Mr Lukwaro
JF-Expert Member
- Jun 3, 2023
- 357
- 621
Nakumbuka kipindi cha mchakato wa Katiba, Prof Issa Shivji akitoa Darsa kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa, alisema Wananchi wengi hawana Elimu ya Katiba na kusema Ukienda kuwahoji wanataka Katiba ipi, jibu lake atasema Sijui Katiba, hivyo hautapata hiyo Katiba unayoitaka kwasababu umekwenda kuhoji mahitaji ya Katiba wakati wewe mwenyewe haujajiandaa kuhoji na hauna ufahamu wa unachokitafuta!
Prof Shivji alitoa mbinu ya maswali kwa Wananchi, kwamba unawauliza maswali kuendana na Maisha yao, mfano kwenye Elimu Mwananchi anaposema Hajui kusoma ama hajui kinachoendelea kwenye Uongozi wa Serikali yao kama vile wanaowachagua, hapo kwenye Katiba utaeleza upatikanaji wa Elimu Nchini.
Unamuuliza Mwananchi unataka Ardhi imilikiwe na nani na iwaje, kila Mtu atakupa maoni yake.
Una hoji kuhusu Haki,β¦ kila kitu unamhoji, mwisho wa siku utajikuta umepata maoni kibao, kisha kazi ya kuandika Katiba ni ya Wataalam wa Katiba kuchambua yale maoni na kuyaweka kitaalam na ndivyo Katiba inavyoandikwa.
Katiba haisomwi kama hadithi na kuielewa hapohapo, inaeleza kifupi zaidi lakini kila kitu Kimo ndani na ndio sababu inaitwa sheria mama, yaani sheria zote zinatungwa zinatoka kwenye Katiba.
Katiba ni maoni ya Wananchi na inaandikwa na Wataalam wa Katiba kwa ufupi Kisheria.
Serikali inapowaambia Wananchi hawaijui Katiba na wanahitaji miaka mitatu ya mafunzo, hiyo ni dharau kubwa sana ya Serikali kwa Wananchi!
Tume ya Jaji Warioba iliainisha hayo ya Elimu na kueleza Elimu ilivyotolewa, hao Serikali wanasema Wananchi hawajui, Je Serikali imesahau kwamba Tume ya Warioba walikwisha kulimaliza hilo?!!
Serikali wanataka Wananchi wote tuingie kusoma digrii ya sheria miaka mitatu ili tujadiliane Katiba?!
Wananchi mnatupa wasiwasi sana wa uwezo wenu mliopewa dhamana ya Madaraka kutuongoza, hayo sio majibu ya kutuambia Leo Mheshimiwa Waziri wa Sheria ni bora ungesema kiufupi tu kwamba Serikali haipo tayari kwa Katiba mpya hadi baada ya miaka mitatu ili tuelewe hivyo kuliko kutupa sababu ambazo hazina msingi na kutengeneza maswali mengi yasiyo muhimu!!
Katiba mpya ya Wananchi ni sasa.
Tanzania ni yetu sote! πΉπΏπ€πͺπΎ