Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

Imeandikwa Islamic way of..... Haijaandikwa world's way of.... Kila jamii ina njia zake...
Kama wewe ni mroho,hutakosa sababu, basi kula peke yako, wako wakristo wengi ambao huwa tunajumuika nao.
 
aaaah , je mabudha wamepewa kitabu gani na mwenyezi mungu, ikiwa wao wanaabudu sanamu ....wacha wale wenyewe kwa wenyewe, na hata wewe ukitaka kuchinja chinja na ule na familia yako...mzee ila usitoe sadaka kibudu, kwani mwenyezi mungu alishasema ninyi mna mila zenu nasi tuna zetu....
Ungesoma vizuri ukaelewa... Using jibu ulichojibu.... Kila mtu ana imani yake... Na kila mtu atahukumiwa kwa imani yake... Kwa imani yako mabudha wako hovyo na wao kwa imani yao imani yako iko hovyo..... Kilichopo hapa jamaaa juu hapo ametoa aya vyema kabisa.... Mkristu anaruhusiwa kuchinja.... Stori imekata
 
aliyepewa kitabu , maana ni yule mwenye kupewa na kuamini yaliyopo katika zaburi , injil torat na quran hivi ndivyo vitabu vitukufu.
Hivyo kwa majibu haya Kaka MKRISTU ANARUHUSIWA KUCHINJA.... Na muislam akala.... Si ndio mkuu
 
Kama wewe ni mroho,hutakosa sababu, basi kula peke yako, wako wakristo wengi ambao huwa tunajumuika nao.
Matatizo ya ukurupukaji ndio haya...... Ni wapi nimesema nnachinja, au nimechinja.... Kusema hiyo ni njia ya kiislamu sio ya kidunia nimekuwa mroho na mchoyo!!!!! Punguza ulevi wa dini.... Wanyama kibao wanachinjwa kwa mitambo na mnakula afu unakuja kuleta shudu... Kuchinja kwa machine ni njia ya kiislamu!!! ...au kidunia!!! ..
 
Ungesoma vizuri ukaelewa... Using jibu ulichojibu.... Kila mtu ana imani yake... Na kila mtu atahukumiwa kwa imani yake... Kwa imani yako mabudha wako hovyo na wao kwa imani yao imani yako iko hovyo..... Kilichopo hapa jamaaa juu hapo ametoa aya vyema kabisa.... Mkristu anaruhusiwa kuchinja.... Stori imekata
wala haujalazimishwa kwa kuwa una mila zako, baki nazo nasi twabaki na zetu,

maana visa vya namna hii viliwahi kutokea enzi za mtume(S.A.W) na chanzo cha kushushwa surat KAFIRUUN
 
Hebu tulia kwanza,kunywa maji na urelax, nimekwambia hivi dini ya kiislam haiendeshwi na google na wewe usipoteze time yako kutaka kupotosha coz hutafanikiwa, naona unakuja spidi kama umetumwa vile?!

Samahani kwa msaada zaidi unaweza kutupia aya tajwa hapo juu kutoka katika kitabu kitakatifu ili tukajua anatupoteza. Maana unaweza kupiga picha halafu tukapata kujua mbichizipi. Kama huwezi kuweka hapa kwa njia ya picha au maneno bado utakuwa hujamsahihisha
 
Ukweli upo hvi Mr cDNA, wala msile vibudu (yaan ambavyo havijachinjwa) , wala ambavyo havijachinjwa na muislam, (yaan yahud & naswaraniya na wengineo).
Lete maandiko toka ktk vyanzo vya sheria ya uislamu
 
Ni vema kufanya hivyo kutokana na ugeni wa uislamu kwa waislamu walio wengi. Ila kiuhalisia waislamu wanaruhusiwa kula kilichochinjwa na wakristu pia mayahudi kwani ktk Qur-ani ipo aya inaruhusu kula vilivyochinjwa na watu walioteremshiwa Taurati na Injili. Ila si halali kula kilichochinjwa na mshirikina hata kama ni muislamu kama wale wanaojitia kutibu kwa kutumia majini na wapiga nyota.
Pia ktk uislamu mwanamke aruhusiwa kuchinja.
wasiokuwa waislamu wanachinja kwa jina la nani?? halafu muislamu ale
 
Mna complicate maisha Sana nyie binadamu, mnashindana achinje nani alafu mnasahau dhambi ya uzinzi nyambafu kabisa
 
Kuna njia tatu za uchinjaji na katika hizo tatu moja ndo inayo tumika tz halal, hii yote ni kupunguza kiasi kikubwa cha nyama isipotee
 
Na wewe na uclever wako wote unashindwa kitu chepesi ... Toa aya inayosema mkristu asichinje..... Mbona ishu ndogo tu kama kweli imekatazwa..... Kama imekatazwa lazima Imeandikwa kwenye "kitabu cha Mungu" kutoka mbinguni
Watu wengine mnajitiamo tu na vicomment vya hovyo ili mradi tu na wewe usisahaulike kua upo humu duniani! Umeniquote comment yangu inayoelezea kitu kingine kabisaa na wewe unadai kingine kabisaa! Haya tumeshakusoma kumbe na wewe upo humu JF hongera sana, umefurahi sasa?
 
Napenda sana kufuata taratibu na kuwajali wengine .sasa nani anisaidie kumchinja kiti moto ?
 
Hawa jamaa zetu ni shida sana... Nafika ukurasa wa 6....kitu chepesi kabisa wanashindwa kujibu.... Leteni hadith, sura sijui aya inayosema mkristu haruhusiwi kuchinja wanabaki kurukaruka tu.....
Ndio maana ukajiita Mtoto wa nzi,unajijua kua unarukia rukia kila mahali na kwa vitu hovyo tu bila kueleweka!
 
Acha uongo wewe, ili nyama iwe halal ni kusomwewa jina la Mwenyezi Mungu, hata mkiristo akichinja kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu hiyo nyama inakuwa halal
jina la Allah ama Mohammedi?
 
Wakristo sio tu kwamba haturuhusiwi kuchinja, tunaweza na tunaruhusiwa kula chochote isipokua nyamafu tu. Tukiamua kuchinja wenyewe hakuna tatizo lolote kwa upande wetu, tatizo jamii zetu zimeingiliana na kuna ukaribu wa hali ya juu sana na ujirani kati ya waumini wa dini hizi mbili, sasa kwa wengine hawaruhusiwi kula kilichochinjwa bila kufuata taratibu zao, kuamua kuchinja wenyewe italeta kuwanyima ushiriki wa hao ndugu na jamaa zetu.

Tunafanya hivyo kwa kuweka maelewano tu na kujumuika, kuchinja tunaweza sana. Kama hatuwezi, mnyama nani hua anachinja?
Katika hili wakristo wanaonesha upendo hata kwa wa upande wa pili.
 
Back
Top Bottom