Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

navula wewe una google vitu vyako nd maana haujui uchungu wa dini na i swear ipo siku utaulizwa jinsi ulivyowapoteza mamia ya watu kwa upumbavu wako..au wewe ni mkristo ila unatumia ubavu huo kutuharibia dini yetu..toka mwanzo nakuona unavoandika pumba zk mi sitokoment tena nazn aya nimeiweka utaiona
 
..Na (mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu na
wanawake wema katika wale waliopewa kitabu kabla yenu, mtakapo
wapa mahari yao na kufunga nao ndoa, bila ya kufanya uzinifu au
kuwaweka kinyumba...” (5:5).
K
 
Soma Quran uelewe ndugu yangu, na huwezi kufafanua aya kwa Quran kwa kutumia hadithi. Soma hizi sura

Quran 6:38 inasema kuwa hatukuacha kitu chochote katika hiki kitabu (Quran)
6: 114: Je mnatafuta hakimu mwingine Zaidi ya Mwenyezi Mungu, hali amekuteeremshieni hiki kitabu kilichojitosheleza? Sio google nimekuwekea aya hapo soma na uelewe.
labda ngoja nikwambie kitu ,mh Mimi Quran nimekaa chini na nikasoma situmii Google mh.,Mara nyingi haya inaposhuka mtume uitolea ufafanuzi ili iweze kueleweka na ,waislam wote
 
Ndo maana twasema; mwala kibudu mnakataa. Kisicho andaliwa ipasavyo ni kufru tuu wala si vinginevyo. Nyiye hata zoga la mbwa mwala tu
Mjomba lete hiyo aya inayosema mkristu asichinje.... Umalize utata....
 
ina maana waislamu waume inaruhusiwa kuoa wale wanawake ambao walioshika kitabu i mean tofaut na uislam lakin wanamuamin mungu sasa kkwann tunasema hv kwa sababu mwanaume ni mtu mwenye nguvu ya ushawishi kivyovyote anaweza kumshawishi mkewe akawa miongoni mwa dini yake.pia zao watakalolipata litakuwa katika muongozo wa dini ya kiislamu.lakin hapo hapo tunakataa mwanamke wa kiislam kuolewa kwa sababu kama za hapo juu...
 
labda ngoja nikwambie kitu ,mh Mimi Quran nimekaa chini na nikasoma situmii Google mh.,Mara nyingi haya inaposhuka mtume uitolea ufafanuzi ili iweze kueleweka na ,waislam wote
Shusha sasa aya... Si unaisoma sana.... Lete aya inayosema mkristu asichinje... Mbona mnatumia nguvu nyiiiiiiingi kwa vitu vyepesi
 
labda ngoja nikwambie kitu ,mh Mimi Quran nimekaa chini na nikasoma situmii Google mh.,Mara nyingi haya inaposhuka mtume uitolea ufafanuzi ili iweze kueleweka na ,waislam wote
huyu jamaa nahic si miongon mwetu anataka kuwapotosha watu..kanikasirisha kweli yan alaf ni mbishi hatak kuelewa
 
Wakristo sio tu kwamba haturuhusiwi kuchinja, tunaweza na tunaruhusiwa kula chochote isipokua nyamafu tu. Tukiamua kuchinja wenyewe hakuna tatizo lolote kwa upande wetu, tatizo jamii zetu zimeingiliana na kuna ukaribu wa hali ya juu sana na ujirani kati ya waumini wa dini hizi mbili, sasa kwa wengine hawaruhusiwi kula kilichochinjwa bila kufuata taratibu zao, kuamua kuchinja wenyewe italeta kuwanyima ushiriki wa hao ndugu na jamaa zetu.

Tunafanya hivyo kwa kuweka maelewano tu na kujumuika, kuchinja tunaweza sana. Kama hatuwezi, mnyama nani hua anachinja?
Sasa kama na mimi siruhusiwe kwa imani yangu kula kilichchinjwa na huyo na tupo pamoja kwenye jamii itakuwaje? Na je hao wenzetu wanakula nyama ambazo wanyama wamechinjwa kiwandani kwa mashine?
 
Nilitaka kukurekebisha kua mwanamke haruhusiwi, wewe unasema anaruhusiwa!! Acha kupotosha wewe unajiandikia tu vitu usivyovijua,eti umeweka hiyo aya yako ya google,uislamu hauendeshwi kwa google acha kukariri maisha,

Hivi unawajua wamiliki wa google? Hivi unajua kua si kila kilichopo google ni accurate? Tuliza mzuka acha kujifanya mjuaji na kujifanya unaijua dini ya watu kuliko wenyewe, najua lengo lako kuu ni Kupotosha but huwezi kupotosha hii dini wenzako walishajaribu na wakashindwa.
Hawa jamaa zetu ni shida sana... Nafika ukurasa wa 6....kitu chepesi kabisa wanashindwa kujibu.... Leteni hadith, sura sijui aya inayosema mkristu haruhusiwi kuchinja wanabaki kurukaruka tu.....
 
naheshimu swala la dini maana kila mtu anahaki ya kuabudu atakavyo. sasa ndugu kingereza unakielewa vizuri?? wapi hapo kwenye hiyo aya imeruhusu waislam kula kisichochinjwa na muislam?
Waambie waislam walete aya inayomzuia mkristu kuchinja....
 
Shusha sasa aya... Si unaisoma sana.... Lete aya inayosema mkristu asichinje... Mbona mnatumia nguvu nyiiiiiiingi kwa vitu vyepesi
Hakuna Jamii isiyo ruhusiwa ,ila je mnachinja kwa jina la mungu yupi? kama mtachinja kwa jina la mwenyezi mungu hewara.
 
MKUU,HUYO AMEKIMBILIA KUCOPY GOOGLE NA KUPASTE HAPA,WALA HATA HAKUSOMA KILICHOANDIKWA, KUNA MKUU AMEMFAHAMISHA KWENYE POST #49 LAKINI KAJIFANYA HAJAIONA.!!
Na wewe na uclever wako wote unashindwa kitu chepesi ... Toa aya inayosema mkristu asichinje..... Mbona ishu ndogo tu kama kweli imekatazwa..... Kama imekatazwa lazima Imeandikwa kwenye "kitabu cha Mungu" kutoka mbinguni
 
Waambie waislam walete aya inayomzuia mkristu kuchinja....
“Basi kuleni katika wale waliosemewa jina la Allaah, ikiwa nyinyi mnaziamini aya zake” (6: 118). aya hii inazungumzia waliopewa kitabu wale wenye kuamini , swali je kwa sasa waliopo wanaamini? Allah na kitabu vyake hasa qurani? kama una aamin na ukachinja kwa jina la mwenyezi mungu ni ruhusa kwa muislam kula na kuchinja pia kwako, ila kama sio unakula kibudu kaka
 
Hakuna Jamii isiyo ruhusiwa ,ila je mnachinja kwa jina la mungu yupi? kama mtachinja kwa jina la mwenyezi mungu hewara.
Kwa hiyo BUDHHA NAO WACHINJE KWA JINA LA MUNGU WA WAISLAMU!!! WAHINDU NAO!!! DINI SIO UKRISTU NA UISLAMU TU.... MSIKARIRI... ETI MUNGU YUPI.... MIMI SITAKI HAYO MAELEZO YAKO.... NATAKA AYA NIKASOME MWENYEWE MAANA KUR'AN NIMEISOMA.... KWETU WAISLAMU WAKO WA4 WAKRISTU TUPO WA 4 NA DINGI ALIMUACHA KILA MTU AAMUE DINI YAKE.... Hivyo naomba aya mkuu....
 
Ukweli upo hvi Mr cDNA, wala msile vibudu (yaan ambavyo havijachinjwa) , wala ambavyo havijachinjwa na muislam, (yaan yahud & naswaraniya na wengineo).
“Basi kuleni katika wale waliosemewa jina la Allaah, ikiwa nyinyi mnaziamini aya zake” (6: 118). aya hii inazungumzia waliopewa kitabu wale wenye kuamini , swali je kwa sasa waliopo wanaamini? Allah na kitabu vyake hasa qurani? kama una aamin na ukachinja kwa jina la mwenyezi mungu ni ruhusa kwa muislam kula na kuchinja pia kwako, ila kama sio unakula kibudu kaka
1)muamini ni nani
2) aliyepewa kitabu ana sifa gani
 
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetuMtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhiwa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya MwishoUislamu umehalalisha kila lililo zuri na ALLAAHسبحانه وتعالىhakubali ila zuri katika kila jambo. Jambo ambalo limehalalishwa na Allaahسبحانه وتعالىau Mtume Wakeصلى الله عليه وآله وسلمbasi linakuwa na maslahi kwetu na lililoharamishwa linakuwa ni lenye madhara. Mwanadamu anapofanya ovu anasema kuwa tumeamrishwa hilo na Allaahسبحانه وتعالى, lakini Allaahسبحانه وتعالىyuko mbali na jambo hilo. Allaahسبحانه وتعالىAnasema:{{وَإِذَا فَعَلُواْ فَاحِشَةً قَالُواْ وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءنَاوَاللّهُ أَمَرَنَا بِهَا قُلْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءأَتَقُولُونَ عَلَى اللّهِ مَا لاَ تَعْلَمُون}}{{“Na wanapofanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo babu zetu, na Allaah ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Allah haamrishi mambo machafu. Mnamzulia Allah msiyoyajua}}Al-A'araaf: 28Na Allaahسبحانه وتعالىanatueleza kwamba hakuharamisha isipokuwa yaliyo machafu na sio yale mazuri.Anasema:{{قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللّهِ الَّتِيَ أَخْرَجَ لِعِبَادِهِوَالْطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ قُلْ هِي لِلَّذِينَ آمَنُواْ فِيالْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ كَذَلِكَ نُفَصِّلُالآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ}}{{قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَابَطَنَ وَالإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُواْبِاللّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُواْ عَلَىاللّهِ مَا لاَ تَعْلَمُونَ}}{{Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Allah alilowatolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua}}.{{Sema: Mola wangu ameharamisha mambo machafu ya dhahiri na ya siri, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Allah naasichokiletea uthibitisho, na kumzulia Allah msiyoyajua}}Al-A'araaf 32 – 33 .Na katika Hadiyth ni ile iliyopokea kwa AbuHurayrahرضي الله عنهkwamba Mtume wa Allaahصلى الله عليه وآله وسلمamesema🙁(Hakika Allaahسبحانه وتعالىni Mzurina Hakubali ila zuri. Na hakika Allaahسبحانه وتعالىamewaamrisha Waislamu yale aliyowaamrisha Mitume. Akasema Allaahسبحانه وتعالى‘Enyi Mitume! Kuleni vizuri na fanyeni mema’(23: 51). Na akasema tena Allah Aliyetukuka:‘Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyowaruzuku(2: 172)))[Muslim].Kwa aya na Hadithi zinatutaka sisi tule vilivyo vizuri na hiyo ni kwa maslahi yetu wenyewe. Na miongoni mwa vilivyo vizuri vyaAhlul Kitaab(waliopewa Kitabu). Allah anasema:{{الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلُّ لَّهُمْ}}{{Leo mhelalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao}}Al- Maaidah :5Inatakiwa tuelewe kuwa aya zinazoteremshwa na Allaahسبحانه وتعالىni kwa ajili ya kutekelezwa na Waislamu wa zama zote na kila sehemu katika hii dunia. Hebu tuangalie Mufasirinawa Qur’ani wanatueleza vipi katika suala hili.Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na Muislamu au myahudi au Mnasara (Mkristo), kwa sharti ile ya kuchinja – sio kuwanyonga. Ama wasiokuwa hawa hakiwi halali wanachokichinja. Ama chakula kisichokuwa cha kuchinja ni halali kwa Muislamu kukila hata kikitengenezwa na makafiri, kwa madhehebu ya Kisuni maadamu:- Hujaona kuwa kimeingia najisi- Si katika vile vyakula vilivyokatazwa naUislamuWafasiri wanachambua:“Vyakula vyaAhlul Kitaab” inajumlisha wanyama wanaochinjwa na wao.“Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu”ina maana ya kuwa hakuna vikwazo kwetu au kwao kula chakula pamoja. Waislamu wanaruhusiwa kula chakula pamoja naAhlul Kitaabna wao piakula na Waislamu. Lakini kukaririwa kwa sentensi “vilivyo vizuri na safi” ni muhimu sana. Hii inamaanisha kuwa Waislamu hawafai kula vyakula vyao, ikiwaAhlul Kitaabhawatachunga kanuni muhimu kwa muono wa Uislamu au wakachanganya vitu katika vyakula na vinywaji ambavyo si halali. Kwa mfano, ikiwa hawatataja jina la Allaahسبحانه وتعالىjuu ya mnyama wanaomchinja, nyama hiyo itakuwa haramu kwa waislamu. Hivyo hivyo, ikiwa pombe au nyama ya nguruwe au kitu chochote haramu kitaandaliwa, Waislamu hawataruhusiwa kukaa meza moja na wao.Kanuni hiyo hiyo ndiyo inayotumika kwa vyakula na vinywaji vya wasiokuwa Waislamu isipokuwa Waislamu hawafai kula nyama ya wanyama waliochinjwa na wasiokuwa Waislamu (wasiokuwaAhlul Kitaab). ""Maana ya ayah ii kwa ufupi ni kuwa kuanzia siku hii ya leo vyote vilivyo vizuri na safi vinaruhusiwa kwenu, Waislamu. Kwa vile Allaahسبحانه وتعالىhakukataza, vyakula vya Mayahudi na Manasara inaruhusiwa kwa msingi wa ile ruhusa ya asli ya kukubaliwa. Kwa hivyo mnaweza kula nyama ya wanyama waliochinjwa au kuwindwa, nao wanaweza kula mliochinja au kuwinda. Japokuwa Uislamu unachukua msimamo mkali kwa washirikina, unakua laini kwa wale waliopewa Kitabu kwani wao wako karibu na Waislamu katika itikadi zao kuhusu wahyi, utume na misingi mingine ya Dini. Uislamu unaturuhusu kula nao, kuoa wanawake wao na kwa jumla kuwa na mahusiano ya kijamii na wao. Matumizi ya kauli, “Vyakula vyaAhlul Kitaabni halali kwenu” kwa ujumla wake inajumlisha nyama, mazao na vyakula vyengine. Vyote hivi ni halali kwetu sisi isipokuwa vile vilivyo haramu kwa mfano nyama ya nguruwe, mzoga, damu inayo tiririka, kwanihizi ni haramu bila kujali ikiwa vinatoka kwa Mnaswara, Myahudi au Muislamu. Ikiwa mtu hatomsikia Mnasara au Myahudiakitaja jina lisilokuwa la Allaahسبحانه وتعالىkama kutaja jina la Yesu au mtawa Fulani wakati wa kuchinja mnyama,nyama anayopatiwa ni halali. Lakini ikiwa atataja jina lisilokuwa la Allaahسبحانه وتعالىbasi itakuwa haramu, kulingana na baadhi ya mafakihi ambao wanaosema kuwa hiyo inaingia katika fungu la vile vinavyotolewa kwa asiyekuwa Allaahسبحانه وتعالىilhali wengine wanasema kuwa vyakula vya waliopewa Vitabu vinaruhusiwa kwetu na Allaahسبحانه وتعالىambaye ni mjuzi kwa wanayosema wakati wa kuchinja."Allah ametaja alivyoviharamisha kwa Waumini katika vilivyo vichafu na kuhalalisha vizuri. Kisha akataja hukmu ya waliochinjwa naAhlul Kitaabakasema:“Nachakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu”. Amesema Ibn ‘Abbaas, Abu Umamah, Mujaahid, Sa‘iyd bin Jubayr, ‘Ikrimah, ‘Atwaa’, al-Hasan, Makhuul, Ibraahim an-Nakha‘i, Muqaatil bin Hayyaan: Yaani waliochinja, na hili jambo wamekubaliana wanazuoni kuwa wanyamawanaochinja ni halali kwa waislamu kwani wao wanaitakidi kuwa ni haramu kuchinja kwa asiyekuwa Allaahسبحانه وتعالىna hawataji katika kuchinja isipokuwa jina la Allaahسبحانه وتعالىjapokuwa waowanazo itikadi nyingine ambazo haziendi sambamba na utukufu wa Allaahسبحانهوتعالى. Wanavyuoni wa Kihanafi, Shafi‘i na Hanbali wanaruhusu kuliwa kwa sehemu za mnyama aliyechinjwa na Myahudi japokuwa kwao ni haramu kama mafuta na wametoa dalili ya Hadithi ya ‘Abdullah bin Mughaffalرضي الله عنهwakati alipochukua kiriba cha mafuta kilichotupwa na Myahudi katika Vita vya Khaybar (Sahiih). Na dalili nyingine ni ile Hadithi inayotueleza baada ya vita vya Khaybar mwanamke wa Kiyahudi kwa jina Zaynab alimchomea Mtumeصلى الله عليه وآله وسلمpaja la kondoo na kulitiasumu naye akala na katika kula Sahaba mmoja, Bishr bin al-Bara’ bin Ma‘rurرضي الله عنهaliaga dunia kwa sumu hiyo baada ya kula (Ibn Kathiir,Tafsiirul Qur’aanil Adhiim, Mjalada wa pili).Kwa muhtasari kutoka kwa yale tuliyoyanukuu tunaona ya kwamba:1.Wanyama wote wa halali wanaochinjwa na Ahlul-Kitaab wamehalalishwa kwa Waislamu isipokuwa inapojulikana kwa uwazi kuwa wamechinjwa kwa njia ambayo haikubaliki katika Uislamu. Lakini katika hilo haifai kuchunguza na kudadisi dadisi kuona wanavyofanya.
 
Kwa hiyo BUDHHA NAO WACHINJE KWA JINA LA MUNGU WA WAISLAMU!!! WAHINDU NAO!!! DINI SIO UKRISTU NA UISLAMU TU.... MSIKARIRI... ETI MUNGU YUPI.... MIMI SITAKI HAYO MAELEZO YAKO.... NATAKA AYA NIKASOME MWENYEWE MAANA KUR'AN NIMEISOMA.... KWETU WAISLAMU WAKO WA4 WAKRISTU TUPO WA 4 NA DINGI ALIMUACHA KILA MTU AAMUE DINI YAKE.... Hivyo naomba aya mkuu....
aaaah , je mabudha wamepewa kitabu gani na mwenyezi mungu, ikiwa wao wanaabudu sanamu ....wacha wale wenyewe kwa wenyewe, na hata wewe ukitaka kuchinja chinja na ule na familia yako...mzee ila usitoe sadaka kibudu, kwani mwenyezi mungu alishasema ninyi mna mila zenu nasi tuna zetu....
 
Back
Top Bottom