Makonda na mind games: Ukubali usikubali, Rais Samia anasahihisha madudu ya Hayati Magufuli!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Makonda is on a mission kumsafisha Magufuli kwa mazuri ya mama Samia.

Makonda ni mwanasiasa anayeweka maslahi yake mbele na kuutupa ukweli ili kuridhisha matakwa yake kisiasa.

Magufuli alikuwa na mafanikio yake, na madudu yake kibao.
Magufuli alifanikiwa na SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere na umeme, vituo vya afya nchi nzima, Daraja la Busisi na mengine lakini Mafuguli alikuwa dikteta.

Mbowe aliwekwa ndani sijui mara ngapi, watu walibambikwa kesi, wafanya biashara walinyang'anywa amana zao na kufilisiwa.

Watu waliwekwa ndani na kubambikwa kesi.

Wengine walipotea na kutoonekana, kama Azory Gwanda, Ben Saa Nane na Lwajabe.

Lissu alipigwa Risasi.

Sasa anapotokea Makonda na kumfananisha Maguguli na Mama Samia kuwa wako sawa, basi nasema Makonda huo ni zaidi ya ujinga, ni upumbavu.

Mama Samia kwa sasa ameipaisha nchi kiuchumi, na anasahihisha madudu ya Magufuli.
 
Mbona ni rais mwenyewe alidai yeye na marehemu ni kitu kimoja? Kama Mbowe kuwekwa ndani, kawekwa ndani muda mrefu kipindi cha rais wa sasa kuliko mtangulizi wake. Watu kupoteza, kushambuliwa yanatokea chini ya wote. Sikumvuki kama waMasaai walisumbuliwa wakati wa marehemu, Ila mrithi wake ana chuki ya wazi kwa waMaasai.
 
Na ugumu wote huu wa maisha wewe unasema nchi inapaa kiuchumi? Ni kweli gharama za maisha zinapaa, lakini hilo siyo jambo la kujisifia.
Hivi wengine ujinga wa aina hii huwa mnautoa wapi? Hebu nipe siri na mini nikauazime angalau mara moja nilete hoja za kitaahira kama hii!
 
Na hapo hatujaanza kulipa madeni tunayokopa, muhimu ni fedha zifanye kazi iliyokusudiwa.
 
Mbona ni rais mwenyewe alidai yeye na marehemu ni kitu kimoja? Kama Mbowe kuwekwa ndani, kawekwa ndani muda mrefu kipindi cha rais wa sasa kuliko mtangulizi wake. Watu kupoteza, kushambuliwa yanatokea chini ya wote. Sikumvuki kama waMasaai walisumbuliwa wakati wa marehemu, Ila mrithi wake ana chuki ya wazi kwa waMaasai.

..kama Samia na Magufuli ni kitu kimoja mbona Samia hateki na kutesa wapinzani kama Magufuli?
 
Samia atavuna alichopanda kwa kuteua Mamluki mwenye kashfa , unachagua mtu mchafu ili uwawin Wasukuma , ni msukuma yupi wa kushawishika na Makonda ?

kazi mnayo .
Kabla hujawahusisha wasukuma!.
Jiulize ni kwa nini Makonda alishangiliwa kwa wingi wa ule Umati pale uwanjani Dar es Salaam?
Je!
Washangiliaji walikuwa wasukuma?
Acha upumbavu uliokujaa!
 
..kama Samia na Magufuli ni kitu kimoja mbona Samia hateki na kutesa wapinzani kama Magufuli?
Mbona bado mnasusia chaguzi ndogo kama huyu wa sasa anawapendeni sana wapinzani?

BTW:Wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 yote hayo utayashuhudia.
 
..nakubaliana na wewe kwamba huenda ameficha makucha yake mpaka wakati wa uchaguzi.
 
Makonda is on a mission kumsafisha Magufuli kwa mazuri ya mama Samia.

Makonda ni mwanasiasa anayeweka maslahi yake mbele na kuutupa ukweli ili kuridhisha matakwa yake kisiasa.

Magufuli alikuwa na mafanikio yake, na madudu yake kibao.
Magufuli alifanikiwa na SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere na umeme, vituo vya afya nchi nzima, Daraja la Busisi na mengine lakini Mafuguli alikuwa dikteta.
Japo ni kweli JPM alikuwa dikteta, Tanzania tulipofikia tulimuhitaji dikteta mzalendo, tukamlilia Mungu, akatupatia JPM
Mama Samia kwa sasa ameipaisha nchi kiuchumi, na anasahihisha madudu ya Magufuli.
Naunga mkono hoja
 
Anafosi wafanane ,mjinga kweli.

Magufuli aliharibu Kila kitu ikiwemo Ajira anasingizia kujenga bwawa la umeme na SGR Kila siku.

Mbona Samia ameweza yote na maelfu ya Ajira Kila siku?

Ukweli ni kwamba Magufuli hana maarifa ya kutafuta hela tofauti na Samia,ndio maana Samia kaweza kusukuma mambo mengi Kwa wakati mmja na Kwa mda mchache zaidi.
Ilani ya awamu sita iliandikwa lini?
 
Anafosi wafanane ,mjinga kweli.

Magufuli aliharibu Kila kitu ikiwemo Ajira anasingizia kujenga bwawa la umeme na SGR Kila siku.

Mbona Samia ameweza yote na maelfu ya Ajira Kila siku?

Ukweli ni kwamba Magufuli hana maarifa ya kutafuta hela tofauti na Samia,ndio maana Samia kaweza kusukuma mambo mengi Kwa wakati mmja na Kwa mda mchache zaidi.
Hayo maelfu ya ajira yako wapi?
Au unataka kututhibitishia ulivyo kuwa "Cheti Fake"?
 
Yako mengi sana ,saizi wale jobless wa kuznia 2016-2021 wengi wao wamepata kazi.

Wengine Hawa hapa 👇
Screenshot_20240325-124528.jpg

Hao unaowaita cheti fake Samia kawalipa mafao , Magufuli alishindwa 😁😁
 
Anafosi wafanane ,mjinga kweli.

Magufuli aliharibu Kila kitu ikiwemo Ajira anasingizia kujenga bwawa la umeme na SGR Kila siku.

Mbona Samia ameweza yote na maelfu ya Ajira Kila siku?

Ukweli ni kwamba Magufuli hana maarifa ya kutafuta hela tofauti na Samia,ndio maana Samia kaweza kusukuma mambo mengi Kwa wakati mmja na Kwa mda mchache zaidi.
Katika nafasi ya punda wa kubeba mzigo, Mgufuli aliweza nafasi hiyo, lakini ukuu wa nchi, NO!.
 
Back
Top Bottom