Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

sisi hapa kijijini waislam karibu hawapo kabisa....tunachinja wenyewe....ila ikitokea wametembelea wanachinja wao....si wakichinja tunapiga kama kawaida...tukichinja sisi wao hawali!! thats why wanaachiwa wachinje!!!!
 
wasiokuwa waislamu wanachinja kwa jina la nani?? halafu muislamu ale
Naam ndugu yangu mpendwa...niliweka link ili watu wasome ufafanuzi kadhia hiyo lakini nasikitika hawakuisoma...nitakujibu kwa kuongezea maelezo ktk post niliyoweka aya inayoruhusu. Haya ni mambo ya kisheria hayahitaji misuli tutaelewana tu rafiki.
 
Ukristo hauonyeshi ninamnagani mnyama anatakiwa kuchinjwa,ndio maana utakuta mnyama anapigwa marungu,mshale,shoka na hata risasi.
zipo method nyingi za uchinjaji ikiwemo na hiyo alah method, na zote kitaharam zinakubalika .usipotoshe watu kwa interest zako za dini.
 
Watu kama nyie ni wa muhim sana katika hii jamii ya sasa, nahisi mtakuwa wachache sana, hongera sana mkuu kwa jibu zuri

Ahsante, lakini kila mmoja wetu ana umuhimu wake na tunategemeana. Ni kweli, tumelelewa hivyo nyumbani toka wadogo kabisa, tukitaka kuchinja chochote iwe kuku, mbuzi au mfugo wowote lazima tutatafuta anaestahili kuchinja ili tusiwakwaze wengine.
 
Mkuu umenena vyema, waislamu wengi hatusomi Quran tunaishia kufata upotoshaji wa mashehe walio wengi. Ukiosisoma aya zifuatazo utajua kwamba kitu chochote ambacho utatamka jina la Mwenyezi Mungu kabla ya kula kinakuwa halali kwako, isipokuwa vile ambavyo Mwenyezi Mungu ameviharamisha katika aya ya 2:173 kama ulivyoionyesha hapo juu.

Mwenyezi Mungu anasema katika Quran 6:119: Na kwa nini msile katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, nayeamekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo
lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu.
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua wanao pindukia mipaka.

English version : Why should you not eat from that upon which God's name has been mentioned ? He has detailed for you what is prohibited for you, unless you are forced. Indeed, many people mislead others with their personal opinions, without knowledge. Your Lord is fully aware of the transgressors." 6:119

You shall eat from that upon which God's name has been pronounced, if you truly believe in His revelation." 6:118

Mtu yeyote ambaye ataharamisha ambavyo Mwenyezi Mungu hakuharamisha basi huyo anatenda dhambi.
Quran 6:116. Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi
haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi
Mungu hawatafanikiwa.

Ndio maana tunaaminishwa kwamba kufuga mbwa ni haramu kitu ambacho sio kweli. Ukisoma Quran Sura ya 18:13: Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana
walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu. Hii aya inasimulia wale vijana wa pangoni ambao Mwenyezi Mungu aliwataja kama waja wema . Ukisoma zaidi Quran utagundua kwamba walikuwa na mbwa wao pale pangoni. Kama mbwa angekuwa haramu basi Mungu asingewataja kama waja wema.

Quran 18:18: Nawe utawadhania wamacho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na
kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeli
watokea hapana shaka ungeli geuka kuwakimbia, nawe umejaa khofu.

Pia Mwenyezi Mungu anasema tunaruhusiwa kula ambavyo mbwa tuliowafunza kwa ajili ya kuwinda wamevikamata .
Quran 5.4: Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na
mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Mwenyezi
Mungu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na
mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.


Tatizo tunasoma Quran kama kasuku, tunakaririshwa kwa kiarabu bila kujua maana yake. Yaani unakaririshwa Sura baada ya Sura na kumeza zote bila kujua maana. Kama Quran imeshushwa kama muongozo kwa waislamu, kwa nini tusiisome na kuielewa. Kukariri Quran bila kujua maana yake kuna tofauti gani na mtu ambaye hajaikariri kabisa?

Quran haisomwi kama hadidhi, hizo sura huwa haziongelea kitu kimoja , unaweza kukuta jambo moja liko kwenye aya tofauti tofauti, ili kujua maana kamili ni lazima utulize kichwa ilikuweze kuziunganisha na kupata maana na ujumbe kutoka kwa Mungu

Asante
Heri yako Mkuu, unaongea kwa hoja si kwa kukariri. Natamani wangekuiga kutoa hoja kisomi hivyo. Kongole!!!!
 
Mimi binafsi siwezi kuchinja, nawasifu wote waliojariwa moyo huu, mimi kama ni kuku nikienda kunuwa narudi naye nyumbani ameshatengezwa kabisa kama ni kuweka kwenye friji au kuingizwa jikoni.

Kama ni mbuzi ni vyema kuwashirikizha hawa wenzetu maana tatizo walilonalo ni la kurithi kutoka kwa Founder wao Muhammad.
hupo sawa mkuu.wengine wanapenda damu sana
 
Maa'ida: 5

"This day are (all) things Good and pure made lawful unto you. The food of the People of the Book is lawful unto you and yours is lawful unto them. (Lawful unto you in marriage) are (not only) chaste women who are believers, but chaste women among the People of the Book, revealed before your time, when you give them their due dowers, and desire chastity, not lewdness, nor secret intrigues…"

Kwa ufafanuzi zaidi wa kadhia hiyo rejea: Fatawa Islamiyya, Sheikh Abdel-Aziz Bin Baz, 3/404.

Uliyetaka aya umeelewa??
 
Mi nadhani wanaruhusiwa kuchinja, ila ili kujenga mahusiano mema ya kijamii huwaalika ndg zao wa kiislam...
Yeye anakualija nini?
Wauzaji wa kuku wanaochinja wote ni waislamu?
Anaeona akichinja mbuzi wake bila mwislam hachinjiki na akamualike.
 
Mimi nimeishi katika jumuiya ya watu mbalimbali na wa dini zote.

Cha kushangaza inapofika sikukuu au wamenunua jogoo basi watu hutafutwa kwa ajili ya kuchinja, japokuwa wanaume wapo.

Nimekula sana shingo mchuzi hata vibawa kwa kazi hiyo. Ndio nauliza; Je, kuna madhehebu ya wakristo wanakataza kuchinja?
Nasikitika kwanza umekaa na dini zote umeshindwa kugundua hekima waliyokuwa nayo Wakristo, ndugu ile amri ya mpende jirani yako kuliko nafsi yako hapo ndipo inapotekelezwa na mambo mengi tunayofanya wakristo kwa ajili ya jirani zetu

Huku tunafundishwa upendo Maana vita vyetu si vya damu na nyama Bali ni vya roho Ahsante
 
wasiokuwa waislamu wanachinja kwa jina la nani?? halafu muislamu ale

Maa'ida: 5

This day are (all) things Good and pure made lawful unto you. The food of the People of the Book is lawful unto you and yours is lawful unto them. (Lawful unto you in marriage) are (not only) chaste women who are believers, but chaste women among the People of the Book, revealed before your time, when you give them their due dowers, and desire chastity, not lewdness, nor secret intrigues…

The preceding discussion is in regards to the general ruling with respect to slaughtered meat of the People of the Book; as for the specifics, the slaughtered meat of People of the Book can be one of several cases:

That he slaughters it via the known way specified by shari'ah and he speaks the name of Allah upon it. In this case there is no problem in the permissibility of eating it.

That he does not slaughter it by the way specified by shari'ah as is the case if hechokes it or electrocutes it until it dies or drowns it in water until it dies or kills it by a bullet, etc. In this case there is no doubt that eating it is forbidden since it is maita (meat of an animal that has died without properly being slaughtered) and Allah has forbidden it in the Qur'an (interpretation of the meaning): "… and forbidden unto you is maita…" (al-Maa'ida:3)

That he mentions the name of someone or something other than Allah upon it as he is slaughtering, such as the Messiah or otherwise. Likewise there is no doubt that the meat in this case is haraam, since it is among what has been dedicated to other than Allah, which is specifically forbidden in the ayah in surat al-Maa'ida: 3 (interpretation of the meaning): "Forbidden to you (for food) are: maita, blood, the flesh of swine, and that on which has ben invoked the name of other than Allah; that which has been killed by strangling or by a violent blow…"

That we receive their meat and we don't know if it has been slaughtered properly or not. In this case the rule of thumb is that if we don't know the way of slaughter, the default is that it is permitted if it has been slaughtered by Muslims or Ahl il-Kitaab (Fatawa Islamiyya, Sheikh Abdel-Aziz Bin Baz, 3/404), as per the generally encompassing ayah (interpretation of the meaning) "and the food of the people to whom have been revealed the Book is permitted for you." (al-Maa'ida:5) If it becomes evident to us that they have not slaughtered it properly then it would not be permisible.

That we receive their meat and we don't know what they have mentioned upon it, and in this case likewise the preferrable and recommended opinion is the permissibility of eating it, as per the hadith in Sahih al-Bukhari via Aa'isha (may Allah be pleased with her) that some people said to the Prophet (peace be upon him) that a people come to them with meat which they do not know whether they have mentioned the name of Allah upon it or not. The Prophet replied "Mention the name of Allah upon it and eat it."
 
Naweza sema wengine katika wakristo wanaamini kuwa ni musilamu ndio anayechinja (halali) sababu ya kusema hivyo ni kuwa hapa nyumbani jirani zetu ni wakristo lkn kila wakitaka kuchinja ni lazima watuite sisi,na kuna siku mmoja wao alichinja mwenyewe mbuzi lkn amini nyama ile waligoma kuila na mmoja wa familia ile anaitwa Wema aliniambia mm nyama akichinja mkristo mwenzangu siwezi kula .nikamuuliza kwa nini?akasema moyo wangu tu unakataa kula nyama ilichinjwa na mkristo.nikabaki na mshangao tu

WEMA?
 
Sisi wakristu tukibishana kuhusu dini yetu hutumia vifungu vya biblia, na kuruani imeandikwa lunga ngeni, ni ngumu wao waislamu kujua mengi waliyofundishwa zaidi ya kusikiliza masheikh, hata kama wameruhusiwa kuchicha hawawezi jua, sababu biblia imeandikwa kiswahili ila wengi hawaielewi sembuse kuran iliyoandikwa kiarabu, nimeandika kistaarabu kwa sababu hamkawii kuwaka, msije mkaitoa roho yangu.
 
Sisi wakristu tukibishana kuhusu dini yetu hutumia vifungu vya biblia, na kuruani imeandikwa lunga ngeni, ni ngumu wao waislamu kujua mengi waliyofundishwa zaidi ya kusikiliza masheikh, hata kama wameruhusiwa kuchicha hawawezi jua, sababu biblia imeandikwa kiswahili ila wengi hawaielewi sembuse kuran iliyoandikwa kiarabu, nimeandika kistaarabu kwa sababu hamkawii kuwaka, msije mkaitoa roho yangu.
Kiswahili kinakushinda je wataweza Kiarabu. !! Usizungumze kama hujafanya uchunguzi wa kina!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom