Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Itachukua muda watu kuelewa fiada ya hizi tozo,
1. Huduma za jamii zitaboreshwa
2. Ajira mpya serikalini zitaongezeka
3. Mzunguko wa fedha utarejeshwa kwa wananchi kupitia mishahara/ ujenzi wenyewe / ajira / vibarua na manunuzi.
4. Kutanuka kwa huduma za ziada usafirishaji / fedha (Banking / mobile money services)

Uzuri Tozo hizi hazipelekwi kujenga madarasa Sudani Kusini ni humuhumu nchini.
Hizi tozo zingekuja wakati wa Magufuli dunia ingepasuka!!
 
Hivi vituo 220 vipya budget ya dawa manurse ambulance ikoje? Ni kweli watanzania ni wagonjwa kiasi hiki?
Mkuu wewe unishi sehemu zenye kila huduma, tembea uone, Kuna watu wanakata 15 km kufuata huduma za afya.
 
Magufuli alikopa trilioni 30 ndani ya miaka mi tano
mama Samia amekopa trilioni 20 ndani ya miezi mitatu
 
soma ripoti ya deni la taifa ipo kwenye tovuti ya wizara ya fedha na tovuti ya bot pia mwenye ripoti za cag

Lete hiyo ripoti, unaongopa,

Kuna Mikopo ilikopwa kabla ya Samia ila imekuwa dew wakati huu,

Pengine unasemea hayo,
 
RAIS MAGUFULI VITUO VYA AFYA 44 MIAKA 3 | RAIS SAMIA VITUO VYA AFYA 220 MIEZI 3

Ukisoma "Kitabu Cha Hali ya Uchumi Tanzania " cha mwaka 2018 ukurasa wa 60,utaona wakati Rais Kikwete anaondoka madarakani mwaka 2015 vituo vya afya vya serikali vilikuwa 507,Mpaka 2018|19 jumla ya Vituo vya afya vya serikali ilifikia 551 sawa na Ongezeko la Vituo vipya 44 ambazo ni 9% chini ya Hayati Rais Magufuli,

Kwakutumia tozo hizi za Kizalendo Rais Samia anajenga vituo vya afya vipya 220 kwa miezi mitatu ( 3 ) tu sawa na ongezeko la 43.4%,Nakwa lugha rahisi kabisa,Tunasema kasi ya Ujenzi wa vituo vya afya ya Rais Samia kwa miezi mitatu ni X5 zaidi ya kasi ya Ujenzi wa vituo vya afya ya Rais Magufuli kwa miaka mitatu mfululizo,

Jumla ya vituo vyote vya Serikali vipya na alivyokarabati Hayati Rais Magufuli kwa miaka mitano vilifikia 487 ( soma Hotuba yake ya mwisho bungeni ukurasa wa 24 ),Hii inamaana gani, Rais Samia kwa muda wa miezi hii michache atajenga karibu nusu ya vituo vyote vilivyojengwa|kukarabatiwa na Hyt Rais Magufuli kwa miaka mitano aliyokaa madarakani,Mama anastahili pongezi kama kweli tunamwogopa Mungu,

Na kwa andiko hili,Itusaidie kutambua faida ya tozo kwenye kuwahudumia na kuwafikia kwa haraka watoto wa masikini wa nchi hii wanaokufa kila dakika kwa kukosa huduma za afya hasa hasa akina Mama na Watoto huko vijijini,

Att |Isionekane napinga kazi nzuri ya Hyt Rais Magufuli hapana, ni katika kuangazia Mwanzo wao wote kwenye hili la vituo vya afya na Samia hakamatiki kwani namba hazidanganyi,

|[ Hili ndio Jibu la kwanini leo tozo na Sio zamani ]|

|WANAOULIZA RAIS SAMIA SULUHU ANATUPELEKA WAPI | HERE IS WHERE WE GO BRO'S & SISTERS KUWENI NA AMANI NCHI YENU IKO MIKONO SALAMA & SHUPAVU YA MAMA|

...Kazi iendelee ...

View attachment 1922453
Not mesoma tu kichwa Cha habari. Kusema rais amejenga mradi fulani ni ujinga wa kiwango cha juu sana. Miradi inajengwa kutokana na kodi tunazolipa sisi wananchi. Rais ni mtumishi kama watumishi wengine, na anatekeleza majukumu ya ofisi yake kwa mujibu was sheria, na miradi inayotekelezwa sio hisani ya rais bali ni stahiki za raia kutokana na kodi wanazolipa.
 
Sio vibaya kujenga vituo lkn wahudumu wa afya ni wauaji na hawana roho ya imani kabisa. Yaani mgonjwa anakufa kwa sababu ya uzembe wa kijinga tuu. Ukitaka kuwashauri hawasikii, sijui hata huko chuoni wanafundishwa nini, kuua au kuokoa maisha ya watu. Mungu anawaona kwa kweli na kuna siku mtatoa hesabu za matendo yenu
 
Wako wachache na maslahi finyu wanachoka ,wewe ukiumwa wapitishie rupia kidogo fasta utakuta wako na wewe mda wote
 
Not mesoma tu kichwa Cha habari. Kusema rais amejenga mradi fulani ni ujinga wa kiwango cha juu sana. Miradi inajengwa kutokana na kodi tunazolipa sisi wananchi. Rais ni mtumishi kama watumishi wengine, na anatekeleza majukumu ya ofisi yake kwa mujibu was sheria, na miradi inayotekelezwa sio hisani ya rais bali ni stahiki za raia kutokana na kodi wanazolipa.
Vyovyote iwavyo sifa huwa zinaenda kwa kiongozi mkuu wa Serikali.Na diwani atasema nimejenga kituo hiki cha afya,halikadhalika mbunge.
 
Back
Top Bottom