kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,318
- 12,622
NI kweli Katiba hii ya mwaka 1977 ni nzuri sana kwa kiongozi na chama kilichoko madarakani. Hata CCM ikianguka leo chini ya katiba hii na sheria hizi za uchaguzi na jeshi la polisi haitarudi tena madarakani milele.
Hata CHADEMA kama ikiingia Ikulu leo chini ya Katiba hii na sheria hizi za uchaguzi na jeshi la polisi hata wao hawatapenda kuandika Katiba mpya, wataing'ang'ania Katiba hii hii.
Katiba hii ya 1977 ni nzuri sana kwa kiongozi ambae anajali watu wake kwakuwa kwa kutumia katiba hii unaweza kujenga barabara ya njia 6 hata kwenye mitaa yenye msongamano mkubwa kama ya Posta au Kariakoo kwa gharama ndogo kabisa. Lakini, Katiba hii ni mbaya kwa kiongozi mbaya, mwizi, mbadhilifu, mvivu, mkabila, mdini, goigoi na dikteta.
Hata hivyo, sitaki mtu atuaminishe watanzania kuwa Katiba mpya ndiyo itakayomaliza shida zetu za upatikanaji wa hewa safi, maji safi, chakula, afya, amani na huduma nyingine ambazo sasa hivi hazifanyi vizuri. Kenya tuliwasifu sana kuwa wanayo Katiba mpya na yakisasa kabisa, lakini hali yao sio bora kivileee kama nilivyokuwa ninatarajia kuiona. Bado Kenya walihangaika sana na mambo yao ya uchaguzi na kutoa matokeo ya uchaguzi. Kule Marekani wanayo katiba bora sana lakini bado walisumbuliwa na uchaguzi na utangazaji wa matokeo ya uchaguzi wao.
Siwezi kuunga mkono serikali kupunguza fedha kwenye miradi kama ya maji, afya, elimu, kilimo, na miundombinu kwasababu ya kwenda kuandika Katiba mpya. Wengi wanaoitaka Katiba mpya haraka na kufa na kupona ni kwaajili tu ya kuongeza uwezekano kwa kundi na watu wao kuweza kuchaguliwa na kupata uongozi wa kuchaguliwa kama vile Urais, Ubunge na Udiwani na kuunda serikali. Malengo kama haya sio kipaumbele kwangu mimi mtanzania.
Ninapenda Katiba mpya, lakini Katiba ambayo inamuadhibu kikamilifu mtu yeyote ambae ataiba au kutumia vibaya rasilimali zetu, katiba ambayo inalinda rasilimali zetu na watu wetu kikamilifu, katiba ambayo inajali haki za watu, lakini Katiba ambayo asiyefanyakazi hatakula wala kutibiwa.
Na mara nyingi "Kaiba nzuri" ni ile inayowafurahisha wazungu, yenye maslahi kwa wazungu kuliko raia.