Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano?
 
🤣🤣🤣🤣🤣
2025 inamtesa. Kama yeye tu hana uhakika wa kushinda 2025 bila kuiba uchaguzi je hao watakaomfuata 2030 wataweza? Watakubali abadilishe katiba baada ya 2025 ambapo yeye hatokuwa na cha kupoteza?

Aache hadaa. Na hao mabeberu washaanza kumsoma. Maneno matupu hakuna concrete action. Mwakani kuna uchaguzi serikali za mitaa kampeleka mkwe TAMISEMI kwenda kusimamia. Chaguzi ndogo zinafanyika kupoteza hela tu hakuna demokrasia yoyote. Hiyo 2025 kutakuwa na tofauti gani?
 
Umejitahidi kupotosha mkuu,

Alichosema ni kuwa, watu wapewe shule vizuri ya katiba hii tulionayo, na pia kasema vizuri kabisa, katiba ni ya watanzania, hatuwez sema tuchukue maoni ya wanasiasa tu ndio tuunde katiba, lazima kila mtu atoe maoni, na ili kila mtu atoe maoni ni lazima watu waijue hii katiba iliyopo, na yupo sahihi.
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya ! je mko tayari kwenye mashindano???
Na ndio maana wanawaona watu ni wajinga sio! Hayo ni mawazo yake! Katiba tunaifahamu vizuri sana na haitufai kwa wkt wa Sasa. Kama tusingekuwa tunaielewa tusingetoa maoni ya katiba mpya kwenye time ya Jaji Warioba. Period!
 
Umejitahidi kupotosha mkuu,
Alichosema ni kuwa, watu wapewe shule vizuri ya katiba hii tulionayo, na pia kasema vizuri kabisa, katiba ni ya watanzania, hatuwez sema tuchukue maoni ya wanasiasa tu ndio tuunde katiba, lazima kila mtu atoe maoni, na ili kila mtu atoe maoni ni lazima watu waijue hii katiba iliyopo,
Na yupo sahihi
Mbona huko bungeni,wanasiasa hupitisha mambo badala yetu mkuu tena mengi ambayo hata wananchi hatuyataki lakini wao hupitisha.
 
Hapo maana yake, ianzishwe topic ya katiba kwenye masomo shuleni na vyuoni. Na kizazi hiko kinachosoma topic hiyo hadi kikue kifikie umri wa mtu mzima.
Hapo wanalenga kizazi cha mwaka 2055 hadi 2070. Wakati huo kizazi hiki kinacho simamia serkali, kitakua kishakwisha, uamuzi utabaki kwa vijana wa kipindi hiko.

Kazi kwelikweli..!!
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya ! je mko tayari kwenye mashindano???
Aiseeh kashtuka kaona hapa juzi tu nimewapa ka Uhuru kakuongea wanani chahafya hivi vipi ikija tume huru nakatiba mpya😆😆😆

Gafra kaiona faida ya katiba ya zamani kwa kiongozi Kama yeye😆😆 nyelele hakuwa mpuuzi aiseeh🙌🙌
 
🤣🤣🤣🤣🤣
2025 inamtesa. Kama yeye tu hana uhakika wa kushinda 2025 bila kuiba uchaguzi je hao watakaomfuata 2030 wataweza?? Watakubali abadilishe katiba baada ya 2025 ambapo yeye hatokuwa na cha kupoteza?

Aache hadaa. Na hao mabeberu washaanza kumsoma. Maneno matupu hakuna concrete action. Mwakani kuna uchaguzi serikali za mitaa kampeleka mkwe TAMISEMI kwenda kusimamia. Chaguzi ndogo zinafanyika kupoteza hela tu hakuna demokrasia yoyote. Hiyo 2025 kutakuwa na tofauti gani??
Hajavunja rekodi ya "mkwe" wetu yule.

Hapo vipi? - Makongoro Nyerere.
 
Back
Top Bottom