Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,157
115,690
Wanabodi,

Leo ni sikukuu ya Eid El Haji, Iddi ya Kuchinja.

Leo ni siku ya Sikukuu ya Idd El Haj, ni iddi ya kuchinja, asubuhi nilikuwa naangalia matangazo ya mubashara ya Baraza la Iddi kupitia TBC, kutoka Msikiti wa Mfalme Mohammed VI wa Morroco, Bwakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kumbe Msikiti Mkuu wa Bakwata, sasa umebadilishwa jina!, na kupewa jina la Mfalme wa Morroco!

Mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye amesilimishwa na kupewa jina la Aboubakar Chalamila!, na mawaziri akiwemo Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa. Baadhi ya watu maarufu niliowaona ni pamoja na Alhaj Sheikh Ali Nguruko, Alhaj Chande, Idda Azan, Shaweji Abdalah, Salum Mwalimu, Juma Simba Gadafi, Salum Abladaha "TRY Again", Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mruma, Kadhi wa Dar es Salaam, Shamin Khan, mwenyekiti wa JUAKITA, pia kulikuwa na mabalozi wa Balozi wa Moroko, na wa Comoro.

Katika salam zake, Sheikh Aboubakar Chalamila alisema utulivu wa jiji la Dar es Salaam, unawategemea sana viongozi wa Dini.

Salaam za Waislamu, zimetolewa na Alhaj Sheikh Nuru Mruma, Katibu Mkuu wa Bakwata ambaye amewasisitiza Waislamu kudumisha amani na kuilinda amani. Wazazi watakiwa kulea watoto wao kwa tabia njema, kujenga taifa la kizazi cha watu wema ambao hawatapokea rushwa wala kufanya ufisadi.

Amesema kupanda miti na utunzaji wa mazingira ni ibada muhimu kwa Waismamu wote.

Pia amewataka Waislamu kujitokeza kwa wingi, kujiandikisha kwenye uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura na wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Salaam za Mufti, zimetolewa na Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata. Aamezungumzia Watanzania tutafakari, sadaka ya kuchinja siku ya Iddi El Haj, ni iddi ya kuchinja. Zamani ilikuwa sio kuchinja tuu wanyama, bali walichinja hata binadamu ana akatolea mfano Sadaka ya Nabii Ibrahim kutaka kumtoa mwanae Ismail, kwa sadaka ya kuchinja.

Hakuna ubishi kuhusu Wakristo na Waislamu, kuwa ni watoto wa Baba mmoja, Nabii Ibrahim hivyo huu ni uthibitisho wa Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu Mmoja, na sheria za dini hizi zote mbili Wakristu na Waislamu, ni sheria moja ile ile ya Musa, ila kuna watu wanafundishwa ukweli na kuna watu wanadanganywa!.

Hakuna ubishi kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail aliyezaa na mjakazi wa Kimisri, Hagir, na Isaka ni mtoto wa pili wa Ibrahim, aliyemzaa na mkewe Sarah.

Hakuna ubishi Ibrahim alitaka kumtoa mtoto wake Sadaka ya kuchinja.

Waislamu na Kitabu chao Kitukufu cha Quran Tukufu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Ismail. Wakristo na Kitabu chao Kitakatifu cha Biblia Takatifu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Isaka.

Je, ukweli halisi ni upi? Hii maana yake. Kama tukio la Ibrahim kutaka kumchinja mwanae kumtoa sadaka ni tukio moja, then

1. Hii maana yake ni kuna watu wanadanganywa, haiwezekani kwa Waislamu mtoto huyo awe ni Ismail na kwa Wakristu mtoto huyo awe ni Isaka, hii maana yake kuna kitabu hapo kinasema kweli na kuna kitabu kinasema uongo!, jee ukweli ni upi?

Umuhimu wa kuujua ukweli huu, unakupa fursa ya kujua ukweli ni upi, hivyo ufuate mafundisho yapi ambayo ndio mafundisho ya kweli!

Bandiko hili linakutaka kwanza uwe open minded, kama wewe ni mfia dini, unaamini dini yako ni ya ukweli mtupu, bandiko hili halikufai.

Pili unatakiwa uwe na ngozi ngumu ya kuukubali ukweli halisi hata uwe mchungu vipi!, ikitokea ni dini yako unayoiamini kuwa ni dini ya kweli, kumbe ni dini ya uongo, uwe na uwezo wa kustahimili maana.

Nawatakia Waislamu wote,
Iddi Mubarak njema ya kuchinja.

Paskal
 
Wanabodi,
Leo ni sikukuu ya Eid El Haji, Iddi ya Kuchinja.

Leo ni siku ya Sikukuu ya Idd El Haj, ni iddi ya kuchinja, asubuhi nilikuwa naangalia matangazo ya mubashara ya Baraza la Iddi kupitia TBC, kutoka Msikiti wa Mfalme Mohammed VI wa Morroco, Bwakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kumbe Msikiti Mkuu wa Bakwata, sasa umebadilishwa jina!, na kupewa jina la Mfalme wa Morroco!.

Mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye amesilimishwa na kupewa jina la Aboubakar Chalamila!, na mawaziri akiwemo Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa. Baadhi ya watu maarufu niliowaona ni pamoja na Alhaj Sheikh Ali Nguruko, Alhaj Chande, Idda Azan, Shaweji Abdalah, Salum Mwalimu, Juma Simba Gadafi, Salum Abladaha "TRY Again", Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mruma, Kadhi wa Dar es Salaam, Shamin Khan, mwenyekiti wa JUAKITA, pia kulikuwa na mabalozi wa Balozi wa Moroko, na wa Comoro.

Katika salam zake, Sheikh Aboubakar Chalamila alisema utulivu wa jiji la Dar es Salaam, unawategemea sana viongozi wa Dini.

Salaam za Waislamu, zimetolewa na Alhaj Sheikh Nuru Mruma, Katibu Mkuu wa Bakwata ambaye amewasisitiza Waislamu kudumisha amani na kuilinda amani. Wazazi watakiwa kulea watoto wao kwa tabia njema, kujenga taifa la kizazi cha watu wema ambao hawatapokea rushwa wala kufanya ufisadi.

Amesema kupanda miti na utunzaji wa mazingira ni ibada muhimu kwa Waismamu wote.

Pia amewataka Waislamu kujitokeza kwa wingi, kujiandikisha kwenye uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
na wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Salaam za Mufti, zimetolewa na Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata. Aamezungumzia Watanzania tutafakari, sadaka ya kuchinja siku ya Iddi El Haj, ni iddi ya kuchinja. Zamani ilikuwa sio kuchinja tuu wanyama, bali walichinja hata binadamu ana akatolea mfano Sadaka ya Nabii Ibrahim kutaka kumtoa mwanae Ismail, kwa sadaka ya kuchinja.

Hakuna ubishi kuhusu Wakristo na Waislamu, kuwa ni watoto wa Baba mmoja, Nabii Ibrahim hivyo huu ni uthibitisho wa Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu Mmoja, ila kuna watu wanafundishwa ukweli na kuna watu wanadanganywa!.

Hakuna ubishi kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail aliyezaa na mjakazi wa Kimisri, Hagir, na Isaka ni mtoto wa pili wa Ibrahim, aliyemzaa na mkewe Sarah.

Hakuna ubishi Ibrahim alitaka kumtoa mtoto wake Sadaka ya kuchinja.

Waislamu na Kitabu chao Kitukufu cha Quran Tukufu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Ismail.
Wakristo na Kitabu chao Kitakatifu cha Biblia Takatifu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Isaka.

Jee ukweli halisi ni upi?.
Hii maana yake, kuna watu wanadanganywa, haiwezi huku awe huyu na kule awe yule!.
Umuhimu wa kuujua ukweli huu, unakupa fursa ya kujua ukweli ni upi, hivyo ufuate mafundisho yapi ndio ya kweli?..

Nawatakia Waislamu wote,
Iddi Mubarak.

Paskal
Ujuwe tu kuwa Quran ina miaka 1400 wakati Bibilia ina miaka zaidi ya 2000. Hapo utagundua ni nani kakopi kwa nani?

Halafu kuna watu wanadanganywa eti Mtume wao aliteremshiwa kitabu. Uwongo mtupu
 
No siwachokonoi ila kuna wanaofundishwa mafundisho ya ukweli na kuna wanao danganywa!. Lengo hapa ni kuutafuta ukweli ili tusiendelee Kudanganywa!.
P
Uongo unaaminika kirahisi kuliko UKWELI.

Wanaamini INJILI na INJILI zote zimeandikwa juu ya Kuzaliwa, kufa na kufufuka Kwa Yesu,

Lakini Hadi Leo sie tunaonekana ndio waongo.

Sasa hiyo KAZI unayoifanya ni ngumu mno.
 
Ujuwe tu kuwa Quran ina miaka 1400 wakati Bibilia ina miaka zaidi ya 2000. Hapo utagundua ni nani kakopi kwa nani?

Halafu kuna watu wanadanganywa eti Mtume wao aliteremshiwa kitabu. Uwongo mtupu
Kitu muhimu ni tuutafute ukweli, Mungu hakuleta dini wale Yesu hakuleta dini!. Hoja hapa ni nani mkweli na nani muongo?. Mtoto aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni nani?.
P
 
Naona unawachokonoa walioamua kuchukua BIBLIA na kuzifanyia editing na kuongeza wayatakayo yawafurahishe.
Tofautisha kutafsiri kwa lugha ya eneo husika na editing. Ni upuuzi kukaririsha watu kusoma kitabu kwa lugha moja ya kiarabu wakati watu wana lugha zao.

Ndiyo maana mnaambiwa mpigane ili kumtetea Allah wakati Wakristu wanaambiwa Mungu atawapigania na kuwatetea.

Kuna sababu kweli ya kuupigania Uislamu ili ukapate mabikra 72? Yaani huko peponi cha maana ni mabikra tu? Umeishi duniani mabikra hujawahi hata kuwatongoza kisha utegemee wa peponi.

Je wanawake wanaotetea Allah nao watakutana na na marijali wangapi ambao hawajawahi kuto-mba?
 
Uongo unaaminika kirahisi kuliko UKWELI.

Wanaamini INJILI na INJILI zote zimeandikwa juu ya Kuzaliwa, kufa na kufufuka Kwa Yesu,

Lakini Hadi Leo sie tunaonekana ndio waongo.

Sasa hiyo KAZI unayoifanya ni ngumu mno.
Mambo ya Nabii Ibrahim ni Agano la kale, Bible Takatifu na Quran Tukufu is the same ila kuna upande wanadanganywa!.
P
 
Waislam na Wakristo wote wanakubaliana kuwa Kaburi la Ibrahim, Sarah, Rebekah na watoto wengine wa Isaka yako Hebron, katika msikiti unaitwa Masjid Al Ibrahimi ambao nusu ni Sinagoni na Nusu ni msikiti.

Lakini Waislam na Wanazuoni wa Kiislam hawajawahi kuja na Uthibitisho ni namna Gani Ibrahim alifikaje Mecca ya Leo na ilikuwaje akafia Kaanani/Israel ya Leo.

Kumbuka Hajiri alikuwa Mmsiri na Ibrahim alimfukuza Hajiri baadae kutokana na migogoro ya kifamilia.

Kulingana na Tamaduni za Kiyahudi Jiwe lililomo ndani ya Dome of the Rock au ule msikiti wenye paa la Dhahabu Ndio Ibrahim alitoka kumtoa Sadaka Isaka, kutoka yalipo makaburi ya Ibrahim na ilipo Yerusalem hoja hii ina mashiko zaidi ya Hoja ya Waislam

1000017224.png
 
Mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye amesilimishwa na kupewa jina la Aboubakar Chalamila!, na mawaziri akiwemo Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Kama kweli amesilimu ni jambo la heri sana.
 
Back
Top Bottom