Unaweza kuthibitisha kauli yako?Kenya wana katiba tunayoambiwa ni bora sana lakini ufisadi na umasikini kwa raia umekita mizizi!
Ndio kusema kwamba katiba ya Kenya ni nzuri kwa wanasiasa tu!
Katiba nzuri na huku una njaa ni sawa na unyani
Tunahitaji Katiba ya Wananchi itakayotokana na mawazo yao na siyo Katiba nzuri.Kama Katiba ya Kenya haijatatua changamoto zao za kiuchumi,kijamii,kisiasa,usawa ama haitoi Haki sawa kwa wananchi,ni jukumu lao kuiboresha na isiwe sababu ya Watanzania kutokuandika Katiba yao.
Sidhani kama ni sahihi kuwatisha Wananchi, ujenzi wa uchumi hauwezi kuwa mbadala wa Katiba Bali Katiba Bora ni msingi wa kujenga uchumi endelevu.
Tusiwapotoshe Watanzania. Kwenye madaraka hawastahili kuwazibia Wananchi kujipatia Katiba waitakayo.