Hii habari ya kulazimika kudhaminiwa na chama cha siasa ukitaka kugombea nafasi yoyote inatakiwa ikome

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,210
12,710
Hii ishu siyo ya kidemokrasia kabisa. Kwanza inamnyima haki ya kidemokarisia mwananchi mpaka alazimike kuwa kwenye haya magenge ya siasa.

Pia inawanyima wananchi kuchagua wampendae, badala yake ni kama kwa sehemu wanachaguliwa na haya magenge. Fikiria kuna wagombea labda 3. Kila mtu/watu wanampenda wao. Lakini chama cha siasa kinampitisha wao, wananchi wanatakiwa kuchagua waliopitishwa na haya magenge tu na si wamtakae. Kama ni hivyo basi waseme hata kupiga kura lazima uwe kwenye chama cha siasa.

Wengi wanaweza kuwa wanafaa kuwa maspika wa jamhuri ya muungano. Na kila mbunge kuna mtu anaona anafaa, lakini haya magenge yatachagua wachache na wabunge watalazimika kuchagua hao.

Kiufupi ni kwamba, haki ya ugombea binafsi ni muhimu.
 
Ukishakuwa na serikali inayotumia propaganda cheap namna hii za kwenda kwenye mitandao ya jamii na kufanya spins, ujue kuna tatizo kubwa serikalini.
 
Hii ishu siyo ya kidemokrasia kabisa. Kwanza inamnyima haki ya kidemokarisia mwananchi mpaka alazimike kuwa kwenye haya magenge ya siasa.

Pia inawanyima wananchi kuchagua wampendae, badala yake ni kama kwa sehemu wanachaguliwa na haya magenge. Fikiria kuna wagombea labda 3. Kila mtu/watu wanampenda wao. Lakini chama cha siasa kinampitisha wao, wananchi wanatakiwa kuchagua waliopitishwa na haya magenge tu na si wamtakae. Kama ni hivyo basi waseme hata kupiga kura lazima uwe kwenye chama cha siasa.

Wengi wanaweza kuwa wanafaa kuwa maspika wa jamhuri ya muungano. Na kila mbunge kuna mtu anaona anafaa, lakini haya magenge yatachagua wachache na wabunge watalazimika kuchagua hao.

Kiufupi ni kwamba, haki ya ugombea binafsi ni muhimu.
Uhuru nanguvu ya wapiga kura itakuwepo, ukiondoka ulazima wa kudhaminiwa na chama cha siasa kwa wagombea. Ukweli ni kuwa mgombea binafsi TZ ni ruksa kwa kufuatana na hukumu ya mahakama kuu au mahakama ya rufaa (sina hakika ni ipi), ila hili swala bado kutekelezwa na tume ya uchaguzi sijui wanangoja nini? Mimi ninafikiri tume ya asasa ya uchaguzi inavunja sheria ya nchi kwa kutoruhusu wagombea binafsi.
 
Back
Top Bottom