tamasha la shika Ndinga, lilifanyika pale Uwanja wa TP Sinza, Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Paul Makonda.2. TUKIO LA PILI