Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Jamani kweli wanatufanya wapumbavu,
Hivi video ile anayoshindwa kunyanyuka kwenye kiti kuna slow motion gani pale???
Kwanza kabla ya kunyanyuka mwangalie uso unavyomshuka na kuchanganyikiwa huku akihisi kizunguzungu
 
Mkuu, napingana na wewe kuhusu hilo. Hata kama haijaandikwa, afya ni kigezo muhimu. Pengine muhimu kuliko vyote. Ni kazi ganui siku hizi mtu anaingia bila kupima afya? Kutegemeana na kazi, kuna magonjwa hayakubaliki katika kazi fulani fulani.

Afya ya kiongozi mtarajiwa ni suala nyeti sana. Tumeyaona ya akina, Michael Sata, Levi Mwanawasa, Bingu wa Mutharika na Yardua kule Nigeria. Yardua alikuwa mahututi siku nyingi Nigeria ikabaki inaongozwa na mkewe na gege la wajanja wachache hadi alipofariki "rasmi"

Ni sawa mkuu na umenena vyema.

Suala linabaki pale pale nani atamfunga paka kengere. Genge la wanasiasa ndo wanatengeneza vigezo vya wagombea wao kutoka kila chama. So far, kama Pasco anavyosema kila wakati chama pendwa ndiyo kinaongoza dola. Kinapaswa, au kwa matazamo wa haraka kuwa role model; hicho ndicho kimeweka pemneni kigezo cha afya; kwa hiyo logically nakubaliana hatuwezi mpa mtu uongozi wa nchi akiwa na afya tete. Kisheria huwezi mbana yeyote maana haijawekwa popote, kwamaba afya bora ni moja ya kigezo!!!

Kwa hiyo hapa tunaongelea, technically hakuna wa kumbana mgombea yeyote atakayethibishwa kuwa na afya mbovu, maana si kigezo na hakikuandikwa kokote! Kama wao watalazimisha kumleta mgombea yeyote... ambaye sisi wananchi tunaamini ni mgonjwa, kwa umoja wetu tumkatae. Kumkataa, ndo shida inapokuwa, what if kati ya watakaomleta akakubali kwa wengi!! Atapita tu, na taongoza kwa style yeyote iwayo.

So relax...
 
Last edited by a moderator:
Bongo ndiyo penyewe,wasiofaa URAIS ndiyo tunaoshabikia,halafu tunalia UCHUMI umedorora oh wezi,mafisadi,saa hizi tuko busy kuwapamba kwa kila maua du.Hii nishidaaaaaaaaaaaaaaaaaa naomba tutafutiwe Consultant aje kutupima UWEZO WETU WA KUFIKIRI.Nadhani Mibongo yetu inashida kidogo.......:angry::angry::angry:
 
Nimeamini binadamu anaweza kukua huku unaona. Hivi hawa washauri wa huyu mzee hawaoni kuwa mzee hali yake kiafya si nzuri? Watu wanapenda pesa utu unawatoka. Kipi muhimu afya ya mgombea wao au urais?

Mzee wa watu anaumwa hilo sio siri tena anaumwa sana tu kitu cha muhimu apumzike angalie afya yake kwani afya yake ni muhimu kuliko urais.
 
Jamani kweli wanatufanya wapumbavu,
Hivi video ile anayoshindwa kunyanyuka kwenye kiti kuna slow motion gani pale???
Kwanza kabla ya kunyanyuka mwangalie uso unavyomshuka na kuchanganyikiwa huku akihisi kizunguzungu

Kudharauliwa, kama kaka yangu Mzee Mwanakijiji alivosema, tusha dharauliwa. Mana kwa mgombea anayetuhumiwa kuwa mgonjwa, na ninavyoona kwa matazamo wangu kuwa Lowasa ni mgonjwa; lakini bado umati mkuuubwaaa unatoka kushangilia na kumtia nguvu agombee; kwa hiyo wao, wa TeamLowasa tayari walikwisha tudharau, maana ndai ya mioyo yao wanajua mzee wao ni mgonjwa. Wanajipa moyo, kuwa akishaingia tu mengine yatajiseti.

Wewe kama ni mtumiaji mkubwa wa social media utakubali, Lowasa anadhaminiwa na watu lukuki. Kwa mazingira ya kawaida, ni dalili ya kupendwa na watu. Kama amenunua hao au la haijalishi ukweli unabaki pale pale watu wanampenda, au ndivyo inavyotengenezwa tujue "anapendwa" Tumekwisha dharauliwa na hao.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna madharau yoyote.
Watu wengine wanapenda kuwachafua wenye mafanikio. Hata Richmond sihusiki sasa wameona haitoshi wanageukia uongo wa Afya za Watu.

Hawajui wakinichagua Umaskini basi Tanzania!
Maana mimi na uchukia umaskini na Umaskini siyo sifa.


Mkuu hii safari ya Matumaini.Hata yesu akiwa bado kwenye ubao na misumari mkono bado baba hawajui walitendalo wasamehe bure.




[h=3]Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais ..[/h]
- Nikichaguliwa kuwa Rais lazma nihakikishe wakina baba wanawaheshimu wakina mama.Wakina baba muache ulevi,muache kulewa na kuwaonea wakina mama.


 
Mficha maradhi kifo humuumbua.hawa TEAMLowasa vichwani vyao ni weupe kabisa wanakuja utetezi dhaifu sana mtu ameshindwa kunyanyuka kwenye kiti hamtaki kukubali kuwa ni mgonjwa?
Nimeamini kuwa ccm unatakiwa kujitoa ufahamu kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Mimi jamani naomba kuuliza maana hili limeshatangazwa sana hapa..!!!

Inasemekana kwamba Lowassa anaumwa Parkinson Disease, hili limesemwa sana hapa ndani, na huu ugonjwa unasemekana athari kubwa ni kumsababishia mtu kutetemeka na baadhi ya viongo vya mwili kukosa nguvu.

Swali je ugonjwa huu unasababisha hitulafu yoyote kwenye Ubongo? Je waweza kisababisha kifo?

Lowassa mwenyewe amepata kusikika akisema Ugonjwa na uzima ni neema kutoka kwa Mungu. Akadai kwamba yeye ni mzima wa afya. Akasema yeyote mwenye mashaka na afya yake akishawishi chama chao watengeneze utaratibu wa kila mgombea/mtiania Urais kupimwa ili ijulikane nani mgonjwa na nani mzima. Sasa mbona hatujasikia mrejesho toka kwa wagombea wengine wakishinikiza kwenda kipima ili kupata vidhibiti vya kumzuia Lowassa "Kihalali" kugombea nafasi hiyo kuliko wanavyomchafua bila uthibitisho?

Nijuavyo mimi kunamagonjwa ambayo matokeo yake yanaonekana hadharani na mengine ni ngumu kujua bila vithibitisho vya Daktari. Sawa twaweza kusema Lowassa mgonjwa hata tu atakapoonekana kujikwaa na kudondoka. lakini hao wagombea wengine ni wagonjwa kiasi gani? Au kwasababu hawajawahi kujikwaa na kuanguka? Mbona Kikwete amekaa na ugonjwa huo alioenda kutibiwa Us kwa. miaka takribani tisa madarakani bila mtu kujua? Je upi ni ugonjwa hata, Saratani ya kibofu au Mtetemo wa viongo vya mwili? (Haijathibitika)

Nimeona kina FaizaFoxy Nyunyu OLESAIDIMU na wengine wakijaribu kumshambulia Pasco kwa utetezi wake Lowassa, Je mnajua afya za wagombea wengine wa ccm? Au kwasababu wao miili yao inaficha magonjwa yao ndani kwa ndani?

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
labda wengine mmeshaliona hili:



My take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.






wote wanaotengeneza hizo picha wana akili kama yako.ni upuuzi na ujinga mkubwa kutengeneza picha za kijinga na anayeziamini ni tondo na taahira
 
Nmeamin kweli waTz noma wanajua mpaka siku mtu anayokufa...du

Nakumbuka usemi wa mwanajamii forum mmoja

Miafrika ndivyo tulivyo
 
respect wa boda hakuna anayemshambulia Pasco, tunasema ukweli. Ukweli ambao hata Pasco amesema kuwa ukiangalia video ya kukaa kwenye kiti, ni "bonafide genuine" Je mkuu hayo maneno ya Pasco unayaelewa maana yake? Hakuna anayemshambulia Pasco tunajadili. Na Pasco hajasema anashambuliwa tunajadili, maana sisi ni sehemu ya Jukwaa la Wafikiriao kwa kichwa na si kwa feeling.
FaizaFoxy ametaja "kila dalili za ugonjwa" hajatuhumu Lowasa kuugua huo ugonjwa, bali kasema kila dalili... wakuthibitisha hayo ni daktari wake na familia yake. Hili liko ndani ya uwezo wa hao tulowataja, na ndo maana mimi msimamo unabaki Lowasa anaumwa, kwa kuwa sina uhakika na ugonjwa anaoumwa sijautaja; tunaelezea dalili za machoni, ambazo zaweza kuwa kweli au si kweli.

Lowasa alisema chama kiandae utaratibu wa kuwapima wagombea wote ikiwamo na yeye, hii ni kauli ya kisisasa maana hata yeye anajua hilo haliwezekani, hata ukiwapima uamuzi wa kutangaza matokeo hautakuwa wa chama bali mgombea binafsi. Na ninadhani hii inaweza kuwa sababu kubwa ya kutoweka afya kama kigezo, chama hakina uwezo kutangaza matokeo ya kiafya ya mgombea yeyote yule. Kwa kwa technicality hii Lowasa na yeye alisema vile out of jazba maana anajua haiwezekani. Sasa sisi ambao haya hatuyajui, tunatokwa mapovu pasi kuruhusu akili zetu kufikiri mara mbili.

Yeye anajijua, anaumwa. Nyinyi ambao mnaamini vimaneno vya niko fit kwa mapambano, haya subirieni, only time will tell na tutakaa pamoja kama waTZ kukubali kumbe alikuwa anaumwa!!!!

Mfungo memo ndugu, kama wafunga weye...
 
Na ile live event iliyokuwa inarushwa pale Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akitangaza nia nayo ilifanyiwa "slow motion"? Kila mtu alishuhudia jinsi viungo vya mzee visivyopatana; kila kimoja kikitenda jinsi kipendavyo pasi na "central command".

Mkuu umenifurahisha sana
 
wote wanaotengeneza hizo picha wana akili kama yako.ni upuuzi na ujinga mkubwa kutengeneza picha za kijinga na anayeziamini ni tondo na taahira


kwa bahati nzuri na kwa mda maalumu nimekuwa karibu na huyo anayetajwa humu....mengi nimeyashuhudia na ni zadi ya haya yanayosemwa humu...ni ukweli usiopingika kwamba lowassa anauwa tena anaumwa sana...hali yake si nzuri kabisa. siku za mwanzo kabla hajabadili utaratibu wa maisha hasa nyakati za usiku alikuwa anapata shida sana anapolala, kugeuka hawezi. ikitokea daktari amechelewa kumdunga sindano na kumpa vidonge basi atavimba vidole,miguu, kutembea hataweza na akitembea basi atajikokota sana, hataweza hata kupiga mswaki, achilia mbali kushika kikombe cha chai....
kuna siku alikuwa arusha kuonana na baba askofu wa katoriki wakati wa mazungumzo alimba udhuru zaidi ya mara sita kwenda kujisaidia haja ndogo hata baada ya kuonyeshwa mahali pa haja hiyo bado aliomba mtu wake ampeleke (siku natangazia nia arusha alikwenda haja ndogo mara mbili akitkea pale jukwaa kuu)...alitembea kwa shida sana, vidole vilikuwa vikitetemeka sana,na baada ya mazungumzo mzee alishindwa kupanda kwenye gari..kunyanyua mguu ilikuwa ni shida sana mpaka akasaidiwa....
lowasa hapo alipo hawezi kugeuza shingo..anageuka mwili mzima ..ngozi ya mwili wake imebadilika kwa kiasi kikubwa ..weupe alio nao wa sasa si kawaida, hawezi hata kukunja nne...hatua ilipofika kwa sasa analala chumba kimoja na daktari wake na mkewe chumba kingine ili daktari aweze kumwangalia kwa ukaribu...

wakati flani kwenye mazungumzo alisikika akisema anatamani awe rais wa nchi hata kwa wiki mbili tu...hata hivyo tahadhari zote zimezingatiwa katika kumpata rais wa nchi anayefaa ...
 
Kama ni editing kweli basi technology yetu imekua sana wapelekeeni bongo movie tukuze soko la filamu maana huwa wanachemka hapo tu
Sema dah mazee mtamuua mwenzenu aisee
 
Bi Mkubwa Alinda (samahani nimeangalia avatar yako kama kuna makosa utanisameh) teamlowassa muda huu inaangaika kweli kweli tayari wanajua afya ya boss wao ni mgogoro wasichotaka kijulikane kwa waTanzania hasa wapiga kura ni afya kabla ya mwezi october.Baada ya hapo Ikulu itaongozwa na mtu yoyote wakati Lowassa atakuwa kwenye chumba cha matibabu Ujerumaniiiiiiii.

Nimeamini binadamu anaweza kukua huku unaona. Hivi hawa washauri wa huyu mzee hawaoni kuwa mzee hali yake kiafya si nzuri? Watu wanapenda pesa utu unawatoka. Kipi muhimu afya ya mgombea wao au urais?

Mzee wa watu anaumwa hilo sio siri tena anaumwa sana tu kitu cha muhimu apumzike angalie afya yake kwani afya yake ni muhimu kuliko urais.
 
Last edited by a moderator:
Jamani kweli wanatufanya wapumbavu,
Hivi video ile anayoshindwa kunyanyuka kwenye kiti kuna slow motion gani pale???
Kwanza kabla ya kunyanyuka mwangalie uso unavyomshuka na kuchanganyikiwa huku akihisi kizunguzungu
Eti yeye kafanyiwa slow motion ila yule mlinzi anaeonekana nae pale hajafanyiwa, duh.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, japo mimi siko Team Lowassa, wala team yoyote, ila namsupport huyu 'jamaa yangu', kiukweli tangazo hilo is a mistake!, kwanza namfahamu huyo jamaa aliyesaini hapo anajiita Mshauri wa Siasa wa Team Lowassa Makao Mkuu, the way alivyoiweka ni misleading, watu wanaweza kudhani ni kweli huyu ndie mshauri wa Team Lowassa, kiukweli huyu ni kiongozi wa fb group na whatsup group linalojiita team lowassa na huyu ndio mshauri wa group hilo.

Mimi nimeiangalia video moja hiyo ya kukaa, ni bonafide genuine, kuhusu hali ya afya ya 'jamaa yangu' hata mtu mwenye macho tuu ya kawaida, hahitaji kutumia darubini au hadubini kuona au kuelezwa kuwa mzee ni mgonjwa, ila, hali ya afya ya mgombea sio miongoni mwa sifa, vigezo au sababu ya kukubalika au kukataliwa, kwa sababu inachohitaji CCM sio kiongozi bora, kama CCM inataka kiongozi bora itampitisha Jaji Agustino Ramadhani. CCM haihitaji kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kuihamisha Tanzania hapa ilipo kuifikisha kule ilikopaswa kuwepo. Ingehitaji kiongozi wa aina hii ingempitisha Prof. Mhongo, Dr. Magufuli au Prof. Mwandosya. Rushwa na ufisadi sio tatizo kwa CCM, kwa sababu CCM ndie mzazi, mlezi na msimamizi mkuu wa rushwa zote na ufisadi wote unaolitafuna taifa hili.

CCM inachohitaji ni ushindi tuu!. CCM inataka kushinda tuu uchaguzi kwa landslide victory, kwa njia yoyote ile, na kwa mbinu zozote, yaani by hooks and crooks!. Kiongozi wa kuwapatia CCM hiyo landslide victory ni huyu 'jamaa yangu', hiyo afya ataimarishwa na yule yule anayesimamia kuhakikisha 2015 'jamaa yangu anatinga Ikulu ya Magogoni au kupitia CCM au kupitia njia nyingine yoyote!.

Ikitokea ni yeye akapitishwa na CCM, then huyu ndie rais wetu 2015!. Ikitokea asipitishwe na CCM, chama chochote atakachojiunga nacho ndicho chama kitakachoishika ikulu yetu!. Hii hali ya afya tunamuachia YEYE ambayo huyu 'jamaa yangu' ameishasema wazi kuwa "nayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!.

Kwa sasa zimebaki siku 10 tuu muhimu!.

Pasco



Mkuu Pasco umeongea ukweli kabisa lakini hapo kwenye swala la afya nitakuwa nipo na tofauti na wewe kusema afya siyo kigezo cha mgombea uraisi siyo sawa kwani kama tulifanya makosa 2005 hatuwezi kurudia tena hayo mwaka makosa mwaka huu .Kigezo cha kwanza cha mgombea uraisi mwaka huu lazima tuangalie afya yake kwanza .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom