Bilionaire kekeman
Senior Member
- Nov 26, 2022
- 142
- 823
Mimi bwana sipendi sana kuandika mambo ya siasa hizi za Bongo siku hizi sio kwasababu sipendi ila sipendi tu kuandika kuhusu hizi siasa uchwara.
Ok ni hivi, acha niandike kwa ufupi kuhusu tamko la Mbowe (CHADEMA)
Nimefikira sana kuhusu kauli na kuendelea kujifunza kuhusu mambo mengi sana juu ya siasa uchwara zilizopo Tanzania kutoka upinzani na chama tawala.
Kwenye hili la CHADEMA juu ya kutangaza maandamano yatakayoanza rasimi tarehe 24 Jan 2024 Ili kupinga miswaada mitatu ya sheria ambayo itaanza kusikilizwa hivi punde huko bungeni, ambayo miswaada yenyewe itahusu maswala ya uchaguzi, sio kosa kuhusu hilo maana nalo ni swala la msingi lakini naomba uelewa zaidi kuwa je watanzania swala la uchaguzi ndio swala pekee muhimu zaidi Kuliko mengine?
Kinachoonekana hapa ni kuwa CHADEMA hili la uchaguzi limekua tatizo au kikwazo kwao kwasababu lina msrahi kwao ya nafasi za uongozi maana wao hapo ndio wanapo patia Pesa na ulaji.
Sijaona umuhimu sana wa CHADEMA kuhitaji kutumia nguvu kubwa ya maandamano kwajili ya kutetea hili la uchaguzi, maana yapo ya maana zaidi kwa watanzania na hawakutumia nguvu kama hii wanayotaka kuitumia sasa.
Ok ni hivi....
Yapo mambo mengi sana ambayo ni matatizo makubwa kama mafuta kupanda bei, Ulaghai kwenye pembejeo, Ukatikaji wa Umeme usio na tija, Vikokotoo kwa watumishi wasio wanasiasa, Sheria mpya ya Bima ya afya, Kuwaongezea Viinua mgogo wanasia wa ngazi za juu, Sheria mbovu za kodi, Ukosefu wa ajira, na Upigaji kwenye ripoti ya CAG.
Ajabu sasa mambo haya ambayo yanawaumiza Watanzani kila leo na kuwaingiza kwenye umasikini mkubwa na kuwaacha bila matumaini ya kesho yapo na yanafahamika na wanasiasa hawa wanao jiita watetezi wa haki za watanzania lakini awajaweza hata siku moja kutoka mbele na kuitisha maandamano makubwa nchi nzima.
Wapo kimya na ikijulikana kuwa hayo matatizo yapo na yakiwatesa watanzania wanasiasa hawa hawajawahi kutumia nguvu kubwa kama hili waliyotumia ya kuitisha maandamano kupinga haya na kupigani haya.
Isipokuwa wamekaa kimya kama hayapo. Je, swali ni kwanini?
Jibu ya hili ni kwasababu hayana masilahi ya moja kwa moja kwao, ila yale ya uchaguzi yana faida ya moja kwa moja kwao, kwasababu yanawagusa wao, kwa mantiki hiyo inaonesha kuwa wanasiasa wetu hawapo kwajili ya matatizo yetu bali macho yao yanangalia chaguzi na jinsi wao watakavyo weza kushinda viti hivyo au nafasi hizo ili wapate ulaji, Wanacho Linda na kupigani ni nafasi zao na matumbo yao na sio kero za watanzania.
Kwasababu huu ndio maana niliona siasa zetu ni upuuzi mtu, hakuna mwanasiasa wala kiongozi ndani ya CCM au nje ya CCM aliyepo kwajili ya Mtanzania.
NB: Jiepushe kutumika kwajili ya matumbo na manufaa ya watu wachache ambao wemejivisha koti la uzalendo ili hali ndani yao ni matapeli wa kisiasa.
Siasa safi anza kupigania uchumi wako mwenyewe, ukiwa safi kiuchumi huto tumika na hawa wanasiasa uchwara kwa masilahi yao binafsi.
Zingatia kuwa Siasa zetu bado zinatafunwa na matumbo yenye njaa, Ulafi, Unafi, Ujinga na Undumila kuwili.