Hela inatafutwa kwa nguvu jamani, mmh!

Hela inatafutwa kwa nguvu jamani, mmh!

Furaha hua ina mwisho,utasema nikipata kitu fulani nitafurahi,ni kweli utafurahi kwa muda kisha kitu hicho utakiona ni cha kawaida tu,halafu utahamia kwenye kitu kingine na kusema ukikipata utafurahi....furaha hua ni ya muda tu,furaha ya kweli haisababishwi na material possessions,

Wakati ukiishi kwa kukimbizana na hela tambua kua muda wako wa kuishi hapa Duniani nao unapungua,at the end unakuja kukumbuka kua ulisahau "Kuishi"
Best advice ni kuenjoy every moment ya furaha unayoipata..ukipata fursa ya kufurahia maisha na uhai furahia
Hata kama Kwa kidogo
 
*
Mathayo 6:25-34
25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.*
 
Natoa pole na pongezi kwa yeyote mwenye kutafuta riziki yake, mchezo sio mdogo🙌🏾, Mungu MKUU na atutangulie!
Weka bidii kwenye utafutaji ila pia usisahau kula raha na kufurahisha nafsi.

giphy-downsized.gif
 
Usipokuwa mvumilivu unaweza kukufuru bure, maana Kila unachofanya kujipatia kipato unakuta kinagoma

Na ukienda kwa Mganga, hataki damu ya Kuku tena, anataka utoe Watoto 🙌

Anyways, Maisha ni foleni aliimbaga Bonny Mwaitege 🙏🙏
 
Yani hapa nimelala usiku masaa mawili hivi, embu nijiegeshe asubuhi hii, leo nijipe off (mchana najua kazi itaendelea, ila nilale asubuhi hii)
Usipoijali afya yako sasa hivi,basi itakusumbua sana huko mbeleni,

Sasa hivi wewe na afya mnaitafuta hela,baadae itakua wewe na hela mnaitafuta afya.
 
Nafanya.lakini najikuta natamani kukifanya kwenye ubora zaidi.na kuhitaji wa nguvu ndipo unapotokea.maana hata kile nkifanyacho hakikidhi mahitaji

Muuza nyanya angekaa tu angeuza?
Akitembeza na mzigo kichwani door to door ndo anauza
Na wengine Wana mitaji wanafungua magenge wanauza
Tuendelee kupambana, hakuna kukata tamaa. Maisha hayajawahi kuwa rahisi, wewe unapitia hili, mwingine anapitia lile. Kila mtu ana changamoto yake hapa duniani. Bahati mbaya dunia haina huruma, tuzidi kupambana hadi pumzi ya mwisho.
 
Vyote viwili mkuu,yani uwe na maisha mengine nje ya utafutaji,unatenga muda wako wa kuishi,unafanya kitu ambacho nafsi yako inapenda,maisha sio kukimbizana na hela tu,kila siku watu husema "Natengeneza kesho yangu" cha ajabu hiyo kesho hua haifiki,

Yachukulie maisha simple tu hata kama unapitia magumu,relax and enjoy the life,

Uhai una thamani kubwa sana kuliko kitu chochote kile,as long as una afya njema,don't forget to live your life,maisha ni mara moja tu,ukifa hurudi tena,usiishi maisha yako yote kwa kujikatia tamaa,kujiona mnyonge au kujiona wewe ni masikini,uhai peke yake ni utajiri mkubwa sana.
Mie nimekuelewa sanaaa.
 
Best advice ni kuenjoy every moment ya furaha unayoipata..ukipata fursa ya kufurahia maisha na uhai furahia
Hata kama Kwa kidogo
Hapa ndio point ilipo dada mkubwa kuishi maisha ya shukrani kila siku kuamka tu asubuhi ni utajiri mkubwa sema wengi tumeji condition utajiri kwenye material things only kumbe utajiri ni kuwa na upendo, afya njema. Chukulia mfano wa kina chaba wahazabe fedha kwao si kigezo cha furaha yao Trump anamsemo wake anasema never ever lose momentum
 
Tuendelee kupambana, hakuna kukata tamaa. Maisha hayajawahi kuwa rahisi, wewe unapitia hili, mwingine anapitia lile. Kila mtu ana changamoto yake hapa duniani. Bahati mbaya dunia haina huruma, tuzidi kupambana hadi pumzi ya mwisho.
Kabisa dunia haitakuwa na huruma mfano kama umefuatilia ishu ya Jaffrey Epstein nadhani utaelewe na kwanza mfumo wa dunia hauwahitaji watu kama hao wenye huruma nilishangaa sana kusoma post mahala kuwa utajiri mkubwa upo kwenye umaskini yani kuwa tu maskini wa kifkra unaopelekea umaskini halisi kuna NGO kibao na mataifa kibao yanadili na huo umaskini lakini anaefaidika ni hao wanao deal nao na siyo hao maskini 😭
 
Back
Top Bottom